Jamani..!!! Na Mbeya tena..???

St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
7,633
4,515
1.JPG


Kijana wa miaka 17,Jafar Welino mkazi wa mtaa wa mianzini kitongoji cha Mabatini naye ameibuka na kikombe chake.

8.JPG

Mama mkubwa wa kijana huyo Edina Sanga akisaidia zoezi la kutoa dawa
9.JPG


Tangazo

7.JPG


Dogo akipata kikombe..

5.JPG


Dawa ikichemka.

2.JPG


Wagonjwa wakisubiria dawa..


Source: Michuzi.
 
Hii imeanza lini?nae kaoteshwa au mganga wa jadi?kama ni kweli basi tusubiri tuone tunakoelekea na haya matibabu
 
Hii imeanza lini?nae kaoteshwa au mganga wa jadi?kama ni kweli basi tusubiri tuone tunakoelekea na haya matibabu



Mkuu, huyu naye anadai ameoteshwa ila yeye hajaoteshwa na Mungu bali kaoteshwa na mama yake mzazi ambaye kwa sasa ni marehemu.
 
Nasikia Chama cha waganga wa dawa za kienyeji wanawakataa hawa jamaa. Sasa sijui ni kimaslahi ama kiprotokali.
 
Modern Day mediums at work. Kwa wale wanao fuatilia alama za nyakati, tumefikia kile kipindi cha shetani kuigiza kuja kwa Yesu. What we are seeing are just preminary tests. Soon and very soon mtasikia kwamba Musa, Maria, Paul na mitume na manaabi wametokea wapo semu fulani wanasema hivi na hivi. Lakini Biblia inasema wafu hawajui lolote. Ndungu zangu shetani yupo kazini, let the reader understand.
 
kila lenye mwanzo halikosi mwisho.. tutasikia mengi mwaka huu. sasa na huyu masharti ya kikombe ni yapi..?!! hakuna kurudia kama babu??
 
Dalili za watu kukosa imani. Kama kweli mfumo wetu wa afya ni affordable, hizi foleni za sasa zinatoka wapi? Ee Mungu Tupe ufahamu wanao, upepo wa Mashariki unatutikisa Bwana wetu.
 
2.JPG


Ndugu zanguni hebu tuitazame vizuri hii picha na kuitafakari,hawa ni wagonjwa kweli au ni wahuni tu wamekusanywa ili kumfanyia matangazo kijana??
 
jamani mbavu zangu, kuna bonge moja baa zima kabisa nalo kwenye foleni, hakianani
 
2.JPG


Ndugu zanguni hebu tuitazame vizuri hii picha na kuitafakari,hawa ni wagonjwa kweli au ni wahuni tu wamekusanywa ili kumfanyia matangazo kijana??

Paka, watu hawajapima ukimwi ila wana wasi wasi wana ukimwi, kuna watu wameenda kwa babu kwakua wana wasi wasi wana ngoma, si unajua tena tunavyoogopa majibu!
 
swali: alikuwa wapi siku zote? mpaka anakuja kipindi hiki baada ya babu!




Kwa yule warombo wala sikushtuka sababu nilijua ni lazima tu katika hawa ndugu zetu atatokea wa kuchagamkia tenda, sasa mpaka Nyanda za juu kusini??Sasa tusubiri sijui atakayefuata atakuwa wa wapi mpaka nafikiria na mimi nikusanye jamaa zangu nijitangaze waje kuchukua kikombe kwangu najua baada ya wiki moja tu naanza na mimi kukusanya mtaji.....
 
tumeyataka wenyewe kwa kuaminiamini kila kitu kirahisirahisi!

yana mwisho haya, Mungu yupo

Glory to God
 
Back
Top Bottom