Jamani housegal wangu.........

asanteni kwa ushauri nimejitahidi kumshauri kwa kutumi ushauri mlionipa, kiukweli imesaidia kiasi ameelewa na amepunguza kulia
 
Wanaume sijui roho zao zikoje!wana roho ngumu hawa viumbe wala hawa hisi vibaya kumfanyie msichana hivi, mwambie avute subra yatakwisha na atasahau,huyo bwana nae atapata wakumsugua roho kuliko alivyo mfanyia mwenzie.
 
Kuweni naye karibu mkimwambia hiyo ni kawaida, atazoea. Nyumbani awaambie wamebadili tarehe mpaka siku ingine itayopangwa.
Jamaa alitumia lugha ya kuoa, kambpitia sasa kamtosa. Mpe pole na mwambie huu ndo ulimwengu na hawa ndo binadamu.
 
nawasabahi kutoka moyoni, natumai mu wazima wa afya njema.

Naombeni mnisaidie jinsi ya kumsaidia huyu binti yangu apate ahueni ya mzigo wa mawazo yanayomfanya alie kila cku. Kisa ni hiki.

Nilikuwa nakaa nae ktk mkoa flani,wakati wa likizo nilikwenda nae dar kwa mapumzko. Tukiwa huko alifahamiana na kijana mmoja na akamwambia anataka kumuoa, likizo ikaisha tukarudi mkoa, kwa kipindi chote hcho ckuwa nafahamu chochote, juzi ndg yake toka kjjn, alinipigia na kunieleza kuhsu uchumba wa huyo kjna na huyu binti kuwa tarehe 22.9. Wanapeleka posa, nikasema ouuk. Sasa leo baada ya kutoja job, binti kaangua kilio kikubwa sana nikajua kafiwa.....oooooooh shittt, akanionyesha sms toka kwa mchumbake kuwa hatamuoa tena wazazi wake wamekataa. Binti analiaa atawaambia nn ndg zake hali wanajiandaa kwa trh 22.9. Nimejitahd kumshauri chozi halikatki. Msaada tafadhali na poleni kwa ujumbe mrefu.

Wasiwasi wangu i kuwa yawezekana binti alimhonga kijana tunda na baada ya kijana kulitafuna bila hata ya huruma na hakulipenda au ndizo mbinu zake.........................za kutafunatafuna matunda ya walalahoi kwa mkopo usiolipika basi kachanja mbunga na hilo jingine ni kisingizio tu...........................alimwahidi vipi atamchumbia wakati hata hajapata baraka za wazee............mimi hawa vijana ninawafahamu kwa utapeli wao.................kwanza kampime mtoto wa watu kama hajaunganishwa kwenye mtandao wa wanavirusi.................pili pima kama hana uja wepesi.......................lol
 
jaribu kumtia ila yule aliekua anataka kumuoa ili amuene kua alikua si wa maana na hafai hata kidogo na mungu amemuwezesha kumnusuru na ndoa hiyo!
 
Sasa siawaambie ukweli kama ulivyo wazee wake. Na wewe hata kumshauri aseme kweli huwezi? unanshangaza sana!

Au kisha bebeshwa mzigo? semeni ukweli! maana kama ni posa tu kuvunjwa, inasikitisha lakini si kihivyo.
 
Back
Top Bottom