Jamani!! Mgao wa Umeme umeanza tena?

UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
3,445
5,405
Jamani mgao wa umeme bado upo?mbona Mvua
zinanyesha nchi nzima!Jamani mi mbona
sielewe kwani maeneo ya Mbezi beach leo
siku ya pili hatuna umeme kuanzia kati
ya saa kumi mpka saa tano.Kuuliza ni
Mgao Je mabwawa hayajaja maji!mm
hii kali wakati masika yameanza nchi
nzima?
 
UPOPO,UPOPO! Tanzania kuna mgao wa umeme artificial...it is a man made disaster,kwani kile chama cha magamba na lijizirikali lake huvifahamu eti??? kwenye masika kuna mgao je itakuwaje ikija kufika July...wenzetu Kenya tayari wameingia barabarani sie bado tumelala
 
UPOPO,UPOPO! Tanzania kuna mgao wa umeme artificial...it is a man made disaster,kwani kile chama cha magamba na lijizirikali lake huvifahamu eti??? kwenye masika kuna mgao je itakuwaje ikija kufika July.
 
Mgao wa umeme bado upo, ila hauna ratiba, na unafanyika katika njia ambayo haieleweki.

Mfano hai mimi sikuwa najua kama mgao unaendelea, jana nimerudi home nakuta giza, nauliza watu wa nyumbani wananiambia toka nilipoondoka tu ile saa 2 asubuhi umeme ulikatika hadi saa 2 me narudi bado haujarudi. Nikashangaa kwani sio kawaida kwa maeneo yetu ya K/nyama kukatika umeme kwa muda mrefu, nilipowaendea Tanesco, wakaniambia kuwa kuna shoti imetokea mahala nyaya imekatika toka mchana. Kwa kuwa kulikuwa na mgao huku kwetu mafundi hawakuweza kufanya kitu. Hivyo waliporudisha umeme saa 12 jioni mafundi ndio wakaingia mt aani kutafuta hiyo sehemu yenye shoti ili watengeneze, na mategemeo ya kurudi hadi watakapopata tatizo lilipo na watengeneze, kifupi, hajui utarudi saa ngapi. Nikaenda zangu kulala gizagiza, hadi saa nane usiku ndio ukarudi.

Nilishangaa na kumuuliza kwani mgao unaendelea? na mbona watumiaji hatujui? na ratiba yao ipoji, akasema yeye anachojua mgao upo na jana ilikuwa zamu yetu, hiyo ratiba ipoje yeye hajui.

habari ndo hiyo jamani, MGAO UPOOOOO, wala haujajivua gamba.
 
hiyo namba ni general kwa ajili ya dar es salaam na mikoa ya jirani, lakini kwa msaada wa uhakika full time ni bora ukapiga kitengo cha dharura kwenye mkoa wa tanesco wa eneo lako....., na ukajipatia namba yao ya mkononi na sio kutegemea hizi landline maana usiku mara nyingi hawazipokei......

Regions Emergency Tel no.

- ARUSHA - 027 2506110/0732 979280
- ILALA - 022 213 3330 or 022 211 1044/5
- Kinondoni NORTH – 0784-768584 or 022 2700367/
- Kinondoni SOUTH - 022 217 1759/66
- TEMEKE - 022 213 8352
- DODOMA - 026 232 2095
- IRINGA - 026 270 2019
- KAGERA - 028 222 0061/3
- KIGOMA - 028 280 2668
- KILIMANJARO - 027 275 5007/8
- LINDI - 023 220 2282
- MARA - 028 262 2020
- MBEYA - 025 250 4219
- MOROGORO - 023 3501/2 or 260 4028(night)
- MTWARA - 023 233 3902
- MWANZA - 028 250 1060
- RUKWA - 025 280 2097
- RUVUMA - 025 260 2281
- SHINYANGA - 028 276 2120
- SINGIDA - 026 250 2133
- TABORA - 026 260 4784
- TANGA - 027 264 6779
- MANYARA - 027 253 1045
 
Mara nyingi hawa jamaa wa TANESCO hawawi wakweli, na ndio culture ya mashirika mengi ya UMMA. Kwa kule Ulaya lazima uwajibike lakini kwetu wala hakuna hata 'apology", wketu ni bora liende.
 
Uhuru walionao huku ukilindwa na sera za kibabe za CCM na siasa zao zisizo na utekelezaji ndizo zinazotupa tabu. R.I.P TANESCO
 
Back
Top Bottom