Jamani mnalikumbuka hili!.

Nakumbuka kile kipindi cha Brothe Mic mahmood-Npe Habari, piga simu 9090 da er salaam,
Pia saa moja jioni mnajiunga na taarifa ya habari ya Tanzania zanzibar-jamaa wamewekwa kaswida duh ndo ngoma za kuanzia tarifa ya habari
 
Ahaa asante mkuu, kwa kweli hata mimi mmenikumbusha mbali saana. ila sio siri mimi mpaka leo huwa siachi kukumbuka kile kipindi cha mama na mwana hivi bado kipo. maana zile hadithi za binti chura, adili na nduguze, unyoya wa kipanga azizi, mfaule juha, ua jekundu, aha tena nakumbuka kipindi hiki kilikuwa siku ya juma pili saa nane mchana. kweli ya kale ni dhahabu. I wish kipindi hiki cha redio kingekuwepo maana kilikuwa kinawafanywa watoto kutulia na kuzikiliza hizi hadithi ambazo zilikuwa zinamafunzo kwa watoto.
 
Enzi hizo Tanzania tulikuwa na kituo kimoja cha radio, RTD. Piga ua ilikuwa lazima tu usikilize vipindi vyao vile vya ajabu ajabu kama vile,
1. Mbiu ya mikoa
2. Asilia salamu
3. Ukulima wa kisasa
4. Fimbo ya mnyonge
Nakwambia ilikuwa shughuli haswa, mwenye kukumbuka vinginvyo aongezee.
una kikumbuka kile kipindi cha mikingamo?
 
mkuu Sikonge na wengineo mmenikumbusha mbali sana...hasa kipindi cha nyimbo zetu,..sijui kama zile nyimbo zinapatikana wapi sasa hivi>?
 
Duu Mmenikumbusha mbali sana. enzi hizo za 47. Mifisadi ilianza toka zamani....
mnakumbuka
"Liangalieni Limbukeni hili, Linakula mali ya umma. wewe wacha kuharibu mali ya umma Wewe wacha kumaliza mali ya Umma, wewe wacha kuiba mali ya ummaa, wewe wacha ...... mali ya umma iki.........
 
Vipindi hivi bado vipo, tofauti siku hizi tunafungulia redio nyingine lakini ukitaka kukumbuka enzi za Mwalimu, nenda TBC Taifa.
 
Kwa kweli hii thread haikutakiwa kuwa under Jokes. Hata hivyo, shukrani kwako Mkuu Yegomasika kwa kutukumbusha enzi zile. Nakumbuka matangazo ya biashara km:
-Aspro ni dawa ya kweli
-Cafenol ni bora kuliko aspirin peke yake, hutuliza maumivu, homa, mafua na flu...
-Chai iliyo bora ni Green Label..kwa wakati wowote...hukupa nguvu...kiburudisho boraaaaa
-Surf mwamba
-Wembe chapa (mamba?)....utakunyoa na kukunyoa na kukunyoa
-Sukari ya Tanzania..chapa ya Bwana Sukariiiiii
Kulikuwa na kipindi cha STC. Kabla ya RTC kulikuwa na STC (State Trading Corporation) lakini waswahili tukaita Saidia Tujenge Chetu.
Ah jamani! kweli tumetoka mbali!
 
hahahahahahahaahahahaah,du ebwana kumbe tumekua walikuwa na chaguo la msikilizaji kipindi niko msingi ukuisikia unajua shule ushachelewa na msosi haujaiva,mambo ya mkoani hayo, hizo mboko za ticha balaaa ila tumetoka mbali si mchezo
 
Bila kusahau tumbuizo asilia....captain wake akiwa uncle J nyaisanga.

Utamsikia akisema haooo mwanakuja sasa waluguru...anaachia ngoma
yao kidogo then utamsikia akisema aahh waluguru acheni hasira njooni pole pole
then anaachia ngoma sasa.


hahahahhahh...
....Mkuu tumbuizo asilia sterling mwenyewe alikuwa Marehemu (RIP) Michael Katembo!!!
 
..Enzi za Club raha leo show, Habari na muziki, Chuo cha ushirika moshi, Majira (mtangazaji Ben Kiko)....
 
Enzi hizo Tanzania tulikuwa na kituo kimoja cha radio, RTD. Piga ua ilikuwa lazima tu usikilize vipindi vyao vile vya ajabu ajabu kama vile,
1. Mbiu ya mikoa
2. Asilia salamu
3. Ukulima wa kisasa
4. Fimbo ya mnyonge
Nakwambia ilikuwa shughuli haswa, mwenye kukumbuka vinginvyo aongezee.
BWANA UMEME sasa tufanyeje sikilizeni BIBI UMEMEM, wakati kulikuwa hakuna mgao wa umeme!!!!ahhhhhhhhhhh
 
Du kwa kweli tumekumbushana mbali sana, enzi hizo watu ilikuwa heri wakose taarifa ya habari lakini mazungumzo baada ya habari wasiyakose. Nakumbuka kuna wakati wenzetu wa nchi ya jirani waliwahi kuitwa Manyang'au, nadhani baada ya kuzing'ang'ania mali karibi zote za iliyokuwa Jumuia ya Africa mashariki. Walipandisha mzuka ile mbaya maana kwao neno Nyang'au lina maana ya Fisi.
 
Mazungumzo baada ya habari.
Jifunze kifaransa.
Umoja wa mataifa wiki hii
Inueni mioyo
 
Mmenikubusha Abdul Omar Masudi Jawewa (RIP) saa mbili kasorobo Michezo. Msemo wake maarufu baada ya Yanga kufungwa na Mwadui alisema
" Mdharau Mwiba Guu huota Tende" . Wakati ule alikuwa Katibu Mwenezi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom