Jamani naomba mnisaidie, malaria inanimaliza!

JAK

Member
Apr 23, 2012
92
20
Natumia chandarua, lakini hazipiti wiki tatu bila kuugua malaria. Nimeisha tumia dawa za malaria (marafin, quinin injection) lakini hali inaendelea.
 
Pole sana mkuu. Lakini una uhakika ni malaria? ulipima sehemu iliyo na watu makini? Dalili je,unazo?
 
Chandarua tu hakitoshi jaribu kuyamaliza maeneo ya jirani na kwako ambayo Mbu wanaweza kuzaliana, hakikisha nyumbani kwako hakuna mbu kwa kutumia dawa na pia jiepushe kwenda sehemu ambazo Mbu wanaweza kufanya sherehe kwenye mwili wako.
 
Nenda Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS) idara ya Parasitology utapata msaada wa kutosha ili kumaliza tatizo lako kama utapimwa na kuthibitishwa ni malaria.
 
Nenda Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS) idara ya Parasitology utapata msaada wa kutosha ili kumaliza tatizo lako kama utapimwa na kuthibitishwa ni malaria.

kuna issue mbili:
je unaPata new infections? Ni muhimu baada ya kutumia dawa wiki 1 uende kupimwa tena.
Ama unatibiwa malaria haiishi? Kama una uzito wa zaidi ya 100 kgs, probably dose haikutoshi. Ongea na daktari wako.
Usisahau kuzingatia matumizi ya chandarua, kuondoa.mazalia ya mbu na kutumia anti-mosquito lotion ukiwa nje nyakati za usiku.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Napenda kukuuliza Je, una uhakika kuwa unajiepusha vizuri vya kutosha? Kama unatumia Chandarua haiwezekani ndani kukawa kuna mbu ukawa unagusana na net usiku? je hakuna maeneo unayokuwepo mbali na home ambapo kuna mbu? Mazingira ya mbu yanajulikana sana. Kama umejitahidi kwa hali zote ikiwa ni pamoja na ukitumia dawa baada ya muda mfupi inaonekana tena ni ishu inatakiwa kufanya mabadiliko. Waweza kunicheki zaidi kwa email: healthwealthfirst@gmail.com
 
Nenda Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS) idara ya Parasitology utapata msaada wa kutosha ili kumaliza tatizo lako kama utapimwa na kuthibitishwa ni malaria.

Mkuu ubungo, nadhani

1. Ni vizuri kwenda hospitali na si Parasitology dept..kwani issue kama ni Bloodslide for Malaria Parasite( B/S for Mps) inafanyika not necessarily "muhas", besides anaweza mkuu JAK anaweza kuwa hayuko Dar es salaam.

2. Ni vizuri kuzingatia ushauri wa mkuu King'asti.
 
Back
Top Bottom