Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,196
Majambazi yafanya kufuru Dar
Na Moshi Lusonzo
24th January 2010
Wimbi la majambazi linazidi kutikisa nchini, ambapo jijini Dar es Salaam watu wawili wameuawa kwa risasi na wengine wamejeruhiwa vibaya baada ya kundi la majambazi kuvamia mitaa miwili na kuiteka kwa muda wa saa 1.30.
Tukio hilo limetokea juzi eneo la Kimara Temboni, ambapo majambazi hayo yalianza operesheni hiyo ya kupora mali kuanzia majira ya saa 1:30 hadi saa 3:50 usiku.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Esaya Kalinga, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini hakuwa tayari kuzungumzia zaidi kwa kueleza yupo eneo la tukio.
Katika matukio hayo, majambazi hayo yaliyokuwa yamesheheni kila aina ya silaha ikiwa pamoja na bunduki za kivita, bastola, mapanga na mashoka, yalisababisha vifo vya watu wawili baada ya kuwapiga risasi pamoja na kuwajeruhi watu wengi kwa kuwakata mapanga na shoka.
Hata hivyo, kati ya watu waliokufa mmoja ameweza kutambuliwa kwa jina la Godfrey Chandeu mkazi wa Kimara B.
Waliojeruhiwa wametajwa kuwa ni Editha Peter (36) mumewe Peter Temarilwa (41) na mfanyakazi wao Sospeter Peter (2, Renatha Malya (33), mkazi wa Kimara Temboni pamoja na Mhasibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Gelvas Macha (41) mkazi wa Kimara Temboni.
Majeruhi wote wamelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa ya Muhimbili (MOI).
Wakisimulia tukio hilo, mmoja wa watu walioshuhudia tukio hilo, Salum Bakari, alisema kundi la majambazi idadi yake haijafahamika, walivamia eneo la Kimara Temboni majira ya saa 1:15 usiku, ambapo watu wawili wenye silaha walisimama mwanzo na mwisho wa mtaa huo na kuanza kuwaamuru watu wote wanaofika mtaa huo kulala chini na kisha kutoa vitu vyote walivyokuwa navyo.
Mmoja wa watu hao, Salum Bakari alisema katika tukio hilo watu wengi walijikuta wakiwa wametekwa na kukusanywa pamoja na kuanza kupigwa kwa kutumia mapanga na mashoka huku wakiwashurutisha kuonyesha kila kitu walichokuwa nacho.
"Ilikuwa ni hali ya kutisha, watu wengi walijeruhiwa kwa kipigo na mmoja alikufa baada ya kupigwa risasi kutokana na kutokea mabishano wakati walipomuamuru kulala chini," alisema Bakari.
Hata hivyo, Renatha Malya ambaye ni mmoja wa waliojeruhiwa alisema mara alipofika eneo hilo, alishtukia mtu akimfuata kwa nyuma na kumwambia kulala chini na alipohoji kwa nini alale chini, alishtukia akipigwa kitu kichwani na papo hapo alipoteza fahamu.
Baada ya kuhakikisha wamewateka watu wengi walianza kuwapekua kila mmoja na kuchukua kila kitu ikiwemo pochi, mikoba, simu na pesa walizokuwa nazo na kuondoka eneo hilo.
Operesheni hiyo haikushia hapo, watu hao walikwenda katika mtaa wa jirani wa Kimara B, huko waliwapiga risasi watu pamoja na kufanya uporaji wa mali kwa watu mbalimbali.
Majeruhi mwingine anayeishi mtaa huo, Edither Peter, alisema watu hao walimvamia wakati akiingia ndani ya nyumba yake, ambapo katika tukio hilo walijeruhiwa kwa kupigwa shoka kichwani yeye,mume wake na mfanyakazi wake. Pia majambazi hayo yalimfungia ****** mama mkwe wake ambaye alikuwa amelala sebuleni.
Alisema watu hao walichukua pesa taslimu shilingi milioni 1.8, simu nne, mkoba mmoja na kompyuta yake ya mkononi.
Aidha, wakati wakiondoka eneo hilo walimpiga risasi jirani yake aliyekuwa akipita eneo hilo na alifariki papo hapo.
Afisa Uhusiano wa MOI, Almas Jumaa alisema majeruhi wote waliolazwa hapo wanaendelea kupatiwa matibabu, lakini hali zao bado mbaya kutokana na majeraha waliyokuwa nayo.
CHANZO:NIPASHE JUMAPILI
My take:
Ufike wakati sasa viongozi wajifunze kuwajibika kutokana na uzembe wao. Katika hali ya kawaida, baada tu ya lile la Ukerewe, ilikuwa IGP na waziri wa mambo ya ndani waachie ngazi.
Halafu kingine, hivi idara ya usalama wa taifa nchini ilifutwa? Kama ipo inafanya kazi gani? Si isaidie kulinda usalama wa raia? Au usalama wa taifa manake nini kama watu wanauawa kila kukicha?
Shida na hawa majambazi wanatuonea sisi raia masikini, wanatuua kwa ajili ya visimu tu, si wavamie huko majumbani kwa mawaziri?
However, gazeti la juzi lilisema polisi ni member wa ujambazi, sasa wa kutulinda nani? Wadau mnasemaje kuhusu mwelekeo wa nchi?
Kuna tetesi kwamba chama xx kinakusanya hela ya uchaguzi, kuna ukweli kuhusu hilo?