Jamani,Huku si kuchochea vurugu:DC atuhumiwa kushusha bendera!!

sijui nini

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
2,553
1,285
VYAMA vya CUF na CHADEMA, wilayani Pangani, mkoa wa Tanga, vimemlalamikia Mkuu wa Wilaya hiyo, Zipora Pangani, kwa kitendo chake cha kushusha bendera ya vyama vyao bila sababu za msingi. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Tanzania Daima, jana kwa njia ya simu, walisema walishangazwa na kitendo hicho kwani hakikuwatendea haki hasa wakati huu wa kampeni.
Katibu wa Wilaya CUF, Kitwana Sefu, alisema DC Zipora, alifanya hivyo kwa lengo maalumu ili kumuonyesha mgombea mwenza wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Gharib Bilal, alipopita juzi katika eneo la Bweni kuwa hakuna upinzani.
Alisema pamoja na kujaribu kuwachokoza wana CUF, bado wanaamini hawatakubali kuchokozeka ila wataonyesha kuwa upinzani katika wilaya hiyo upo na utafanya vema.
Naye Mkuu wa Wilaya huyo, alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, alikiri kuwaagiza bendera hiyo ishushwe kutokana na kitendo cha kupandisha mabango.
Mbali ya CUF, DC Pangani alisema bendera ya CHADEMA ilionekana iko katika maeneo ya ofisi za serikali, ambapo haparuhusiwi kuwepo bendera kisheria.
Naye mgombea wa CHADEMA, Mzee, alisema kweli alikutana na mkuu wa wilaya na wamekubaliana kila mmoja, achukue jukumu la kuepusha vyanzo vyote vya uvunjifu wa amani ili zoezi hili la uchaguzi liweze kufanikiwa.
 
Katibu wa Wilaya CUF, Kitwana Sefu, alisema DC Zipora, alifanya hivyo kwa lengo maalumu ili kumuonyesha mgombea mwenza wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Gharib Bilal, alipopita juzi katika eneo la Bweni kuwa hakuna upinzani.
Au ndo kuwatafutia JWTZ sababu ya kuonekana wapinzania wana fujo wakati wa uchaguzi???
 
Back
Top Bottom