mtanzania in exile
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 1,325
- 1,181
Habari wanajamii,
Nina tatizo zito na naomba ushauri wenu. Stori ni ndefu lakini nitajaribu kuifanya ndogo na ieleweke.
Miaka kama mitatu hivi iliyopita nilihamia katika mji mwengine kikazi na katika harakati za kutafuta nyumba nilikutana na kijana wa kitanzania ambae alinisaidia sana ikiwa na pamoja na kunipa ushauri wa sehemu gani ni safe zaidi kuishi na sehemu gani ni za kuziepuka katika mji huu. Baada ya hapo tukawa marafiki wakubwa, akanijulisha kwa mkewe na mwanawe, pia kwa ndugu zake wote waishio hapa. Tumezoeana sana kiasi kuwa tunatoka sana pamoja, tunatembeleana,, tunasaidiana matatizo, na mambo mengi tu, kwa ufupi tuko close sana tu.
Katikati ya mwaka jana mke wa rafiki yangu alianza kuniuliza masuali juu ya mumewe, kama jee najua ana nyumba ndogo, na masuali hayo yalikuwa akiyaleta kila tukikutana. Kusema ukweli huyu rafiki yangu siamini kama ana nyumba ndogo kwa namna anavyompenda mkewe na mwanawe, daima mazungumzo yake ni kuhusu maisha mazuri na ya furaha aliyonayo na baraka aliopewa ya kuwa na mke na mtoto. Nami nimemueleza mkewe na kumhakikishia kwa kadri ninavyojua mimi mumewe hana nyumba ndogo, na daima anapokuwa na mimi hajawahi kuongea nyumba ndogo au kufafata wanawake mitaani. Baada ya miezi michache maongezi yakabadilika na sasa akawa tukikutana anasema ana uhakika kuwa mumewe ana nyumba ndogo kwa sababu hamshuhulikii chumbani na ni kwa muda mrefu sasa na pia yuko cruel na hata alishawahi kumpiga. Nilimshauri azungumze na mashemeji zake, lakini alikataa na kusema kuwa mashemeji zake watafurahi mno kwani hawampendi na walikuwa against na ndo yao toka siku ya mwanzo. Nilijitolea kuwa nitazungumza na rafiki yangu, lakini pia akakataa kabisa idea yangu.
Anyway, hivi karibuni alifika nyumbani kwangu bila ya taarifa, na baada ya muda mchache tu wakuwepo kwangu akasema kuwa anavutiwa na mimi na anataka kufanya mapenzi nami there and then, na akajileta karibu yangu huku akipunguza mavazi yake. Niliruka kama baruti na kuwa mkali niwezavyo na kumuonya kwa kitendo alichifanya. Alianza kulia na kuomba samahani, baada ya kumtuliza na kumsihi asirudie tena tulikubaliana tusahau yaliopita na hakuna haja ya kumueleza mumewe na akaondoka zake.
Mara baada ya kuondoka akanitumia message kwenye mobile yangu kusema kuwa bado ananifikiri na hawezi kunitoa kichwani mwake. Nilimjibu kuwa awache kuniandikia message za namna hii na kumkumbusha kuwa mimi ni rafiki mkubwa wa mumewe na isitoshe mumewe anampenda sana tu. Hata hivyo hiyo haikuwa dawa text zilikuwa zinazidi kuja nami nikizidharau kuzijibu nikitegema kuwa atachoka, lakini haikuwa hivyo. Kuna siku nikakutana nae mitaani na akasema kama siko tayari kuwa na affair nae basi atavunja urafiki wetu mimi na mumewe kwa kumwambia kuwa nilimjaribu siku moja, na akasema kwa namna anavyomjua mumewe na anavyompenda atamuamini tu. Niliamu to call her a bluff na nikasisitiza kuwa haitatokea hata siku moja nikamsaliti rafiki yangu.
Tatizo ni hili, hivi karibuni rafiki yangu amekuwa ananikwepa kwepa sana, na hata tukizungumza mazungumzo ni mafupi na hayuko na mood kama za zamani. Hata simu sin sana kunipigia na ninapompigia simu haidumu hata dakika tano wakati zamani tulikuwa tunakaa kwa muda mrefu mno. Juzi nimekutana na mdogo wake na yeye pia amekuwa na mood za maajabu kwangu. Nahisi huyu mwanamke ametimiza ahadi yake na amemwambia uongo mumewe juu yangu. Kwa sasa nataka kumuweka chini rafiki yangu na kutaka kujua ni kwa nini amebadilika.
Jee ndugu zangu, ikiwa rafiki yangu ataniambia sababu ni kuwa nimemjaribu mkewe, mimi nifanyeje? nimueleze ukweli? nimuonyeshe messages zote alizonitumia mkewe? Jee ni lipi bora nivunje urafiki au nivunje ndoa ya rafiki yangu? nahisi nikikaa kimya watu wataanza kusema sema na jamii ya watanzania hapa soon wote watajua na kuniona mimi kama mhaini mkubwa. Naomba ushauri wenu, jee nifanyeje?