Jamani Nauliza Nipate Kujua..... Ilikuwaje?

Kisa cha mtema kuni:
Huyu jamaa alienda kukata kuni porini,siku zote huwa na kawaida ya kukata kuni za chini lakini siku hiyo hazikuwepo.Jamaa akaamua kupanda juu ya mti ili akate kuni za juu,sasa ikatokea kuwa tawi alilokua anakata ndilo alilokalia bila ya yeye mwenyewe kufahamu.Nafikiri unafahamu kilichomtokea baada ya kukata hilo tawi na hicho ndicho alichokiona..
 
Hii methali inatokana na hadithi au simulizi ya mkata kuni (Mtema kuni... Hiki ni kiswahili cha zamani).

Kwa ufupi inasimuliwa kwamba mkata kuni alikwenda porini kwa nia ya kutema kuni (kukata kuni) kutokana na sababu anazo zijuwa yeye au kwa kuzidiwa na mawazo alipofika porini akapitiwa na usingizi (kama bado nakumbuka vizuri) ndio kwanza ulikuwa muda wa Mawio yaani jua linachomoza).

Alipokurupuka... kuangaza uku na uku shoka lake halioni, na hali anakumbuka vizuri kulichukuwa...

Yeye hakahisi labda limedondoka mahali... akaanza kulitafuta kuanzia Mawio mpaka Machweo (Kuzama kwa jua Wakati wa Magharibi) Mwisowe akajikuta amechoka na shoka halionekani.

Akaamua kukaa chini ya mti ili apumzishe akili na kutafakari upya wapi alipolidondosha shoka lake. Wakati anajiandaa kukaa chini kuangalia begani kwake analiona shoka lake... kumbe alikuwa amesahau kuwa shoka lilikuwa amelining'iniza begani kwake...

Hapo ndipo palipo patikana huo msemo wa "Utakiona cha mtema kuni... Kutafuta shoka wakati lipo begani."

kulikuwa na hadithi ndefu kidogo ya mtema kuni

mtema kuni maana yake anaechanja kuni......

huyu sikumbuki vizuri lakini mwishowe aliuwawa na mfalme..

alituhumiwa kumuambia uwongo mfalme..

yeye alikutana na kichwa cha binaadamu kinaongea....

na akaenda kumwambia mfalme..

mfalme akafunga safari ya kukiona hiko kichwa..
kufika kichwa hakikuongea..
mfalme akaamuru mtema kuni auwawe..

baada ya kuuwawa ,kichwa kikazungumza.....

ni hadithi ndefu nimeikatiza katiza

athuman ni kama imetumika kuwakirisha jina la binadamu kwani mungu huwezi kumfananisha na binadamu
binadamu akipewa nafasi ya kugawa ridhiki anaweza kupendelea lakini mungu hafanyi hivyo
mtema kuni siku moja akiwa katika shughuli zake za kukusanya kuni zilizo kauka porini akajikuta amefunga mzigo wake wa kuni na boooonge la nyoooka ambalo baadaye likamuua kwa kumviringa kuanzia kichwani hadi mguuni
mkaidi yeye kutokana na tabia yake mbovu hawezi pata nafasi ya kukaribishwa dinner/lunch na individuals ila siku ya sikukuu hakuna anayejari nani kakaribishwa na nani hajakribishwa ukizingatia sisi waafrika sherehe hapo zamani ilikuwa inafanyika bila mwaliko wa kadi au kitambulisho
AAAAH MENGINE MNISAIDIE NATOKA KIDOGO

Kisa cha mtema kuni:
Huyu jamaa alienda kukata kuni porini,siku zote huwa na kawaida ya kukata kuni za chini lakini siku hiyo hazikuwepo.Jamaa akaamua kupanda juu ya mti ili akate kuni za juu,sasa ikatokea kuwa tawi alilokua anakata ndilo alilokalia bila ya yeye mwenyewe kufahamu.Nafikiri unafahamu kilichomtokea baada ya kukata hilo tawi na hicho ndicho alichokiona..

Babu ako konfyuzdi na hiki kisa cha mtema kuni.....

Hadithi zimekuwa nyingi mpaka nashindwa kuelewa ni ipi hasa ya ukweli
 
Kabla sijakugongea, ngoja kwanza:
1. Inaeleweka na umeielezea inavyostahili, lakini kwanini lilitumika jina la ATHUMANI? Kwanini haikuwa Lizzy, Ashadii, Asprin et el? Hiyo Athumani iliingiaje hapo? Huoni lazima kutakuwa na hadithi flani ambayo labda hatuijui (damn utandawazi, mababu zetu wa siku hizi hawasimulii hadithi...tunagongana nao gesti na kuishabikia Manchester United).....Hii ATHUMANI lazima itakuwa na chanzo bana.... ndo naitaka hapa kama Boss na Xpaster walivyotoa hadithi ya Mtema kuni hapo juu.
2.Nayo ni sawa na inafahamika hivyo. Kwanini afaidi siku ya IDDI peke yake wakati kuna Xmass, pasaka, maulid, Muungano, Uhuru day etc etc? Hauoni hapo pia kuna kahadithi ka kusimuliana?
Mkuu, Asprin... kwanza kabisa cheo cha ubabu, tunakuvua, kwani kwenye thread hii ndio umedhihirisha kuwa wewe jina la babu si cheo chako bali ni jina lako nina maana kuwa wewe unaitwa babuu (joke). Ah ah ah ah anyway tuendelee...! Kila lugha ina asili yake na athari zake kwa jamii, lugha ya kiswahili ilianzia Pwani ya Afrika mashariki na ndiko kwenye hayo majina yenye asili ya Kiarabu, kihindi na Kiajemi (Iran). Sasa ni aghlabu sana kukuta watu wa pwani wa enzi hizo kutumia majina ya watu wa Kimagharibi (uropa), kama John, Brown n.k.

Hii Metahli ya Mungu si Athumani, inawezekana kuwa huyu mtu alikuwa maarufu sana au alikuwa ni mwenye uwezo na majigambo kwa watu, kiasi ya kupelekewa kuchukiwa kwa kiburi chake, na pale alipopatikana, mtu mwingine kupata kitu au mafanikio ambayo wengi walifikiria bila ya Bwana Athumani basi uwezi, ndio wakawa wakisema Mungu si Athumani umpa kila mtu bila ya upendeleo si kama Bwana Athumani ambaye kwa ubinadamu wake amejikuta anapendelea wale tu anao wataka yeye.

Vile vile kwenye Methali ya Mkahidi hafaidi mpaka siku ya Iddi...! Neno Iddi linatokana na neno la Kiarabu Eid. Ikimaanisha Sikukuu, tamasha au sherehe... Kwa maana hiyo hiyo hata sikuku ya christmas inaitwa Eid ul-Milad (عيد الميلاد) yaani sikuku ya kuzaliwa Yesu, nchi kama Lebanon zinasheherea hizi sikukuu, vile vile kwa faida zaidi siku ya Pentecost inaitwa ‘Īdu l-‘Anṣarah. Kwa hiyo hizi hazina tofauti na sikukuu za Eid ul Adha au Eid ul-Fitr.
Kwa hayo machache nadhani utakuwa umepata kuelewa japo kidogo maana ya neno idd, kwani tunajuwa kuwa siku za sikukuu au sherehe, kila mmoja ushehereka, hata wale wakorofi maana nao tunawashirikisha pia... Ndio wahenga wakasema "Mkahidi hafaidi mpaka siku ya Idi".
 
Mkuu, Asprin... kwanza kabisa cheo cha ubabu, tunakuvua, kwani kwenye thread hii ndio umedhihirisha kuwa wewe jina la babu si cheo chako bali ni jina lako nina maana kuwa wewe unaitwa babuu (joke). Ah ah ah ah anyway tuendelee...! Kila lugha ina asili yake na athari zake kwa jamii, lugha ya kiswahili ilianzia Pwani ya Afrika mashariki na ndiko kwenye hayo majina yenye asili ya Kiarabu, kihindi na Kiajemi (Iran). Sasa ni aghlabu sana kukuta watu wa pwani wa enzi hizo kutumia majina ya watu wa Kimagharibi (uropa), kama John, Brown n.k.

Hii Metahli ya Mungu si Athumani, inawezekana kuwa huyu mtu alikuwa maarufu sana au alikuwa ni mwenye uwezo na majigambo kwa watu, kiasi ya kupelekewa kuchukiwa kwa kiburi chake, na pale alipopatikana, mtu mwingine kupata kitu au mafanikio ambayo wengi walifikiria bila ya Bwana Athumani basi uwezi, ndio wakawa wakisema Mungu si Athumani umpa kila mtu bila ya upendeleo si kama Bwana Athumani ambaye kwa ubinadamu wake amejikuta anapendelea wale tu anao wataka yeye.

Vile vile kwenye Methali ya Mkahidi hafaidi mpaka siku ya Iddi...! Neno Iddi linatokana na neno la Kiarabu Eid. Ikimaanisha Sikukuu, tamasha au sherehe... Kwa maana hiyo hiyo hata sikuku ya christmas inaitwa Eid ul-Milad (عيد الميلاد) yaani sikuku ya kuzaliwa Yesu, nchi kama Lebanon zinasheherea hizi sikukuu, vile vile kwa faida zaidi siku ya Pentecost inaitwa 'Īdu l-‘Anṣarah. Kwa hiyo hizi hazina tofauti na sikukuu za Eid ul Adha au Eid ul-Fitr.
Kwa hayo machache nadhani utakuwa umepata kuelewa japo kidogo maana ya neno idd, kwani tunajuwa kuwa siku za sikukuu au sherehe, kila mmoja ushehereka, hata wale wakorofi maana nao tunawashirikisha pia... Ndio wahenga wakasema "Mkahidi hafaidi mpaka siku ya Idi".
Mkuu, hiyo bold hapo nakushauri ukai-edit mapema kabla wajukuu zangu hawajaamka LOL

Ahsante kwa kunielimisha mkuu... Kumbe Iddi = Eid = Sikukuu.... Mkaidi hafaidi mpaka sikukuu....Nafurahi na sina mashaka na ufafanuzi wako kuhusu msemo huo.

Ila hii ya Mungu si Athumani......ufafanuzi wake nimeuelewa fika. Na kiukweli hiyo ndio tafsiri yake. Ila je hakuna hadithi iliyopo ambayo inaukweli ndani yake kuwa kuna mtu alikuwa anaitwa Athumani ambaye ndo alisababisha uwepo wa msemo huu?... Naamini lazima kulikuwa na kisa cha ukweli kuhusu huyu Bwana Athumani.

Kisa cha mtema kuni nacho tuna hadithi nne tofauti mpaka sasa....... sijui ni ipi iliyo sahihi.

Babo babu......siyo babuu (ntake radhi), ako konfyuzd!
 
Ah ah ah ah, usikonde mkuu, wajukuu zako hataona hiyo kitu, nimeiwekea speacial codes ambazo wajuu wote hawawezi kuona nilicho andika, ah ah ah ah ah.

Hizi Methali ni kweli zina asili yake na vyanzo vyake, ila bado sijabahatika kuvijua baadhi, ila kama nikibahatika basi tutafahamishana tu.
 
Yaani mpaka leo bado sijapata jibu sahihi.

Ngoja nikawaulize walevi kaunta, naona magriit thinkaz wamechemsha....!
 
<br />
<br />
mmh! Unaniruhusu niende?! Kweli babu hunitakii mema.
Nakutakia mema, nakushauri usiende, fataki atakufataki yule. Habari za Mpwapwa?

Mhhhh!!! babu...unanidai nini??? ugoro au.....????!!!
Ugoro kanikataza daktari, kaniambia nile matunda na samaki........ waweza kuniletea apple? Samaki naogopa miiba......
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom