MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,562
Na kweli mwali ila tu nafikiri waangalie namna ya kumkuza kwenye maadili mmema. Kwa jinsi nilivyomsoma naona kama kuna kipunje cha kiburi!! Kama anaambiwa aandae meza, yeye anatandua meza kwa madai ya kuwa mamake kakosea hakumwambia aandae chakula kwa nini atandue na kukaa kuwaangalia kusubiri wamuulize kwa nini ametandua?? Kwa nini akiambiwa aandae meza; asimkosoe tu mama yake kuwa......sio kuandaa meza mama, ni kuandaa chakula .............huku akifanya kile alichokuwa anajua mama yake anakimaanisha?!lol! umenifurahisha mpendwa. wanawake smart namna hii, akina nyamayao wa kesho huwa hata ku-date mfumo dume hawawezi.inaishia date ya kwanza,lol! amkazanie tu kusoma ili akutane na civilised mwenzie!
Na wasiporeduce hii speed (hasa kwenye kubishana na wazazi wake kwenye vitu vya kmsingi, iko siku atawaumbua mbele ya wageni). Hakawii kuropoka wewe baba umezoea kuja umelewa hadi unakokotwa .....imtoke mbele ya wageni. Ndio anahoji na kukemea tabia mbaya juu ya mzazi wake mlevi lakini sehemu na namna atakavyokemea lawama zote zitakujamrudia mamake kuwa kamdekeza, kamlea vibaya.
Hapana wampunguze speed kwa mambo yasiyo na maana la sivyo wanalea maradhi. Mambo ya msingi ambayo ni haki yake kuhoji na kudadisi wamuongoze ahoji na kudadisi kwa adabu.