Jamani nimsaidiaje uyu Msichana?

Ngaliba Dume

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,710
3,669
Wasalaam ndugu wapendwa.. Nina mpenzi wangu kwa zaidi ya miaka mitatu,tulifahamiana wakat huo yeye akiwa bado chuoni,nilimpenda kweli na yeye nafikir alinipenda..tumeendelea kwa furaha muda mrefu,lakini badae nikaja kugundua ana mtu uko kijijini kwao,ni mpenzi wake toka wakiwa secondary,ila jamaa ni ticha ya primary anampenda sana uyu mdada...nilipogundua nilifuatilia bila mpenzi wangu kujua..badae nikamwambia...Alilia sana,akakiri kuwa jamaa anampenda sana ila yeye hamfeel jamaa..ulikuwa eti ni utoto wa kishule shule,lakin jamaa anafahamika kwa wazazi wa mwanamke,amemsaidia sana wakati mwanamke akiwa chuo..boom likiisha jamaa ana-supply mkwanja. Lakin mwanamke anasema jamaa si wa ndoto zake,ni kweli alimsaidia na huwasaidia pia wazaz wake uko kijijini..lakini haisi kuendelea kuwa nae!jamaa nae analalamika,anahuzunika kuwa kaghalamia na mshahara wake wa ualimu..hawezi kumwacha msichana Mi sitambuliki kwao,japo msichana ananipenda,analia sana..wiki jana nimempa msimamo kuwa sitaendelea nae!frankly speaking alizimia around 45 minutes...analalamika kanipenda,hajisikii kuendelea na jamaa..na mimi namwonea huruma mwalimu(boyfriend wake),ananung'unika sana,analalamika kaibiwa mjini na mbaya zaidi jamaa hana access ya kuja mjini...NIMEAMUA KUJITOA NIMWACHE JAPO NILIMPENDA SANA NA HAPA MJINI NIMEMPA KAMPAN SANA YA KUPATA KAZI!
 
Na Eric Shigongo, itaendelea kwenye kitabu kitakacho toka hivi karibuni.
 
Linaweza kuwa jambo la busara kuachana naye. Masikitiko ya huyo jamaa aliyemgharimia yanaweza kuifanya ndoa yako isiwe na amani wala raha. Ningekuwa wewe, ningeachana naye tu. Wanasema mtendee mwenzako kila ambacho ungependa utendewe. Huyo binti inaonekana hivi sasa kinachomsumbua ni tamaa tu. Anaona status yake ya sasa haiendani na ya yule mwalimu wa shule ya msingi. Shame on her.
 
namwonea sana huruma mwl hataweza kumuoa huyo dada though kamgharamia. hata akimuoa ndoa haitakuwa ya raha kwa wote wawili. mdada tayari kesha elimika anaona hapaswi kuwa na mwl tena. mwl bd anapenda. mkuu hongera kwa kuwa na msimamo, naona malalamiko ya mwl yangewaharibia ndoa yenu.
 
Yaweza kuwa alimpenda huyo jamaa kwa ajili ya msaada alokuwa anampatia yeye na wazazi wake pia. Kumpiga chini ni msaada tosha na atajifunza kurudisha upendo kwa huyo jamaa yake, na atajifunza nini maana ya mapenzi!
 
Hana mapenzi ya kweli...amekucheat wewe na mwalimu. She can't make a gud wife to any of u...
 
Mpige chini kwani inaelekea akiendelea kuwa na wewe baada ya muda akipata mwenye msaada zaidi kitakachofuata ni wewe kupigwa chini pia lawama kutoka kwa jamaa wake wa zamani zitakua zikikuangukia wewe
 
Simfagilii huyo dada wala nini...siku zote kama unajua huna mpango na mtu usimtumie na kumpa matumaini yasiyofaa!!

Mchukue na wewe siku aje kumlilia mwingine hivyo hivyo....
 
Linaweza kuwa jambo la busara kuachana naye. Masikitiko ya huyo jamaa aliyemgharimia yanaweza kuifanya ndoa yako isiwe na amani wala raha. Ningekuwa wewe, ningeachana naye tu. Wanasema mtendee mwenzako kila ambacho ungependa utendewe. Huyo binti inaonekana hivi sasa kinachomsumbua ni tamaa tu. Anaona status yake ya sasa haiendani na ya yule mwalimu wa shule ya msingi. Shame on her.
Umetoa ushauri mzuri sana. Ubarikiwe na uwe na j2 njema!
 
Tatizo huwa tunasahau tulikotoka, mwachie mwalimu chake, japo navoona huyo msichana anaweza airudi tena huko kijijini kwa mwalimu wake, sababu keshaharibu
 
Back
Top Bottom