Jamani, matumizi ya dola ya Marekani mpaka vijijini!?

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
8,305
13,265
Mi nashindwa kuelewa hivi hii tanzania tumelaniwa na nani? wala tusimsingizie Mungu[GOD] labda gods,kwani haiwezekani kila mambo ya ajabu ajabu tu,yawe yanatokea kwetu!Inawezekana vipi wafanyabiashara wa tumbaku wanataka kununua tumbaku toka kwa wakulima kwa kutumia fedha za kigeni[US DOLLAR],je hawa wakulima wanazijua hizo pesa?na wanafanya hivyo ili iweje?
 
Duh hii kwa kweli ni serikali kuweka law wakikiuka basi washitakiwe mie ndo navyoona maana inazidi kuenea hii issue
 
Wakati nchi zinajivunia hela zao hapa kwetu shilingi yetu inadharauliwa kama makaratasi kuna maduka na mahoteli kibao hapa Dar bila aibu bei za bidhaa zao zinawekwa kwenye dola za kimarekani.
Inasikitisha sana kwa sababu thamani ya dola inaweza kubadilika hata mara tatu kutwa na hivyo kujikuta wateja mnapata usumbufu mkubwa bei zinapobadilika ghafla.
Hivi sheria ya nchi inasemaje kuhusiana na kadhia hii?
 
Back
Top Bottom