Jamani Maisha ni Magumu sana Ulaya, Watu Wanateseka - Mwana FA

Mwana FA anamagilia JK akirudi amvae amsaidie ajira jamani hilo shuti la mbali hamjui tu.....mtaona akirudi....
__________________
KALOGWA HUYU...KAONA MWENZAKE JUMA NATURE ANAZUNGUKA NA MZEE KWENYE UCHAGUZI AKAJUA.....2010 JAMAA ATAMKUMBUKA KWANI HAMJUI KAMPENI ZIMEANZA JAMANI...NA YEYE AMEANZISHA KAMPENI YAKE.....KILA LA KHERI MWANA
SWALA LA NJE...WAACHIE WA NJE NDUGU NAAMINI KILA ANAEONDOKA KWENDA NJE ANA MALENGO YAKE NA KAMA HAYAKWENDA YALIVYOPANGWA BASI ANA RETURN TKT YA KURUDI JNIA........................

PILI:
NAOMBA TUWE WAZI HUYU BWANA KWELI INAWEZEKANA KASHUKIA KWA JAMAA ALIEKUWA TAITI KINOMA...SASA BASI NI KWELI HAKUNA HAJA YA KUPINGANA NAE UKIMWAMBIA MTU AACHE UMALA$%%% LAZIMA UMSAIDIE KUMSHAURI AFANYE KAZI GANI ITAKAYOMSAIDIA ZAIDI ANAYOFANYA...SASA KAMA YUKO SERIOUS NA HUYO RAISI WAKE BASI TUNAMWOMBA KABLA YA KUWAMBIA WATU WARUDI BONGO AMWAMBIE RAIS ATENGENEZE AJIRA.......JAMANI MAISHA NJE NI MAGUMU ILA NAPENDA KUWAAMBIA WAZI ASILIMIA KUBWA YA MAISHA WANAOISHI WATANZANIA WA NJE SI KAMA YA BONGO DAR ES SALAAM....BONGO NOMA .....
 
I hope hauja nichanganya mimi na Mwana FA mwanamuziki. We share the same name but we are different people.

Ni kweli huwezi kujua ulaya kwa kukaa miezi michache. Wala mimi sijaongelea based on kukaa miezi michache. Unless you have confused me na Mwana FA mwanamuziki I don't know why you quoted me and used speech directed to me
.

Nilikuwa naungana na wewe sio mwanamuziki.

Mwanamuzi amekaa Ulaya kwa miezi minne-mitano, sio rahisi ajue mambo ya Uingereza.

au inawezekana Mwenyeji wake hana network au hajui vyanzo vingi vya mambo Uingereza.hilo linaweza kumletea matatizo Mwanamuziki kama wenyeji wake hawana upeo mkubwa.

Maisha ya nje mara nyingi yanategemea aina ya Visa uliyo nayo kukupatia kazi nzuri n.k

Mimi nina rafiki yangu amekwenda Uingereza kama mwaka mmoja uliopita ana kazi ya mshahara wa pounds elfu tano kwa mwezi wakati Bongo alikuwa akipata mshahara wa laki nne kwa mwezi alikuwa na elimu ya chuo kikuu.

nimeshuhudia mgonjwa aliyekuwa akihitaji kufanyiwa operesheni toka mwezi december mwaka jana hadi mwezi uliopita alikuwa Muhimbili akisubiri kufanyiwa operesheni kila wiki anaambiwa kesho kesho hatimaye umauti ukampata.
operesheni yake ilikuwa kama angekwenda Tumaini Hospital angetibiwa kwa milioni moja au laki tisa.sidhani kama mtu anaweza kufa Uingereza kwa kukosa pesa ya kulipia hospitali au Hospitali kutompa huduma hadi awe na pesa mkononi.

Mwanamuziki ameshindwa kuelewa kuwa yeye kama Mwanamuziki akipita Billicanas atapa chakula bure,akiwa kituoni atapewa lifti,akitaka shati atanunuliwa na promota.hivyo maisha yake yanaweza kuwa ya bure bure TZ, mtu kama huyu sio rahisi kujua watu wenye shida wako vipi?

angejaribu kupita vijijini au maeneo kama Tandale kwa Mtogole,aone watu wanavyowahi sokoni Kariakoo saa tisa usiku waende kubeba mizigo ili wapate mlo wao na familia.atembelee vijiweni maeneo ya MBAGALA,VINGUNGUTI KIEMBE MBUZI,TANDIKA n.k yeye anatembelea Mbezi beach,Masaki,Oysterbay sio rahisi ajue hali halisi za watanzania.

Mtu kama DR.Shayo wa London SouthBank University utasema kuwa arudi nyumbani wakati anafundisha wazungu mazingira na analipwa pounds kibao?
Mtangazaji kama Charles Hilal mshahara wake si chini ya Milioni kumi kwa mwezi BBC angekuwa Radio one ya Mzee Mengi angepata kiasi gani?
 
Mi nafikiri huyu mwanafa anamatatizo ya akili. Ulaya kila mtu anakwenda kwa malengo yake na yakishindikana ataishi lakini ni bora kuliko maisha ya bongo hata usafiri wa daladala ni karaa. huyu ni sawa na wale wanaojiita dr, engineer etc yote ni ulimbukeni. mimi nilifanyakazi na mzungu muhimbili alikuwa PHD holder lakini hata siku moja hajiiti DR fulani. Tuache ulimbukeni wabongo wewe kama umeenda Ulaya ukafikiri ni bongo vitu vya bure mara kwa washikaji upanga imekula kwako. Watanzania tunahitaji sana exposure maana simple decision and sacrifices zinatushinda.
 
Una hoja Babu Ubwete, wabongo we need exposure, maana simple decision na sacrifices zinatushinda. Si huwa unaona wanasoka wetu wakienda nchi nyingine panapohitajika uvumilivu na kujitoa mhanga kwa ajili ya muskabali mzuri wa baadaye? wengi huishia kutoa sababu kibao na lawama kisha wanarudi kujisajili tena timu za bongo contrary to what they said wakati wa kuondoka. utasikia "lengo langu ni kucheza ligi kuu uingereza" wapi!! Danny Mrwanda nasikia karudi toka Qatar yupo "nyumbani" Simba
 
Mzee, we unaonyesha ni mtu wa sports sana.
Embu tuletee mambo kule kwenye jamvi la michezo basi.
So ni MKULIMA MWANAMICHEZO! Big up.
 
Maisha kokote ni tough especially kipindi hiki ambapo mtikisiko wa uchumi umesababisha wengi ambao walikuwa wamesogea sehemu fulani aidha kupiga maktaimu au kurudi nyuma. Kama utafuatilia mambo ya uchumi utaona hata watu kama Bill Gates wamepoteza pesa au thamani ya mali zao.

Pamoja na hayo Ulaya na USA kuna opportinities nyingi kuliko Afrika. Maskini wa Uttah, US au Conventry, UK huwezi kumlinganisha na maskini wa Sunuka, Kigoma Tanzania. Vilevile huwezi kujua kama Mwana FA alikuwa na kibali cha kufanya kazi au la. Kama huna makaratasi nayo inaweza kuwa shida, lakini kuna watu kibao wasio na makaratasi wana maisha poa tu kwa sababu ya struggles zao. Wengine wakifika nchi za watu wanataka ku-chill bila ku-struggle. hata Bongo watu wana-struggle na life.
 
Mwana falsafa ana upungufu wa falsafa. Akumbuke kuwa ulaya hakuna mambo ya siri au ya kujikomba na kupendeleana kama ilivyo bongo; unaishi kwa jasho lako. Sasa kama yeye alitarajia vya mteremko kama anavyofanya sasa kujikomba kwa JK basi ulaya haiwezi kabisa. Ni kweli ukitaka vya bure Ulaya hutavipata hata siku moja.
 
Kila sehemu maisha ni magumu, Bongo inaonekana rahisi sababu wizi, usanii utapeli umehalalishwa, Otherwise ukishi kihalali bado maisha ni magumu
 
Habari kwa hisani ya Abdallah Mrisho 7/17/2009 2:08:12 AM
2534358.jpg
Siku chache baada ya kudondoka kutoka pande za Uingereza anakopiga kitabu, mkali wa Bongo Flava, Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA amesema na ShowBiz amejionea kwa macho yake baadhi ya watu wanaoishi huko wakitaabika bila kuwa na ishu ya kufanya.

Msanii huyo alisema kwamba, baadhi ya vijana wengi bado wana ndoto za kwenda Ulaya wakidhani kwamba maisha ni rahisi kitu ambacho siyo cha kweli kwakuwa huko pia wapo watu wengi wasiokuwa na ajira wanasota mitaani.

“Ulaya maisha magumu washkaji, mtu kama una dili yako ya kupata miambili miambili Bongo bora utulie uendelee kuongeza kipato na kuijenga nchi yako badala ya kukimbilia Ulaya.

Ninachoongea watu wanaweza wasiniamini lakini anayeweza aende akajionee mwenyewe,” alisema FA ambaye hivi sasa anafanya vyema na ngoma yake mpya, ‘Nazeeka sasa’ iliyowashirikisha Prof. Jay na Sugu.

Akiizungumzia picha ya Rais Kikwete iliyopo katika baadhi ya tisheti zake (kama anavyoonekana pichani), Hamisi alisema kwamba, hivi sasa ameamua kuachana na ujinga wa kuvaa nguo zenye picha za mastaa wa Ulaya wakati yeye ni Mbongo. “Yaani mimi namfagilia sana JK kuliko Rais yeyote duniani kwa kuwa ni mzalendo wa kweli. Kwangu mimi Kikwete wa kwanza halafu anafuata Obama,” alisema FA.

Aidha, mchizi aliiambia safu kuwa, mwishoni mwa mwezi huu atarudi Uingereza kwa ajili ya kumalizia masomo yake ambapo anatarajia kukusanya mafaili yake na kurudi Bongo Desemba mwaka huu akiwa na Masters yake.

http://www.nifahamishe.com/entertainment.aspx?NewsID=2534358
 
Ni kweli huko ulaya maisha ni magumu sana kila kitu ni kulipia lakini hapa bongo ni kujitafutia bila ya harama ,angalia kina mama wanajichotea maji wala hayana malipo,bure kwa kila mwanchi .
maji.jpg
 
Unajua nyie mijitu mingine bana!!

Alichosema dogo ni kuwa wengi ambao hawajafika ulaya au Marekani wanadhani mtu akienda huko au akiwa anaishi huko maisha ni RAHISI au atakuwa ameyapatia.

Sasa anachosema FA ni kuwa sio kweli, maisha huko ni magumu kama huku, husije ukaacha kazi yako ukakimbilia huko.

Yap pia wengi wenu ni wabeba mabox!! hamna hata access na sehemu za starehe za nguvu ndo maana mnafanya party zenu za kujichangisha......

Huku Africa hata ukienda Hilton Hotel au Kempinski hakuna anayekuangalia kwa jicho la mashaka. ...raha tu ili mradi uwe na chapaa, huko bana hata kama YOYO anachapaaaa kiasi gani akiingia sehemu ya juu lazima aangaliwe asije akakwapua glass.

By the way hela ya mabox haiwezi kukupeleka sehemu hizo.
 
AMEGUSA KIDONDA HASA. HUKU MAISHA NI MAGUMU, WALA SIO KIDOGO.hakuna mishe mishe, hakuna akiba, kila mwisho na kati ya mwezi ni mikate kwa kwenda mbele. mifumo sawa ni mizuri, lakini watu hawali mifumo wala kunwa mifumo ati. Huku hata wazawa ni watumwa katika nchi yao. aina ya kodi ni regressive, ambayo siku zote huumiza wafanyakazi wa mishahara. kiukweli watu ni wapweke, maskini wa vipato, japo nchi zina pesa, wasio na uhuru zaidi ya kufuata sheria.
Kwa wenzetu waafrika huku ndo utawaonea huruma, wanavyojaribu kujifariji ,kwa vimikutano vya weekend, kupunguzaa upweke, na kugawana umaskini kwa kunywa japo bia, na vinyama. UBAGUZI BADO UPO JUU SANA PIA.
 
sure, hasa UK. kuna jamaa yangu mmoja kaniambia kuna kitongoji huko nimesahau jina lake. ni sawa na manzese huku bongo. huko ndiko wabongo wengi waliko. sasa kuna mshkaji mwingine tumesoma nae bongo then akaenda kusoma UK akaishia kwenye kitongoji hicho. kashauriwa kurudi bongo kasema bora afie huko kwani anaona soo kurudi huku nyumbani.
 
Ni kweli, hizi nchi za ulaya marekani na kwingineko maisha ni magumu. Kila kitu ni fedha, na gharama za maisha ni juu. Kwa hiyo kama unataka kwenda huko lazima uwe na ajira ya kueleweka. Hizi ajira za mitaani za kuosha vyombo hotelini hazilipi. Sana sana utapata pesa ya chakula na kodi ya nyumba. Ukiwa huna ajira, utaishi maisha mabaya kuzidi bongo. Lakini ukiwa na elimu yako na ajira ya kueleweka utaishi kawaida, kama bongo tu. Miundombinu na teknolojia iko juu lakini ni kipato chako ndicho kitakuwezesha kuvitumia hivyo, simply being there doesn't cut it.

Upweke na ubaguzi bado upo, kwa hiyo ukienda huko kupata ajira itakuwa vigumu kidogo na itabidi ufanye kazi mara mbili ya wenyeji ili uweze kupata kipato cha kukuwezesha kuishi. Wapo wanaoenda na kufanikiwa, lakini wengi wanasota. Kama unabisha, nenda kajionee mwenyewe. Maana mtoto akililia wembe....
 
Anazungumza hivyo kwasababu ni popular kusema hayo,kwanza maisha ya UK ni tofauti na USA,pili anazungumzia wasio na elimu,kwasababu anadai heri uridhike na mia mbili yako bongo,kabla ya kuongea tumieni akili wasanii.
Na hilo la kumfagilia JK ni nja tu,anajuwa clouds watamfanyia,true artist is a free one with a free mind!
 
Unajua nyie mijitu mingine bana!!

Alichosema dogo ni kuwa wengi ambao hawajafika ulaya au Marekani wanadhani mtu akienda huko au akiwa anaishi huko maisha ni RAHISI au atakuwa ameyapatia.

Sasa anachosema FA ni kuwa sio kweli, maisha huko ni magumu kama huku, husije ukaacha kazi yako ukakimbilia huko.

Yap pia wengi wenu ni wabeba mabox!! hamna hata access na sehemu za starehe za nguvu ndo maana mnafanya party zenu za kujichangisha......

Huku Africa hata ukienda Hilton Hotel au Kempinski hakuna anayekuangalia kwa jicho la mashaka. ...raha tu ili mradi uwe na chapaa, huko bana hata kama YOYO anachapaaaa kiasi gani akiingia sehemu ya juu lazima aangaliwe asije akakwapua glass.

By the way hela ya mabox haiwezi kukupeleka sehemu hizo.

Yes,either uwe fisadi ama ngozi nyeupe ie mzungu!
Hilo la kusema eti watu wanafanya parties coz hawawezi kwenda descent places ni ushakunaku.....Mara nyingi ni after patries ama wabongo wenye kupenda kuendeleza ubongo bongo na ku reminesce mambo ya home etc,acha mirepresentation.
 
Msanii maarufu wa Bongo Flava Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA ambaye alienda nchini Uingereza kusoma amerudi Tanzania na kusema maisha ya ulaya ni magumu sana na watu wanateseka sana. Mwana FA hawashauri watu waache kazi zao Bongo kukimbilia ulaya.

FA.jpg

Siku chache baada ya kudondoka kutoka pande za Uingereza anakopiga kitabu, mkali wa Bongo Flava, Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA amesema na ShowBiz amejionea kwa macho yake baadhi ya watu wanaoishi huko wakitaabika bila kuwa na ishu ya kufanya.

Msanii huyo alisema kwamba, baadhi ya vijana wengi bado wana ndoto za kwenda Ulaya wakidhani kwamba maisha ni rahisi kitu ambacho siyo cha kweli kwakuwa huko pia wapo watu wengi wasiokuwa na ajira wanasota mitaani.

Ulaya maisha magumu washkaji, mtu kama una dili yako ya kupata miambili miambili Bongo bora utulie uendelee kuongeza kipato na kuijenga nchi yako badala ya kukimbilia Ulaya.

Ninachoongea watu wanaweza wasiniamini lakini anayeweza aende akajionee mwenyewe, alisema FA ambaye hivi sasa anafanya vyema na ngoma yake mpya, Nazeeka sasa iliyowashirikisha Prof. Jay na Sugu.

Akiizungumzia picha ya Rais Kikwete iliyopo katika baadhi ya tisheti zake (kama anavyoonekana pichani), Hamisi alisema kwamba, hivi sasa ameamua kuachana na ujinga wa kuvaa nguo zenye picha za mastaa wa Ulaya wakati yeye ni Mbongo. Yaani mimi namfagilia sana JK kuliko Rais yeyote duniani kwa kuwa ni mzalendo wa kweli. Kwangu mimi Kikwete wa kwanza halafu anafuata Obama, alisema FA.

Aidha, mchizi aliiambia safu kuwa, mwishoni mwa mwezi huu atarudi Uingereza kwa ajili ya kumalizia masomo yake ambapo anatarajia kukusanya mafaili yake na kurudi Bongo Desemba mwaka huu akiwa na Masters yake.

........utaona na kusoma unachokipenda..........
Sawa
 
Back
Top Bottom