jamani nisaidieni

dingi

Member
Mar 13, 2011
6
0
mke wangu akifanya kosa,.hapendi kuambiwa,nikimwambia ananuna wiki nzima,nikicheki simu zake nakuta msg za mamake akimpa pole na ushauri kana kwamba nimekosea kumwambia makosa yake,tena pasipo hata kuniuliza ili abalance story,naombeni ushauri jamani maana sina amani nyumbani kwangu mwenyewe.
kibaya zaidi ni kwamba anarudia makosa yaleyale,sijui ni makusudi?au anapenda tuvurugane tu
 
Dingi, pole sana mkuu, jinsi ninavyo ona mimi mke wako ni katika wale watoto waliozoea kudekezwa na wazazi wao tangia wakiwa wadogo...! Na hayo ni matokeo yake, chakufanya hapo ni kukaa naye chini na kuongea naye kiustaarabu bila kumfokea...! Kama ataendelea na tabia ya kununa basi cha kufanya ni kumwita mama yake mkae pamoja nyote watatu na muyazungumze kiuwazi na kutoa dukuduku lako. Naye ikiwezekana aseme kile kinachomfanya kununa nuna na kisha mama mkwe naye atoe nasaha zake.

Baada ya hapo kama hali itaendelea basi cha kufanya ni kuwaita wazee wako, pamoja na wazee wake mkeo na kuwaeleza tatizo lililopo kati yako wewe na mkeo na hatua ulizochokuwa kabla ya hapo.

Nakutakia kila la kheri kwenye ndoa yako.
 
mmh!pole..sasa na wewe ungejuaje anamwambia mama yake kama usingechokonoa simu yake?mpe privacy na yeye akaa!

Mkalishe chini mwambie hupendi anavyonuna na vijitabia vyake usivyovipenda..mana kununiwa wiki nzima duuh..mwanamke gubu huyo.
haya ukiamua kutafuta wa kukufurahisha nje je atanuna au atacheka..wanawake bwana..twajitafutia matatizo kisha twalia aa
 
Inategemea unamwambia vipi unamfokea au kwa dharau hebu badili mbinu kwa kuongea nae polepole na mpe nafasi nae ajibu.Kuhusu kuangalia simu yake acha kabisa ni tabia mbaya mpe uhuru kwenye simu yake.
 
Inategemea unamwambia vipi unamfokea au kwa dharau hebu badili mbinu kwa kuongea nae polepole na mpe nafasi nae ajibu.Kuhusu kuangalia simu yake acha kabisa ni tabia mbaya mpe uhuru kwenye simu yake.

Inawezekana uko sawa Uporoto kuhusiana na njia anayotumia kumwambia....ila vyovyote vile hamna hata moja inayompa sababu ya kwenda kushitaki kwa mama yake.
Huyo dada anaonekana ana utoto mwingi....mkalishe chini umweleze kwa utaratibu kwanza ni jinsi gani tabia ya kununa na kukimbiza maneno kwa mama yake sio nzuri.....then awe tayari kusikia kuhusu makosa yake na kuyakubali!!!Akiendelea hivyo ipo siku yeye ndo atakuja kuomba msaada wa mawazo hapa JF na inawezekana ikawa too late then..mabadiliko ni kwa faida yake binafsi!!!!
 
mke wangu akifanya kosa,.hapendi kuambiwa,nikimwambia ananuna wiki nzima,nikicheki simu zake nakuta msg za mamake akimpa pole na ushauri kana kwamba nimekosea kumwambia makosa yake,tena pasipo hata kuniuliza ili abalance story,naombeni ushauri jamani maana sina amani nyumbani kwangu mwenyewe.
kibaya zaidi ni kwamba anarudia makosa yaleyale,sijui ni makusudi?au anapenda tuvurugane tu

Kama umeyumia mdomo haijasaidia anza kumzabua vibao anune mwezi mzima baadae atajirekebisha
 
pole sana mkuu,ila ndoa yatakiwa nyie wawili ndio mnatakiwa kuwa msingi wa mahusiano yenu
wazazi wakiingilia mmekwisha
 
Hiyo tabia kaanza lini, kama kabla hujamwoa alikuwa hivyo basi tegemea hayo kuendelea la basi kajifunzia kwako na wewe ndo tatizo. Cha kufanya tafuta siku yuko na furaha sana kaa nae ikibidi nje ya home, jiweke mdogo then muulize kwa lugha laini tu mambo yatajipa utapata majibu yoote.
 
Kama umeyumia mdomo haijasaidia anza kumzabua vibao anune mwezi mzima baadae atajirekebisha

Fidel80 you are jiniasi, Yaweza kuwa altenative Broda, he don't have to ignore it... :lol::lol:
 
Tunza mihasirayako, take some few days kumbembeleza, fanya kama huna hasira at all, mdekeze mfanye ajisikie yupo juu you will find your balance na Usiulize kwa ukali, usijifanye wewe unajua kilakitu... take sometime mfanye au mjengee mazingira ya kuona wewe ndio mtatuzi wa matatizo yake yote, you will enjoy.. achana na mambo ya vikao matatizo yenu wa kuyamaliza ni nyinyi wenyewe, mtajichora na vimatatizo vyenu vya kitoto (kununa wiki)
 
hebu jaribu kufuata kwanza ushauri wa X-Paster!
Pole kaka maana hicho chuo kinahitaji upole na subira!.
 
Dingi, pole sana mkuu, jinsi ninavyo ona mimi mke wako ni katika wale watoto waliozoea kudekezwa na wazazi wao tangia wakiwa wadogo...! Na hayo ni matokeo yake, chakufanya hapo ni kukaa naye chini na kuongea naye kiustaarabu bila kumfokea...! Kama ataendelea na tabia ya kununa basi cha kufanya ni kumwita mama yake mkae pamoja nyote watatu na muyazungumze kiuwazi na kutoa dukuduku lako. Naye ikiwezekana aseme kile kinachomfanya kununa nuna na kisha mama mkwe naye atoe nasaha zake.

Baada ya hapo kama hali itaendelea basi cha kufanya ni kuwaita wazee wako, pamoja na wazee wake mkeo na kuwaeleza tatizo lililopo kati yako wewe na mkeo na hatua ulizochokuwa kabla ya hapo.

Nakutakia kila la kheri kwenye ndoa yako.
Kweli humu kuna wazee khasa!
 
aisee mie nina matatizo nini? siwezi na sijawahi kushataki na sitarajii kufanya hivyo tena kwa mambo ya kitoto2, tutakunjana wenyewe na kunyooshana wenyewe ndani kwa ndani, nikienda kwa maza labda hali ni mbaya kweli kweli!
 
Ndio ukubwa wenyewe huo
 
mke wangu akifanya kosa,.hapendi kuambiwa,nikimwambia ananuna wiki nzima,nikicheki simu zake nakuta msg za mamake akimpa pole na ushauri kana kwamba nimekosea kumwambia makosa yake,tena pasipo hata kuniuliza ili abalance story,naombeni ushauri jamani maana sina amani nyumbani kwangu mwenyewe.
kibaya zaidi ni kwamba anarudia makosa yaleyale,sijui ni makusudi?au anapenda tuvurugane tu
pole mkuu , mama yake ndiyo anampa kiburi huyu, mwambie mambo y andani aache kuyatoa nje au vipi mchenjie
 
Badili style ya kumweleza hayo matatizo yake!!! Mweleze kwa upendo. Mvute karibu kuliko kumweka mbali kwa sababu ya makosa yake.

Matokeo ya kumweka mbali ndio hayo ya kutafuta faraja kwa mama yake.
Mwambie ktk hali ya kumfundisha sio kumfokea na kumlaumu!!! Barikiwa na uwe na Ndoa yenye furaha daima.
 
Mmh!
Pole, mi naona umwambie mama mkwe wako aelewe hali ikoje pande zote mbili.
Kwasababu yupo karibu na mwanae atamkanya.
 
mkuu pole sana ... kawaida ndoa ikishaingiliwa na ushauri wa mama mkwe / dada / kaka / wifi au mashemeji then amani na upendo ndani ya nyumba kutoweka ni suala la muda tu ... kiburi kikizidi mrudishe kwao akamsimulie mama yake matatizo yenu ya ndoa vizuri!! akirudi huko akili itamkaa sawa!! inawezekana nawe pia unamkwaza mkeo lakini tatizo hapo ameshindwa kuwasilisha maudhi yake kwako ... tumia akili ya ziada kutambua kosa lako na ujirekebishe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom