Jamani kulea mabinti ni kazi, kha!

Pole byshernger
sio mabinti tu
hata wavulana
ni kazi mno.

Hakikisha unakuwepo, sio unakuwa baba wa kukodi.

To me girls are more delicate more fragile, like eggs!Ukitetereka kidogo tu limeshapasuka: mimba,etc. And generally the society zooms more on girls than boys; they like to point dirt on girls more! At least that's my experience.
Endelea na kazi ya kulea Bishanga halafu chunga sana mtoto wa kike au kiume asitumie mgongo wa mama yake kuficha mambo yake. Kidokezo cha mgongo wa mama kutumika ni pale unapomwonya mtoto halafu mamake anaingilia kutaka yaishe akitoa kauli zenye kusema:"Watoto wa siku hizi ndivyo walivyo baba upendo,achana nao, utapata presha bure"
 
acha kupasua kichwa bure, hapo mwanao anausoma ulimwengu aweze kuujua umekaaje..... note usisahau siku moja kumwonya kuhusu njia sahihi apaswazo kuzipitia!!!!
 
Ndugu yangu Bishanga kulea hakuna formula wala kuwa mchungaji sio kwamba uchungaji wako ndo unalea watoto hapana,kuwa mchungaji na kumlea mtoto katika maadili ni vitu viwili tofauti,tuangalie watoto wanajifunza nini wakiwa wadogo kama kuna kitu anakifanya akiwa mdogo na hukipendi na hukuchukua hatua stahiki angali mdogo ujue akikua huwezi kirekebisha.Mfano mtoto anaweza akawa mdogo mzazi unamtuma kitu anakuambia sitaki na wewe unainuka kwenda kukichukua unadhani akikua atakutii?kwa mfano una mtoto wa kike na nyumbani una house girl kila kitu anafanya house girl huyo binti yako hutaki ajifunze hata kuosha vyombo unadhani akikua ataweza kufanya hivyo vitu kama hakujifunza akiwa mdogo?hapo hata kwa mume wake atakuwa mzigo,mume anataka ugali mke anasema mi sijui kupika ugali njoo upike mwenyewe,sio anafanya makusudi ni kweli hajui maana hakufundishwa huo ni mfano mdogo sana lakini nataka kukuambia tu mara nyingi mtoto analelewa na mazingira ya nyumbani kwao kama wazazi hawana muda wa kumfundisha atafundishwa na anaocheza nao au atafundishwa na TV kwa enzi hizi tulizonazo,nitakupa mfano hai mimi ni mtoto wa kiume lakini katika utoto wangu wazazi walinifundisha kuheshimu kila mtu mkubwa kwa mdogo tajiri kwa maskini bila kubagua,pia walinifundisha kujitegemea kwa mfano kufua nguo zangu mwenyewe,kuosha vyombo,kupika na hata kufanya usafi wa nyumba,hayo yote tuliyafanya kwa zamu maana watoto wa kiume tulikuwa lukuki katika familia baada ya kukua na kuanza kujitegemea ndo nikaanza kujua kile wazazi walichonifundisha kilikuwa na umuhimu gani ilihali wakati wa utoto niliona kama adhabu hivi.Kwa hiyo kuwa mzee wa kanisa,nabii,askofu,sheikh haimsaidii mtoto kuwa na tabia nzuri hiyo karama uliyonayo unatakiwa kuitumia sasa kulea mtoto hapo ndo atakuwa na maadili mazuri lakini sio kwa kuwa wewe mchungaji Mungu akufundishie watoto kuwa na tabia njema.Makundi pia anayokuwa nayo mwanao yana ushawishi mkubwa sana kaitka kujenga tabia ya mwanao,chunga sana aina ya marafiki wa mwanao
 
Kuna kitu ambacho kama una nyumba huwezi epuka,"kuishi na ndugu",nashauri kama una mtoto wa kiume usiruhusu alale na ndugu wa kiume yeyote yule,hakikisha analala chumba cha peke yake na kiwe jirani na chumba unacholala wewe mzazi ili ujue kila kinachoendelea,kadhalika na mtoto wa kike,lakini siku hizi watoto wagumu zaidi kulea ni wa kiume.
 
Back
Top Bottom