Mkutano wa Bilal wakosa watu,
Magari yakodishwa kuuokoa
Fukuto la kura za maoni lingali linachemka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiasi cha kuathiri mahudhurio ya wanachama kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Mweza, Dk. Mohammed Gharib Bilal, hali iliyolazimu kusafirisha watu kwa magari baada ya uwanja kuwa mtupu.
CCM ilalazimika kuwasafirisha wanachama wake kwa malori ili washiriki mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza katika kata ya Dodoma- Makuru mkoani Dodoma jana.
NIPASHE ilishuhudia watu waliovaa sare zinazotumiwa na CCM zikiwa na rangi ya kijani, njano na alama ya jembe na nyundo, wakiwa wamebebwa kwenye malori na kushushwa katika uwanja wa mikutano uliopo kwenye kata hiyo.
Miongoni mwa watu waliokuwa kwenye malori hayo ni wasanii wa vikundi mbalimbali vya burudani.
Mkutano huo ulipomalizika, malori yaliyotumika awali, yaliwabeba wasikilizaji wa mkutano huo na kuwarejesha kwenye maeneo tofauti yaliyosemekana kuwa karibu na makazi yao.
Kata hiyo inasadikiwa kuwa ngome ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hasa baada ya mgombea udiwani aliyeshinda katika kura za maoni katani humo, Ally Biringi, kuihama CCM na kujiunga na chama hicho cha upinzani.