Jamani nauza trekta Massey Ferguson MF 375

mito

JF-Expert Member
Jun 20, 2011
10,513
10,404
Wakuu nina trekta langu naliuza.
Ni Massey Ferguson MF 375 horse power 75, ni zuri sana kwa ardhi ya TZ. Lina hali nzuri sana. Nilinunua jipya mwaka 2008, nikalitumia kwa miaka miwili tu, nikapata kazi ghafla nje ya nchi, usimamizi ukadorora uchakachuaji ukawa mwingi, nimeamua sasa niliuze tu. Hivi sasa lipo tu linafanyakazi ndogo ndogo tu za nyumbani. Lina kila kitu, yaani jembe, harrow, na tela la kubinua lenyewe (hydraulic trailer). Tafadhali serious buyer tu ndo ani-PM. Bei ni maelewano!

Angalizo: natanguliza samahani kwa atakayelihitaji kwa haraka kwani kwa sasa niko nje ya nchi, ila nategemea kuwa nchini tar 1 September hadi tar 29 November 2012. Kwahiyo kama ni kuliona au kulichukua, itabidi uwe mvumilivu kidogo kila kitu kifanyike ndani ya muda huo.
 
utusamehe kwa tunaolihitaji manake bila BEI, PICHA,MAHALI LILIPO.......n.k
na kama umeamua kutangaza weka wazi vyote ili serious buyer yeye ndo aku-pm
 
Mahesabu, trekta liko Tanga (Muheza), kama nilivyosema bei ni maelewano, picha nilizonazo hapa ni zile za mwaka 2008 wakati nalinunua, hivyo hazitakupa hali halisi ya trekta lilivyo sasa (na mimi sitaki kuongopa).
 
Bei maelewano maana yake nini? Toa bei unayotaka ndiyo negotiations zianze, lakini kama unauza tractor, ambayo picha yake hatujaiona, kwa bei isiyojulikana na tractor yenyewe haitapatikana mpaka September, ndugu yangu huoni kama kidogo hiyo ni stretch?
 
Sijui anaogopa nini, mwenye tractor hebu jilipue tujue wapi pakuanzia mkuu. Tupe bei, na hizo picha hata kama ni za zamani tutafanya kupiga hesabu kabla ya kuliona!! anyway nakuPM
 
Muuzaji naomba nikurekebishe kidogo pengine uko nje ya nchi muda mrefu na hujui kinachojiri TZ kwa sasa.
Kuwa kwako nje hakuwezi kuzuia biasara hata kidogo.
1. Huko Muheza kuna watu kibao wana simu zina kamera, watume wakupigie picha na kukurushia kwenye email.
2. Ili mtu afanye biashara nawe na mlipane, hana haja ya kukutana nawe physically anaweza kukutumia hela huko huko uliko bila kuchomoka kwenye komputa yako.
3. Anayehitaji trekta leo hataweka pesa zake kukusubiri wewe urudi hiyo septemba, atawekeza sehemu nyingine sasa hivi bongo michongo kibao.
So kama una nia ya kuuza, uza leo na si miezi kibao ijayo. Nawasilisha.
 
Mkuu asante sana kwa ushauri wako, akipatikana kwenye nia nitafanya hivyo kama na yeye atakubali
 
huyu bwana anauza sitaki nataka chukua 5m nikusubiri sisi huku shy hilo kwetu ni mali.
 
Back
Top Bottom