Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,013
- 144,371
Hawa watu wa bodi ya mikopo ni watu wasiojua umuhimu wa kutoa taarifa zao mapema kwa wahusika.Hata kama kuna waliofanya makosa isiwe sababu ya kuchelewesha kutoa majina.TCU wameongeza muda mpaka tfh 07/09/2012,sasa ina maana hawa bodi wataendelea kusubiri kisa kuna makosa yamefanyika?Deadline nyingi za TCU na HELSB zimeshapita lakini hawa bodi hakuna kinachoendelea kuhusu kutangaza majina.Mbona TCU wao wametoa selection zao kwa wale ambao hawakuwa na matatizo?Sasa kwa nyinyi bodi ya mikopo mnashindwa nini?
Najiuliza kulikuwa na umuhimu gani wa kuanza kufanya maombi ya mkopo mapema kama mpaka leo mmeshindwa kuwajulisha waombaji ni kiasi gani watarajie kupata kutoka bodi?Nani asiyejua ugumu wa kutafuta na kupata fedha?Muda uliobaki kwa vyuo vingi kabla ya kufunguliwa ni chini ya mwezi mmoja ila nyinyi mnakuwa kama hamlioni jambo hili!
Jamani kujali muda ni jambo la msingi sana, kwani litaepusha matatizo mengi kwa wanafunzi walioomba mkopo.