Jamani namtafuta mbunge wangu nani kamwona? Je nani mwingine mwanajf anamtafuta mbunge wake?

Umenikumbusha kwenye kampeni zake mh. AIRO aliwahi kusema ''mimi sijasoma lakini nimeajili maprofesa ndio wananisadia kufanya kazi zangu, na mkinichangua watanisadia kupanga mipango ya kuwaletea maendeleo' na Shwaiba wake Peter Zakaria (moja ya matajiri kanda ya ziwa) ambae pia hajasoma kwenye kampaini aliwahi kumsemea 'JAMANI MGOMBEA WETU NI DARASA LA SABA LAKINI MAMBO ANAYOFANYA YANAZIDI ALIYESOMA, JAMANI MSICHAGUE MSOMI CHAGUENI ATAYELETA MAENDELEO' hakika wanarorya wamechagua mtu wa kuwaletea maendeleo.

Kazi kweli, unapokuwa na mbunge ambaye hajui kwa nini anataka kuwa mbunge.
 
Wadau nimekuwa nikimtafuta Mbunge wangu wa jimbo la Rorya ndugu LAMECK AIRO kwa muda mrefu, je kuna mtu kamwona? Katika kikao cha Bunge kilichopita nilimtafuta sana Bungeni lkn sikufanikiwa kumwona. Sijui ana mpango gani na wananchi wake ambao wana shida nyingi sana lkn yeye yupo kimya tu; hivi anajua kwamba Ukimwi unawamaliza wananchi wake? na hali mbaya ya uchumi je? Lameck hata kuchangia kwa njia ya maandishi Bungeni imekuwa tatizo? Je ni nani sasa anayewasemea wananchi wake?
Nakifiri kwanza tuanze kumtafuta Rais JK hivi kweli yupo!!!!!?
 
ka kumbe hapa mondo huyo anayeitwa adood,mi nilifikili abood ni mabasi yale yanayoua na kufukia abiria polini
 
Wadau nimekuwa nikimtafuta Mbunge wangu wa jimbo la Rorya ndugu LAMECK AIRO kwa muda mrefu, je kuna mtu kamwona? Katika kikao cha Bunge kilichopita nilimtafuta sana Bungeni lkn sikufanikiwa kumwona. Sijui ana mpango gani na wananchi wake ambao wana shida nyingi sana lkn yeye yupo kimya tu; hivi anajua kwamba Ukimwi unawamaliza wananchi wake? na hali mbaya ya uchumi je? Lameck hata kuchangia kwa njia ya maandishi Bungeni imekuwa tatizo? Je ni nani sasa anayewasemea wananchi wake?

Yuko buzy kwenye hotel yake Mwanza,si mlimchagua wenyewe tulieni hivyo hivyo na matatizo mpaka 2015.
 
Du!! Siamini kama huyu jamaa huwa zinamtosha, yaani hata gamba lililokufunika hakika linakucheka saaaaaana ebu zinduka acha ulofa. Kama mbuge hana jukumu katika kudhibiti maambukizi ya ukimwi hana jukumu katika kusimamia na kufuatilia michakato ya kiuchumi ya nchi yake, ebu tupe upupu wako wa masaburi unafikiri hayo ni ya nani pekee??

Yaani me mwenyewe namshangaa huyu kilaza,sasa kama mbunge anakuwa hana kazi yoyote tusingekuwa na haja ya wabunge,kweli ukiwa ccm akili yote wanaichukua.
 
Jamaa aliua ndugu yake mpaka kapata utajiri acha upuuzi wewe! isitoshe la cairo ina mkono wa mtu!
amka mkuu
jf hapa bro hakuna kufichaficha oh mkono wa mtu we eleza hiyo mikono ni ipi watu wanamsema muungwana sembusa hao maprofesa mwaga!!
 
Mie wa kwangu Zitto Kabwe, historia imeandikwa Kigoma Kaskazini kuna lami nzuri kama Nyerere road, big up Zitto kuna changamoto ndogondogo ambazo nasi tunaendelea kumsaidia ili mambo yaende

kipindi cha kampeni nakumbuka zito kama alisema anamshukuru Rais kikwete kwa kuwezesha kigoma kuwa na Lami... magwanda kipindi walicharuka humu na kumlaani zito .. wale tuliokuwa pamoja kipindi cha kampeni mpaka uchaguzi mtakuwa mnakumbuka hili ..
 
Ambao hatukufanya ajizi tunajivunia... JJ mnyika ni jembe, tumuombee mungu ampe afya njema ili aendelee vyema na majukumu yake
 
Mimi mbunge wangu wa Bukoba vijijini niliwahi msikia akichangia mara moja bungeni,badala ya kuzungumzia matatizo ya jimbo letu alikua anawalaani CDM na kusifia magamba kwa kumwezesha kuingia bungeni!!!
 
Jamaa aliua ndugu yake mpaka kapata utajiri acha upuuzi wewe! isitoshe la cairo ina mkono wa mtu!
amka mkuu

Jiulize mtu kamwua ndg yake bado unahitaji msaada kwake wewe ambaye huna hata ukoo naye? Huyu hafai tena
 
Mbunge wangu ni Mheshimiwa Spika, alikashifiwa na mnafiki fulani kuwa amewekwa na mafisadi lakini hajakanusha na hivyo katuweka njia panda wapiga kura wake kama kweli kawekwa na mafisadi au ni wivu wa kike wa yule mnafiki. Mbunge wetu alikuwa na mkwanja wa kutosha wakati wa kampeni akawanunua wapinzani wake akapita bila kupingwa, hivyo tukabahatika kuepukana na yale manguo ya kijani yenye ishara ya ufisadi. Hatuna mtu wa kupeleka shida zetu bungeni kwa vile mbunge wetu ndio anayepokea shida za wengine hivyo hawezi kujipelekea shida zake mwenyewe, itakuwa sawa na kutoa hela mfuko wa shati ukahamishia wa suruali na kusema zimeongezeka, katiba mpya ije ituokoe. Tunatarajia kumuona mbunge wetu akija kula Xmass na Mwaka Mpya, tutaserebuka naye lakini shida hatutampa yeye kwani hana kwa kusemea, yeye ni spika wa wengine.

Mh! Mna msiba mkubwa ukakosa waombolezaji.
 
Sie tuna mwarabu mmoja anaitwa Aziz Abood, inavyosemekana Ndo mbunge we2 wa jimbo la Morogoro Mjini...Huyu ndo sidhani ka atakuja kuchangia, manake kipindi cha kampeni hata ile kutamka "KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI" alikuwa hadi asome kwenye kalatasi..

Sasa nyie mlimwacha Professor mkamchagua huyo mwarabu wa Division 0 ya Forest Hill, mlitegemea nini?
 
unauliza nini hapa sasa dah ccm majanga tupu, sikia mbunge agawi pesa ila anaweza kuamasisha uchangishaji wa pesa kuhusu miradi flani na pia mbunge anaweza kuzuia ukimwi kwa kuamasisha jamii kwa kutoa elimu ya utambuzi. Sawa Ritz.

Kazi ya mbunge ni kugawa pesa? kazi ya ubunge ni kuzuia Ukimwi? Kazi ya mbunge kuinua uchumi?
 
Wadau nimekuwa nikimtafuta Mbunge wangu wa jimbo la Rorya ndugu LAMECK AIRO kwa muda mrefu, je kuna mtu kamwona? Katika kikao cha Bunge kilichopita nilimtafuta sana Bungeni lkn sikufanikiwa kumwona. Sijui ana mpango gani na wananchi wake ambao wana shida nyingi sana lkn yeye yupo kimya tu; hivi anajua kwamba Ukimwi unawamaliza wananchi wake? na hali mbaya ya uchumi je? Lameck hata kuchangia kwa njia ya maandishi Bungeni imekuwa tatizo? Je ni nani sasa anayewasemea wananchi wake?

Hata mimi namtafuta wa kwangu David Mwakyusa Rungwe magharibi,wapi mbaba kimya kweli na huko home maendeleo hamna,wakulima wa chai hawana mtetezi full kuumizwa na mapebari(WATCO) naambiwa wamewafuata hata waliohamia kwa MOHMED ENTER LMT TZ?Paza sauti mbaba okoa maumivu ya wapga kura wako.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom