Jamani meno yanguuu!

kholo

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
413
75
Heshima kwenu ndugu wana jf, meno yangu hutoboka kisha yanaanza kuuma na baadaye yanaanza ku katika, naombeni msaada wenu wajuzi.
 
Wala usihangaike tafuta dawa ya meno ya Forever na vidonge(forever propolis) tatizo kwishiney. Mimi nimesumbuliwa mika 4 lakini baada ya kutumia hiyo dawa tatizo liliisha bila kung'oa huu mwaka wa 3 sijawahi sumbuliwa na jino. Adios.
 
Mie ni dentist, nakupa ofa kungo'oa meno mdomo mzima, kusafisha nyota ya mdomo na kukwarua ulimi tsh 200,000, wahi mapema. La sivyo kila jino kutoa tshs 50,000.
 
Nakupa Ushauri wangu ikiwezekana unapoamka asubuhi kabla ya kula kitu, unapokwenda chooni jaribu kukinga mkojo wako (urine) Usukutuwe mara tatu kila siku asubuhi kwa muda wa siku 7 kisha unipe majibu yake. Ishallah hayo matatizo yako yataondoka. Unapofanya dawa hii jaribu kukaa kama dakika 5 kisha waweza kusukutuwa maji ya kawaida kwa kupiga mswaki.
 
Cavity Cavity Cavity...ndio sababu ya matundu ya meno, hupigi mswaki vizuri na tumia dama iliyobora to fight cavity.
 
dah! Meno muhimu pengine kuliko hata mkono mmoja. Hakikisha unayapatia tiba kabla haujawa kibogoyo
 
Pole sana,meno huwa hayatoboki siku 1 na kuanza kuuma,yanaanza kutoboka lakini ni painless until cavity inapofika kwenye sensitive areas of the tooth,dentine na pulp..muone dentist as early as possible kuzuia progression ya cavity(restoration).sababu za kutoboka meno
1. Jino lenyewe(kuna % fulani ya watu wana meno yasio imara i.e yenye severe flourosis na mengineyo kama hayo
2. Hali ya usafi wa kinywa
3. Ulaji wa vyakula vya sukari kwa wingi bila kupiga mswaki..na hapo niseme kwamba ulaji vyakula vya sukari pekee hauwezi kusabisha meno kuoza,ila tatizo ni pale mabaki ya vyakula hivyo yanapokaa kwenye meno kwa muda mrefu na kuwapa muda wa kutosha bacteria to turn fermentable carbohydrate into acid ambayo ndio hutoboa jino..kupiga mswaki mara 2 kwa siku asbh na jioni inasaidia sana..adios
 
By Mzizimkavu
Nakupa Ushauri wangu ikiwezekana unapoamka asubuhi kabla ya kula kitu, unapokwenda chooni jaribu kukinga mkojo wako (urine) Usukutuwe mara tatu kila siku asubuhi kwa muda wa siku 7 kisha unipe majibu yake. Ishallah hayo matatizo yako yataondoka. Unapofanya dawa hii jaribu kukaa kama dakika 5 kisha waweza kusukutuwa maji ya kawaida kwa kupiga mswaki
Hii ni dawa kubwa japo ni ngumu kwa matumizi ya kawaida lakini inasaidia sana sina la zaidi kwenye kuielezea bali kama kweli una shida na hizi dawa za siku hizi zime gonga ukuta rudi kwenye asili yetu.Vinginevyo ndio hivyo suka au nyoa
 
Back
Top Bottom