Jamani ni umri gani sahihi wa kuoa?

Yan nikupongeze sana kama ni kweli umefika umri huo bado ni bikra! Watu kama ninyi ni adimu sana kuwapata enzi hizi.
Kinachonifurahisha ni kwamba wewe mwenyewe umeshajua kwamba sasa ni umri wa kuoa ndiyo mana umekua na wazo hilo la kuuliza hapa JF! Kwa kawaida kama usingejua umefika umri wa kuoa wala usingeuliza. Kimsingi umri wa kuoa ni baada ya kutimiza umri wa mtu mzima (18yrs) ila sasa inategemea na ukomavu wa akili (yan kuweza kutunza familia) unaweza ukawa na miaka hata 40 ila akili bado ikawa ya kurukaruka na ukashindwa kutunza familia. Ila kwa wewe nafikiri umri wako unafaa na umeonyesha kukomaa kiakili baada ya kutafakari na kuleta jambo hii kwa wanaJF.
Mia nakupa big up sana anza kutafuta mchumba sasa ONYO usikute ndiyo mbinu zako za kutafuta dada wakifikiri wewe bikra kumbe FATAKI!!!!!
tasante sana kwa ushauri wako ..ushauri umeenda shule sana na moja kwa moja inaonyesha kuwa wewe ni mtu mwenye hekima nyingi sana God bless you ..nimeamini kweli hii ni GT .salute
 
Trustme umeongea vyema sana
Na hilo ndio la muhimu maana kinachotakiwa ni ile akili kukomaa na kujijua kuwa sasa anaweza kukaa na familia yake na wakaunda familia
Maana wengine umri unaweza kuwa mkubwa ila bado akili ya kujua kuwa ana familia na vipi aishi na familia yake inakuwa haipo
Ni jambo la muhimu kama ameweza kujitunza kiasi hicho na ni wakati wake sasa kukaa na kuunda familia
pamoja mkuu ..nimekupata
 
Mmmh! Sijakuelewa hapo. Unasema huna msichana na wala hujawa na hisia za kuanza kumtafuta! Inakuwaje mwanamume aliyekamilika wa miaka 30 hana msichana wala hisia za kuanza kutafuta????? Katika hali ya kawaida unaweza ukawa huna msichana lakini huwezi kutokuwa na hisia. Hebu niweke sawa hapo. Ina maana unataka tu kuoa kwa sababu watu wote wanaoa? Au kwa sababu unajisikia kuoa?? Hakuna umri juu ya lini uoe baada ya kubalehe. Mipango yako ya maisha inaweza kukuchelewesha au kukuwahisha kuoa.
 
umeniacha njia panda kaka

Mkuu muda wako kwa sasa unatafuta mwenzi wa maisha na sio tena kutamani wanawake kila anayepita unamtaka
Kw ahapo wewe unatafuta mwenzi utakayekuwa nae maishani mwako na sio kutamani
Ndo maana amekuambia kuwa utofautishe kati ya kupenda na kutamani
 
naona uzee unaninyemelea wandugu sina mshichana na wala sijawa na hisia za kuanza kutafuta na ki finacial nipo safi na kielimu pia ..but i realy dont know the age of getting marriage.. nakaribia kuwa na miaka 30 baada ya mwaka mmoja ..je nitafute mke au bado niendelee kuwa bachela?
kuna tatizo lolote kubaki hivi ..msaada wenu watu wangu unahitajika hapa ..msinirushia madongo kwani mawazo yenu as a great thinker yatanijenga na wala sio kunibomoa ..
thanks guys and have a nice time:

kwa mjibu wa wana social psycologist wanasema:-
1. 18-25 ni kuoa
2. 25-30 kuzaa watoto, kutengeneza familia
3. 35-45 kuendeleza familia yako kwa kuwapa shule inayostahili, hata kama ukifa waweze kujisimamia.
4. 45-55 ni kujiandaa kustaafu na kupumzika kufanya kazi za kuzalisha mali moja kwa moja.
5. 55-65 umeshastaafu, unakula pension yako, watoto hawakutegemei kwa lolote zaidi ya ushauri, na unaweza ukaingia kweye mabaraza ya maamuzi ili kujenga misingi bora ya wajukuu zako kuishi vizuri.

hivyo kama hujaoa na huna sababu ya msingi, tayari unakaribia kuchelewa, kwani kinyume na hapo kuna uwezekano wa wewe kutokuona maendeleo ya wanao hasa kielimu na mambo mengine ya msingi. Fanya hima, oa, anzisha familia ili kufikia 35, uhangaike namna ya kuwasomesha tu.
 
kwa mjibu wa wana social psycologist wanasema:-
1. 18-25 ni kuoa
2. 25-30 kuzaa watoto, kutengeneza familia
3. 35-45 kuendeleza familia yako kwa kuwapa shule inayostahili, hata kama ukifa waweze kujisimamia.
4. 45-55 ni kujiandaa kustaafu na kupumzika kufanya kazi za kuzalisha mali moja kwa moja.
5. 55-65 umeshastaafu, unakula pension yako, watoto hawakutegemei kwa lolote zaidi ya ushauri, na unaweza ukaingia kweye mabaraza ya maamuzi ili kujenga misingi bora ya wajukuu zako kuishi vizuri.

Hivyo kama hujaoa na huna sababu ya msingi, tayari unakaribia kuchelewa, kwani kinyume na hapo kuna uwezekano wa wewe kutokuona maendeleo ya wanao hasa kielimu na mambo mengine ya msingi. Fanya hima, oa, anzisha familia ili kufikia 35, uhangaike namna ya kuwasomesha tu.
loh hapo redi ni lipo kumbe ni noma mama yangu weeeeeeeeeeeee
 
loh hapo redi ni lipo kumbe ni noma mama yangu weeeeeeeeeeeee

kama ndo umri wako na hauna mtoto, imekula kwako. zaidi utatuongezea watoto vibaka, kwani kwa mjibu wa life expectancy ya mtanzania ya 47 yrs, umeshavuka na unasubiri kujifia tu. pole sana ndugu
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom