Jamani CCM iende wapi?

Wakijiunga na chadema wote kabisa mpaka wale wenye sifa mbaya, basi ni dhahiri kabisa kwamba chadema itaanguka mwereka wa mende.

Kilicho najisi mapambano ya uhuru na kuharibu maana ya uhuru wa mwafrika ni kanisa kupandikiza watu watu wake kupitia nyerere. Kilichofuata ni kuanzisha raia wa daraja la pili na la kwanza. CDM isije kudhani waislamu hawakupata fundisho kutoka katika hili, tutaendelea kuwatumia watu wenye nia njema na maslahi ya waislamu waliopo ndani ya CDM.
 
Wakijiunga na chadema wote kabisa mpaka wale wenye sifa mbaya, basi ni dhahiri kabisa kwamba chadema itaanguka mwereka wa mende.

Nafikiri hakuna mwenye sifa mbaya ,isipokuwa mfumo uliomo ndani na utumiaji wake humo CCM ni dhaifu au ni ule wa hadithi ya nchi ya kusadikika ,Sasa huko CDM wakishajiunga bila ya shaka yeyote watakuwa wapo kwenye safe heaven.

Usiniambie kuwa CDM haiwataki au haitaki na kuwa na hamu ya kuvuna vigogo wa CCM ,si huwaga mnawatangazaga kwa kishindo kikuu? Huko ndio kimbilio lao kwani ndiko kunakoelekea kuwa na mshiko.
 
Kilicho najisi mapambano ya uhuru na kuharibu maana ya uhuru wa mwafrika ni kanisa kupandikiza watu watu wake kupitia nyerere. Kilichofuata ni kuanzisha raia wa daraja la pili na la kwanza. CDM isije kudhani waislamu hawakupata fundisho kutoka katika hili, tutaendelea kuwatumia watu wenye nia njema na maslahi ya waislamu waliopo ndani ya CDM.
Kuwa makini ndugu yangu, hisia za kidini ni hatari sana kwa amani na ustawi wa taifa lolote lile duniani. Tukianza kuliendesha taifa hili kwa kila mtu kufikiria mustakabali wa dini yake badala ya taifa hatutafika popote. Ni lazima tufikie mahali pa kuweza kutofautisha mambo. Pale panapostahili utaifa tuweke utaifa, na pale panapstahili dini tuweke dini. Tusipeweza kuyatenganisha maeneo haya mawili, itakuwa ni ishara tosha kwamba bado hatujastaarabika kama taifa. Kama kweli kanisa lilipandikiza watu kupitia Nyerere, je! waislamu wengi tulionao leo katika serikali walipandikizwa na nani na kupitia mgongo wa nani? Nafikiri si vizuri kulaumu kundi fulani la watu pasipo kuwa na "concrete evidence" kuhusu lawama zetu. Mwisho nasema, Jihadhari sana kuendekeza hisia za udini, maana madhara yake hayachagui kwamba huyu ni mwislamu na huyu ni mkristo, bali yanawafagia wote.
 
Back
Top Bottom