Jamani maskini kigoma

sio mchezo nikiona mh zitto akiwa na makazi yake mjini dar wala sishangai na hii ni kwa wote wale wanao wakilisha majimbo yao wanao penda kukimbilia kuishi jijini dar kwakweli kunaumuhimu wa kuendelezea hii miji atleast pale mikoani

ivi ni huwa asilimia ngapi katika makusanyo ya kodi huwa yanabaki katika mikoa? au ndio lazima ije dar (hq) kwanza alafu ndio wapangiwe?
 
Hii ndio stand ya mabasi. Hapa kama unakwenda Kigoma wakakwambia tunakwenda hadi stand ya mabasi watakushushia hapa.
Na kama unatoka Kigoma kwenda mikoani kwa basi ukiambiwa nenda stand ya mabasi, njoo hapa.
:D

Stand ya bus.jpg

Stand.jpg
 
sio mchezo nikiona mh zitto akiwa na makazi yake mjini dar wala sishangai na hii ni kwa wote wale wanao wakilisha majimbo yao wanao penda kukimbilia kuishi jijini dar kwakweli kunaumuhimu wa kuendelezea hii miji atleast pale mikoani

ivi ni huwa asilimia ngapi katika makusanyo ya kodi huwa yanabaki katika mikoa? au ndio lazima ije dar (hq) kwanza alafu ndio wapangiwe?

Du! Mh Zitto anafahamika kama nini vile utadhani yeye peke yake ndiye mbunge kule Kigoma, Kwa nini? kuna wabunge wengi tu mbona maana kuna majimbo kibao mpaka ya wakina Nsanzugwako yako kule eti. Kule Kigoma naambiwa jimboni kwa Zitto ni safi sana na barabara afadhali kidogo. Jimbo lake liko nje kidogo ya mji wa Kigoma. Sijui kama ni kweli.
Lakini hapa mnapopaona ni kwenye jimbo la Mh. Selukamba. Mtetezi namba moja wa mafisadi.
Hapa Zitto mnamuonea tu wakuu!
:)
 
Zitto hawezi kuishi hapa.......washikaji,beer na nyama choma hakuna.Hapo ndio mwisho wa Reli kwa Buraza Kei
 
Ukiniambia habari ya wahindi wanitia kichefuchefu maana ukiwagusa tu wanakuita mbaguzi lakini hakuna wezi na wabaguzi kama watu hawa.
Angalia skendo zote za wizi mkubwa serikalini wao ni wahusika wakuu.
Tena bwana wee ni wabaguzi kuliko unavyoweza kusema. Hilo watu wengi hawalisemi ila ukieleza kasoro yao nakwambia watakuita mbaguzi we.
Ngoja ninyamaze maana hapa hapa nitasikia wananiita mbaguzi.

Ahsante sana MU kwa kusema kweli. Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko. Thanks a lot.
 
Picha ni hizi hizi mkuu ulikuwa na memory card ya 60MB?
Habari yako ni ndefu sana...iliyo jaa ukweli ambao ni mgumu
kuupokea lakini ungekuwa na tu viambatanisho twa kutosha
ingekuwa pouwa sana.Kwa mfano eneo la ziwa,wavuvi.

Picha za migebuka,dagaa uko hukutembelea?naona umeongelea
lakini hukuwa na viambatanisho...inafurahisha maelezo yenye picha.

Ni mtizamo tu.
 
Buswelu, Asante kwa maoni na mtazamo wako.
Nina picha nyingi sana nina kadi ya 4 gb na kuna maeneo kwa sababu moja au nyingine sikuweza kupata picha zake.
Na kwa kweli sikuwa KG kwa ajili hii nilikuwa katika kutafuta biashara zangu na haya nilikutana nayo. Na kama mwana jf nilikuwa na kitu mkononi cha kuelezea kuhusu KG.
Utanisamehe kwamba nitajitahidi kuweka picha nyingi hapa kadri nitakavyoweza. Lakini niliyoeleza ni hayo na mwingine anaweza kwenda na najua atakuja na habari hii hii.
 
Zitto hawezi kuishi hapa.......washikaji,beer na nyama choma hakuna.Hapo ndio mwisho wa Reli kwa Buraza Kei
Yoyo mbona unamwandama sana Zitto wakati Kigoma ina wabunge wengi?
Waseme na wakina Selukamba na wengine kama Nsanzugwako. Mbona umemshikia Zitto bango peke yake?
Inaelekea una jambo!
:D Hakukupa offer ya nyama choma na beer?:D
 
Kigoma nayo kama miji mingine ya Tanzania haiko nyuma katika kuzalisha watoto wa mitaani. Jamani tunaelekea wapi kama nchi yetu mitaa itaendelea kuzaa?
Ebu angalia walivyo na nyuso za furaha! Picha imepigwa usiku vichocholoni wala hawajali kwamba wanalala nje na kwenye takataka.

Street boys.jpg

Street boyz.jpg

Street boyz-1.jpg
 
Attachments

  • Street boyz-2.jpg
    Street boyz-2.jpg
    20.2 KB · Views: 79
Mchukia Fisadi,

Thread yako naona inaleta simanzi lakini vile vile ni inaleta changamoto kwa viongozi wetu an kwetu sisi kama wananchi. Mara nyingi wengi wetu huwa hatujui madhira wanayoyapata ndugu zetu wanaoishi mikoani kwa sababu muda mwingi tupo Dar es Salaam.

Napendekeza ni vizuri picha zaidi za mikoa mingine ya Tanzania yetu ziwe posted hapa na yeyote anayefanikiwa kusafiri kwenda huko au aishie ili tujue zaidi kuhusu nchi yetu na jinsi hali ya maendeleo ilivyotofautiana mkoa hadi mkoa.....Picha zinaongea zaidi ya maneno.
 
Hii ni beach ya ujiji ambako unaona watu ni wengi sana wakifua na kuchota maji. Hapo ujiji pamoja na kuwa kuna ziwa karibu sana shida ya maji kwao ni kitu cha kawaida kiasi kwamba hao mabinti wawili wanatoka kuchota maji katika kisima cha kuchimba kiko nyuma yao tu hapo walipo na ni 1/4 km kutoka ziwani!
Na watu wengi wengine huko ziwani wanafua, wengine wanaoga, na wengine wanachota maji na ng'ombe wanakata kiu. Angalia watoto wanavyo enjoy swimming!
Hayo ndio maisha.

Ziwani.jpg

Watoto maji.jpg
 
Mchukia Fisadi,

Thread yako naona inaleta simanzi lakini vile vile ni inaleta changamoto kwa viongozi wetu an kwetu sisi kama wananchi. Mara nyingi wengi wetu huwa hatujui madhira wanayoyapata ndugu zetu wanaoishi mikoani kwa sababu muda mwingi tupo Dar es Salaam.

Napendekeza ni vizuri picha zaidi za mikoa mingine ya Tanzania yetu ziwe posted hapa na yeyote anayefanikiwa kusafiri kwenda huko au aishie ili tujue zaidi kuhusu nchi yetu na jinsi hali ya maendeleo ilivyotofautiana mkoa hadi mkoa.....Picha zinaongea zaidi ya maneno.
Ni kweli. Sijui kama wanapata muda wa kuangalia hapa. Lakini wanaona au la, najua message delivered.
 
Haya ni mashamba mengi ya mawese yanayoonyesha utajiri katika kilimo. Sijui kama kuna care zaidi kwa mashamba haya. Mengi yameshakuwa kama vichaka.

Mashamba mawese.jpg

Na watoto hawakosi kufanya vibarua wapate riziki kidogo. Maana hali ya maisha ni tete.

Watoto na kazi.jpg
 
Hili ni jengo Jipya la makumbusho ya Livingstone kwa ajili ya utalii na kuonyesha habari za livingstone. Lingetumika kuonyesha pia historia mbali mbali za Waha pia ingependeza sana kuliko kutumika kwa ajili ya Livingstone pekee.

Makumbusho.jpg

Bado liko under construction lakini kwa ndani laonekana hivi

Makumbusho ndani.jpg
 
Ukifika kwenye Jengo la makumbusho ya Dr Livingstone unakuta majambozi haya.

Livingstone.jpg

Livingstone-1.jpg

Livingstone-2.jpg

Usijali ukifika pale kuna wanahistoria wanakusimulia kila unachokiona na historia yake.
gharama sio kubwa! ni sh. 1,500/= kwa mdanganyika na wazungu wana bei yao.
Ukitaka kupiga na picha unaongeza visenti. Price is negotiable. Mimi nililipa 3,000/= kupiga picha zote ninazohitaji. Wewe unaweza kulipa kidogo au zaidi kwa kufuatana na jinsi gani unajieleza, umenyenyekea kiasi gani, na unafananaje
:)
Ukifika Kigoma nenda ukatembelee pale. Tunahitaji utalii wa ndani pia wajameni.
 
Ehhhhhhhhhh zingine kesho wajameni.
Kwaheri kwa leo, walio bongo usiku mwema na mlio majuu mchana na jioni njema
 
Kigoma zipo theaters nyingi sana kwa ajili ya kuangalizia video na sinema zilizotafsiriwa kienyeji. Hapa jamaa walikosa mshiko wa kuangalia mechi ya Man na Chelsea na wako wanapiga chabo dirishani:D

Chabo.jpg

Na hapa ndio airport ya KG. Ukipata nafasi ya kwenda KG kwa ndege utashukia hapa. Naona palipanda chati kwa sababu ya wakimbizi la sivyo, mmmmhhhh hata hivyo bado ni ka strip kadogo.:)

Airport.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom