JAMANI KWELI YALE MABADILIKO NDO HAYA AU? ?? Mimi nataka kujua kama kunankitu kimeachwa maana naoki

shelumwa

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
516
188
USICHOKE KUSOMA NI HAKI YAKO SOMA KAMA HAUJAELEWA SEHEMU NIPO KWA AJIRI YA KUKUELEWESHA NI HAKI YAKO KUJUA YOTE KAMA ULISHINDWA KUTEMBELEA TOVUTI

HOTUBA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA
CHAMA CHA CHADEMA NA UKAWA MH.
EDWARD NGOYAI LOWASSA YA KUZINDUA
ILANI NA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU
Jangwani-Dar-es-Salaam, 29 AGOSTI
2015
Ndugu Wana Dar es salaam na Watanzania
wenzangu
1. Leo ni siku ya kihistoria. Baada ya
miaka ishirini na tano tangu mfumo
wa vyama vingi urejeshwe, vyama
vya upinzani wa CHADEMA, CUF,
NCCR na NLD umeungana chini ya
Umoja wa Katiba ya Wananchi
kupigania uchaguzi mkuu wa mwaka
huu na kuwa na mgombea mmoja
katika ngazi zote.
2. Miaka zaidi ya hamsini ya utawala
wa serikali za CCM na waasisi wake,
umekuwa utawala wa wachache walio
hodhi madaraka na mali za nchi.
3. Leo tunaanza safari ya uhakika ya
kuleta mabadiliko ya kweli nchini.
1. Mabadiliko yaletayo neema na
kujenga upya mfumo wa
uchumi, haki na sheria nchini.
2. Mabadiliko ya kuimarisha
huduma za jamii kama elimu,
afya, maji na makazi.
3. Mabadiliko ya kuondoa
umaskini.
4. Mabadiliko tunayatoahidi ni
mabadiliko ya kurejesha
matumaini kwa Watanzania
kwa kubadili hali zao za
maisha.
4. Kila mwaka hali na ubora wa maisha
ya Watanzania imeshuka wakati
tunaambiwa kuwa pato laTaifa
linakuwa.
5. Lakini Watanzania wanachotaka siyo
takwimu bali kuona kipato chao
kinakua, shule, hospitali na barabara
bora zinajengwa.
6. Wanataka kupata maji safi na salama
ya kunywa. Wanataka makazi bora.
7. CHADEMA na UKAWA, tuna dhamira ya
kuleta mabadiliko ya kweli ili kuona
azma ya Watanzania tangu uhuru ya
kuondoa umaskini, maradhi,na ujinga
inahitimishwa.
8. Ili tufanye hivyo tuahitaji tufanye
mabadiliko ya fikra, uongozi, sera na
utendaji.
9. Leo Tanzania inakabiliwa na
changamoto nyingi za ki-uchumi,
kisiasa na kijamii. Changamoto hizi
ni matokeo ya sera za utawala wa
Chama kimoja wa miaka hamsini. Sote
ni wahanga wa siasa na sera hizi.
10. Miaka Hamsini ya CCM imetosha.
Tunataka mabadiliko na siyo ahadi
zile zile kila mwaka
11. Tusidanganyike, CCM hawana jipya
12. Chagueni UKAWA wenye dira ya
kubadili maisha ya wananchi.
13. Mimi ninauchukia umaskini na
mimesimamia maendeleo kwa vitendo.
Nilipokuwa Waziri Mkuu nilijaribu
kubadili hali hii. Nilisimamia ujenzi
wa shule za kata, Chuo Kikuu cha
Dodoma. Nilihakikisha mikataba
mibovu ya maji inavunjwa na sasa
wananchi wa kanda ya ziwa
wanapata maji safi.
Ndugu watanzania
14. CCM wanauliza tuna mpango gani wa
kumaliza umaskini. Sisi hatuahidi tu.
Tutatenda.
15. Ilani yetu ni dira ya kuondoa
umaskini kwa mikakati sahihi na siyo
nadharia.
16. Mkakati wa kuondoa umaskini si wa
sekta kwa sekta bali wa sekta zote
kwa pamoja. Ni ujumla wa utendaji
na utekelezaji wa sera za kila sekta
utakao leta maendeleo.
17. Mkakati wangu na UKAWA wa
kuondoa umaskini utakuwa na nguzo
tano:-
1. Kupunguza matumizi ya
serikali na mashirika yake na
kuimarisha utendaji na
uwajibikaji.
2. Kukuza pato la serikali kwa
kudhibiti ukwepaji na misamaha
ya kodi holela na kuhakikisha
nchi inawekeza katika sekta
muhimu na inapata gawio
halisia kutoka wawekezaji
3. Kukuza uchumi kwa sera na
sheria endelevu ikiwa ni
pamoja na kukuza biashara na
uwekezaji hasa katika sekta za
madini, kilimo, viwanda,
ufugaji na uvuvi na kuondoa
kodi kwa wanyonge.
4. Kuimarisha huduma za umma
kama elimu, afya, maji na
makazi, na mazingira
5. Kuimarisha utawala bora na
mfumo wa haki na sheria chini
ya Katiba ya Wananchi.
18. Chini ya misingi hii na ili kufanikisha
mkakati wa kuondoa umaskini,
serikali yangu itafanya yafuatayo:-
ELIMU BORA KWA KILA MTANZANIA
Nimelisema hili huko nyuma. Nalisema
tena leo. Elimu kwanza, Elimu kwanza,
Elimu kwanza.
Kwa hiyo mkakati wetu wa msingi
utakuwa kutoa Elimu itatayogharamiwa
na serikali kwa kila Mtanzania kutoka
elimu ya msingi hadi Chuo Kikuu na pia:-
1. Kuimarisha elimu ya teknolojia,
ustadi na ufundi inayojenga uwezo
wa kujiajiri na ushindani katika soko
la ajira.
2. Ujenzi na uimarishaji wa
miundombinu ya elimu ikiwa ni
pamoja na shule za Kata.
3. Kusimamia ubora wa viwango vya
elimu kote nchini.
4. Kuimarisha taaluma na mitaala
katika mashule.
5. Kuondoa utoro darasani, na
kuboresha afya za wanafunzi.
6. Kuboresha maslahi na vitendea kazi
kwa walimu ikiwa ni pamoja na
nyumba, posho ya kufundishia,
usafiri na zana za teknolojia.
7. Kufuta michango ya maabara ya
shule za kata
AFYA
1. Afya na tiba ya kila Mtanzania
itagharamiwa kupitia bima za
gharama nafuu na mifuko ya hifadhi
ya jamii
2. Tutaimarisha afya ya msingi pamoja
na kinga kupunguza gharama za
tiba.
3. Serikali itahakikisha kuna uwiano na
upatikanaji wa watumishi wa afya
katika kada mbalimbali ili kuleta tija
na huduma stahiki.
4. Itaimarisha miundombinu ya afya
pamoja na kujenga hospitali za
kisasa ili kusogeza huduma za afya
karibu na jamii na pia kuepukana na
tiba za nje ya nchi.
5. Tutarejea kwa lengo la kuboresha
maslahi na vitendea kazi katika
sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na
nyumba na usafiri.
6. Tutathibiti ongezeko la gharama za
huduma za afya bila kuathiri
uendeshaji wa watoaji huduma za
afya kama vile serikali na hospitali
za sekta binafsi.
ARDHI, MAJI NA KILIMO
1. Tutaimarisha mfumo wa umiliki wa
ardhi kwa Watanzania na kudhibiti
migogoro ya ardhi hasa kati ya
wakulima na wafugaji.
2. Tutapima ardhi yote ya Tanzania na
kumilikisha vijiji na wakulima kwa
hati za serikali ili kuipa thamani.
3. Tutaleta mapinduzi ya kilimo kwa
kuimarisha elimu, ufundi na
teknolojia ya kisasa na kumkomboa
mkulima kutoka jembe la mkono.
4. Tutasimamia kilimo, ufugaji na uvuvi
wa kisasa na kuunganisha sekta hizo
na ya viwanda.
5. Kuhakikisha kuwa wananchi
wanatunza na kulinda vyanzo vya
maji.
6. Tutakuza kilimo cha umwagiliaji kwa
kuwapa wakulima elimu na mikopo ya
riba nafuu ya kuvuna maji na
kujenga miundombinu husika.
7. Tutaweka mazingira rafiki
yatakayomhakikishia kwa kila
Mtanzania kupata maji safi na
salama. Kumaliza kero za maji nchini
kutamkomboa mwanamke kutokana na
adha ya kuchota maji kwa kichwa
8. Nitafuta kodi zote za mazao na
mifugo kwa wakulima na wafugaji.
9. Tutasimamia kilimo cha biashara
kinachozingatia maslahi ya nchi na
ya Watanzania.
10. Tutaanzisha programu maalum ya
kufufua mazao asilia ya Tanzania
hususan mkonge.
11. Tutaanzisha Benki ya Maendelo ya
Ufugaji na Uvuvi.
MIUNDOMBINU
1. Tutaboresha bandari zilizopo na
kujenga mpya kama vitega uchumi
vya Taifa ili kurejesha biashara
tulizopoteza kwa bandari za nchi
jirani.
2. Tutajenga barabara nchini kwa
kuzingatia ubora hasa zile za
vijijini.
3. Tutajenga reli ya kati kwa viwango
vya kisasa
4. Tutajenga shirika la Ndege la Taifa
linalojiendesha kwa misingi ya faida.
5. Tutajenga miundombinu ya kisasa na
kuondosha misongamano ya magari
hasa katika majiji ya Dar es salaam,
Mwanza, Mbeya na Arusha
6. Tutaimarisha uzalishaji na
usambazaji wa umeme vijijini ili
kufikia zaidi ya asili mia sabini na
tano ya Watanzania
VIWANDA
1. Tutaimarisha sekta ya viwanda kuwa
mhimili wa uchumi kwa uzalishaji wa
bidhaa na ajira endelevu
2. Tutajenga viwanda vipya vya
kusindika mazao ya kilimo, uvuvi na
ufugaji.
3. Tutahakikisha kuwa ndani ya miaka
mitano mali ghafi zote za Tanzania
zinasindikwa kabla ya kusafirishwa
nje ili kuongeza mapato na ajira ya
mamilioni ya vijana.
4. Tutaanzisha Benki ya Ukuzaji wa
Viwanda
UCHUMI
1. Tutabadili mfumo wa Uchumi wa nchi
ili kuhakikisha kuwa mfumo wa
uchumi wa Tanzania unakuwa ni wa
soko-kijamii ambapo nguvu za soko
zitatumikia jamii kwa serikali
kuweka uwiano wa mapato
unaohakikisha huduma za kijamii
zinapatikana kwa ufanisi.
2. Tutalinda sekta binafsi na bidhaa za
ndani kwa kuwapa Watanzania
upendeleo wa maksudi kwa kipindi cha
mpito ili waimarike na waweze
kuhimili ushindani. Tutawapa
wafanyabiashara wetu upendeleo
katika manunuzi ya serikali na
kuwajengea mazingira mazuri ya
biashara na kodi endelevu.
3. Tutawawezesha Watanzania kupata
mitaji ya biashara kwa masharti
nafuu kabisa.
4. Tutavutia uwekezaji na wawekezaji
wenye tija. Kuweka udhibiti wa
wahamiaji wasioleta tija wala
maslahi kwa Taifa.
5. Tutaimarisha sera ya ubia baina ya
Serikali na Sekta binafsi kwenye
maeneo muhimu ya kiuchumi na
kibiashara. Pia, kuwawezesha
Watanzania kuwekeza kwa njia ya
ubia na wawekezaji wenye mitaji
mikubwa bila kujali wanapotoka.
6. Tutaimarisha usimamizi kwa
kubadilisha mfumo wa Vyama vya
Ushirika nchini ili utokane na
uendeshwe na wakulima wenyewe
ikiwa na pamoja na kuwawezesha
kuboresha makazi kwa mpango wa
kushirikiana kujenga nyumba bora
7. Tutaanzisha na kuwezesha uanzishaji
wa viwanda vidogovidogo vinavyotoa
ajira kwa wingi kwa kuvihusisha na
vyuo vya ufundi na benki maalum kwa
lengo hilo.
AJIRA
1. Tutasimamia swala la ajira hasa kwa
vijana kwa kukuza elimu ya ufundi ili
waweze kujiajiri
2. Tutazipa kipaumbele sekta
zinazozalisha ajira kwa wingi hasa
za viwanda, kilimo, ufugaji, uvuvi na
utalii na kuzipa unafuu wa kodi ili
zikue kwa haraka.
3. Tutawapa wawekezaji wakubwa
katika sekta hizi upendeleo maalum
na viwango vya kodi nafuu.
NISHATI NA MADINI
1. Serikali itashiriki kikamilifu katika
uzalishaji wa nishati
2. Itatengeneza mazingara mazuri ya
kisera yatakayovutia na kuwezesha
ushiriki wa Watanzania na ubia kati
yao na wageni.
3. Serikali yangu itaupa uzalishaji
mkubwa wa umeme wa maji
kipaumbele namba moja, umeme wa
makaa ya mawe kipaumbele namba
mbili, umeme wa gesi asilia
kipaumbele namba tatu na umeme wa
urana kipaumbele namba nne.
4. Serikali itatoa vipaumbele muhimu
kwenye usambazaji wa huduma kubwa
ya umeme sehemu za uzalishaji
uliyolenga masoko ya ndani, ya nchi
jirani na ya nchi za kigeni.
5. Itapitia upya mikataba yote mikubwa
ya nishati na madini ili kubaini iliyo
mibovu na kuifanyia maboresho.
6. Serikali yangu itatumia sehemu ya
hisa zake kwenye raslimali kubwa ya
gesi asilia iliyopatikana hapa nchini
kama rehani kwenye kujichukulia
mikopo kwa ajili ya ujenzi wa miundo
mbinu ya mabomba ya gesi.
7. Serikali itatoza kodi na ada ndogo
zaidi kwa wazawa wenye ubia kati
yao na wageni kuliko zitakazotozwa
kwa wageni wasiowekeza kwa
kushirikisha wazawa.
8. Serikali itasitisha utoaji wa
misamaha ya kodi isiyo lazima kwenye
sekta ya madini, na badala yake
itawekeza kwenye kuongeza thamani
ya raslimali zake za madini.
9. Tutakuza nishati mbadala
kutamkomboa mwanamke kutokana na
adha ya kukata kuni
MALIASILI NA UTALII
1. Tutasimamia uvunaji na matumizi ya
rasilimali za Taifa kwa manufaa ya
kila Mtanzania wa kizazi hiki na
kijacho
2. Tutapiga vita ujangiri na kuimarisha
utunzanji wa hifadhi za taifa na
mazingira
3. Tutachochea ujenzi wa miundombinu
ya utalii nchini ikiwa ni pamoja na
ujenzi wa mahoteli na kuimarisha
mafunzo
4. Tutaongeza idadi ya watalii kufikia
milion mbili ifikapo 2020.
UTAWALA BORA, ULINZI WA NCHI NA
USALAMA WA RAIA
1. Tutasimamia Katiba mpya inayolinda
haki za msingi za wananchi na
kuweka bayana mipaka ya madaraka
ya serikali na viongozi, Bunge na
Mahakama.
2. Tutasimamia haki za raia na
kuangalia upya sheria kandamizi ili
wananchi kama Masheik wa Zanzibar
hawasoti jela kwa sababu za kisiasa.
3. Tutaimarisha mafunzo ya vyombo ya
Polisi hasa wapelelezi na waongoza
mashtaka ili wapate uwezo wa
kusimamia utoaji wa haki.
4. Tutavipa vyombo vyote vya ulinzi na
usalama nyenzo na kuboresha
mazingira yao ya kazi na maslahi
UZALENDO, UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI
1. Tutajenga uzalendo ili kila Mtanzania
aweze kutathmini mchango wake kwa
taifa kila siku
2. Tutaimarisha nidhamu, utendaji na
uwajibikaji katika Sekta ya Umma
3. Tutaimarisha mchango wa Wataalam
wetu, wanawake na vijana katika
kusimamia uchumi na kuwajengea
mazingira stahiki ya kazi pamoja na
mafao.
4. Tutapiga vita rushwa na ubadhirifu
katika sekta ya Umma na binafsi
5. Tutadhibiti na kupunguza matumizi
ya serikali ikiwa ni pamoja na kufuta
safari za watumishi serikalini
zisizokuwa muhimu pamoja na zile za
Rais na kupiga marufuku matumizi ya
mashangingi serikalini.
6. Tutadhibiti deni la Taifa kwa kuanza
na ukaguzi wa madeni ya serikali ili
kuhakiki jinsi yalivyotumika
7. Tutaimarisha uwazi na kuondoa usiri
katika shughuli za serikali na kuweka
bayana mikataba yote ya nchi ikiwa
ni pamoja na ile ya mafuta, madini
na gesi asilia
KUKUZA PATO LA SERIKALI
1. Tutadhibiti mapato kutokana na
raslimali kwa kupitia upya viwango
vya mirabaha kutokana na madini na
gesi asilia ili kuhakikisha kuwa
Tanzania inapata gawio stahiki.
2. Serikali itaanzisha Wizara maalum
itakayosimamia nishati ya gesi na
mafuta.
3. Tutaimarisha ofisi ya Msajili wa
Hazina ili kusimamia vema uwekezaji
wa Serikali katika mashirika na
mapato yake.
4. Tutahakikisha kuwa mashirika ya
umma yanaendeshwa kwa misingi ya
faida na uadilifu.
5. Tutadhibiti ukwepaji kodi za ushuru
wa forodha na kupiga marufuku
misamaha ya kodi holela ili kuokoa
mabilioni ya fedha yanayopotea kila
wiki.
6. Sambamba na hilo tutarahisisha
utaratibu wa kulipa kodi ili kuondoa
kero na mazingira ya rushwa. Kwa
kudhibiti makusanyo ya kodi
tutakusanya fedha za kugharimia
huduma za msingi kama afya na elimu
kikamilifu.
KUIMARISHA MUUNGANO
1. Tutaimarisha umoja, usalama na
udugu wa Watanzania na Muungano
kwa misingi ya haki na usawa
WANAWAKE, WATOTO NA WAZEE
1. Wanawake watapewa fursa na haki
sawa katika elimu na uchumi ili
waweze bila kuwezeshwa.
2. Tutahakikisha wazazi wanapata
fursa ya kuwa walezi na wafanyakazi
kwa kuongeza urefu wa likizo ya
uzazi
3. Tutaimarisha elimu ya watoto hasa
wasichana na kukuza fursa zao na
kukomesha ndoa za watoto wadogo.
4. Tutaongeza uwakilishi wa akina
mama katika ngazi zote serikalini na
mashirika yake kufikia asili mia
hamsini ifikapo 2020.
5. Wazee na wasiojiweza watapewa
posho ya kujikimu inayokidhi mahitaji
ya msingi itakayowawezesha kuishi
kwa heshima na kulinda utu wao
ndani ya familia na jamii zao.
SANAA, UTAMADUNI NA
MICHEZO
1. Tutaendeleza na kuwezesha vipaji
vya sanaa na michezo
2. Tutarudisha viwanja vya michezo
vilivyovamiwa
3. Tutafuta kodi zote za vifaa vya
michezo.
4. Tutadhibiti viwango na maadili ya
bidhaa za nje zinazoingizwa nchini
na kuzitoza kodi halisia
5. Tutajenga taasisi na vyuo vya
kukuza michezo ili kuhakikisha kuwa
ndani ya miaka mitano Tanzania
inashiriki kwa ushindi katika
mashindano ya kimataifa ya soka na
riadha
6. Tutalinda Hakimiliki za sanaa nchini
7. Tutafuta kodi za sanaa kwa wasanii
chipukizi ili kuwapa muda kwa
kujijenga.
SERA YA MAMBO YA NJE YENYE TIJA KWA
TAIFA
1. Tutakuza ushirikiano wa Kimataifa
wenye tija na Ujirani mwema.
2. Tutatetea haki za binadamu, usawa
wa nchi na kuimarisha ushiriki wa
Tanzania katika diplomasia ya
kimataifa.
3. Tutakuza umoja na ushirikiano wa
Umoja wa Afrika, Jumuia ya Afrika
Mashariki, SADC na Umoja wa
Mataifa.
4. Tutaimarisha Umoja wa Mataifa
ikiwa ni pamoja na kudai mabadiliko
ya mfumo ili kuleta usawa wa nchi
shiriki.
Ndugu Watanzania
Naomba nimalizie kwa kusema yafuatayo
1. Natambua kuwa uongozi ni dhamana.
Mkinichagua nitaienzi dhamana hiyo
kwa utendaji uliotukuka.
2. Nawaahidi Watanzania kuwa kwa
uwezo, akili, uzoefu na nguvu zangu
zote nitawatumikia. Nawaomba nanyi
mniahidi jasho lenu na uwezo wenu
wote ili kwa pamoja tuvuke.
Tutajikomboa toka utawala wa CCM
unaodumaza uchumi na maendeleo.
Tutaanza safari ya uhakika kuondoa
umaskini.
3. Mabadiliko pia ni kuthamini utu na
kukataa hadaa ya hongo ili kuuza
haki yako ya kuchagua. Msikubali
rubuni za uchaguzi kwa kupewa pesa
au vitu. Rushwa ya uchaguzi ndiyo
sera ya CCM. Ukikubali basi umeuza
pia haki na sauti yako ya
kuwalalamikia walio madarakani.
Imetosha. Tukatae. Tulinde utu na
haki zetu. Tuchague mabadiliko.
4. Mabadiliko ni fikra. Ni kufikiri na
kutenda tofauti. Hatuwezi kuendelea
kufikiri na kutenda kama kwamba
hatuna dharura ya maendeleo.
Kwanza tuanze kwa kufanya
mabadiliko na tujiamini kuwa sisi
kama Taifa tunaweza. Tunaweza
kujitegemea na kuleta maendeleo
yetu wenyewe bila kutegemea
wafadhili. Hii si ndoto. Nchi nyingi
zimefanikiwa kuondoa umaskini
katika kizazi kimoja. Tujifunze
kutoka kwao.
5. Tuwe taifa linalotumia raslimali zake
kujiendeleza na siyo kuwanufaisha
wageni na kuwafanya Watanzania
watwana katika nchi yao. Inabidi
tuache kuwa taifa ombaomba. Tuache
kuukubali na kuvaa umaskini kama
joho la fahari.
6. Mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa
na CCM. Tusitegemee kuwa leo wana
jipya. Ndiyo maana ahadi walizotoa
miaka thelathini iliyopita ndizo
wametoa juzi. Tukatae hadaa. Miaka
hamsini ya CCM imetosha.
7. Tunaamani kwamba tutashinda kwa
sababu Watanzania mpo nyuma yetu.
Watanzania mmeamua kuleta
mabadiliko. Kura yako ndiyo
itakayokuwa mkombozi wako.
Hakikisha unapiga na kuilinda kura
yako. Wakati wa mabadiliko ni sasa.
Mungu ibariki Tanzania. Asanteni sana
 
Mbona masha analialia alivyowekwa korokoroni?,alivyovunja sheria alijua hatakamatwa sababu alikuwa waziri wa mambo ya ndani
 
Hivi hii ndiyo Ilani ya Chadema au ni Hotuba aliyoandikiwa Lowassa ili aisome kwenye kituo cha Luninga? Aaah nimekumbuka tumeambiwa ilani ipo kwenye mtandao ngoja nikamnunulie bibi yangu wa kijijini Smart phone asipitwe na hii kitu, najua mwezi mmoa unatosha atajua jinsi ya kuperuzi mtandao!!!:A S shade::llama:
 
Back
Top Bottom