Jamani nisaidieni mwenzenu - lesseni yangu

kaburunye

JF-Expert Member
May 12, 2010
672
74
Wanajamvi naombeni ushauri wenu nifanye nini. Wiki iliyopita traffic mmoja alinikamata kwa kuwa road licence ya kigari changu ilikuwa imeisha. Akaniambia ananipeleka kituoni na tulipofika kituo cha mabasi cha salender akasema nipaki pembeni. Baada ya maongezi ya hapa na pale na kuonekana kuwa mazingira ya mimi kutoa rushwa ni magumu basi akachukua leseni yangu na akaniandikia notification ili nikalipe faini na baadae nimletee risiti anirudishie leseni yangu. Kwa sasa ndo nimepata pesa ya kulipia road licence (mwisho wa mwezi) na nataka kesho nikakate. Mpango wangu ni kuwa nikishakata road licence nimwibukie traffic anipe leseni ila nahisi atanidai risiti ya faini ambayo kwa kweli siko tayari kuilipa baada ya kuwa nime-renew road licence yangu. Wadau mnanipa mbinu gani ya kiufundi ili huyu traffic nimfunge goli la mkono??
 
Mkuu usirudie tena hicho kitendo, Trafic hawahusiki kabisa na driving licence wao wako hapo kutekeleza sheria za barabarani, ni makosa makubwa Trafic kuchukua leseni yako, ukishaandikiwa notification inakupasa ndani ya mwezi mmoja uwe umelipia, kama unamjua inakupasa umlipoti achukuliwe hatua za kinidhamu
 
Kamanda wangu kituko kwa kweli hata najilaumu sana kufanya kituko cha kumpa leseni yangu. Yaani sijui akili yangu ilienda mapumziko kwa mda maana baada ya kuondoka ndo nikakumbuka kuwa nimefanya kituko. kwa hiyo nifanyeje kituko?
 
Back
Top Bottom