Jamani Angalieni ITV...

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Kuna kijana anaitwa Humphrey Polepole anaitetea serikali kwa njia ya mzunguko. Anasema si wajibu wa serikali kutoa ajira na Makampuni makubwa ya ndege duniani si ya serikali.
 
msimshangae huyu kijana kwani toka enzi akisoma Azania alikuwa akiwachongea wanafunzi kwa walimu, ni tabia yake , na vitamasha vya kuwakilisha vijana ndivyo vinampa vijisenti vya kuweza kudhani amepata kushibisha tumbo,,,
 
Kuna kijana anaitwa Humphrey Polepole anaitetea serikali kwa njia ya mzunguko. Anasema si wajibu wa serikali kutoa ajira na Makampuni makubwa ya ndege duniani si ya serikali.

Huyu kijana ama ni mbumbumbu wa viwango vya kimataifa au ana mapepo! Kama kweli serikali haina wajibu wa kutoa ajira kwa nini serikali hiyo hiyo kupitia kwa wanasiasa wake inazunguka nchi nzima ikiahidi kutoa ajira? Amesoma ilani ya chama kinachoongoza serikali kwa sasa? Inasemaje hiyo ilani kuhusu ajira? In his right mind huyu kijana anaweza kusema kwa nini wananchi wanailalamikia serikali kuhusu ajira na sio kuli, au mama muuza vitumbua kwa mfano?

Na kuhusu mashirika ya ndege, kama serikali haina nia ya kuwa na shirika la ndege kwa nini wanatumia kodi za walalahoi kulipa wafanyakazi wa ATC? Inaelekea huyu bwana mdogo kafanya research kuhusu mashirika makubwa ya ndege, sasa anaweza kutuambia kama serikali za hizo nchi zenye mashirika makubwa ya ndege zina shares? kwa mfano, serikali ya Kenya ina share zozote kwenye Kenya Airways? Au British Airway -Her Majesty's government ina share zozote kwenye BA? Au KLM- serikali ina share huko?

Ushauri kwa Nape: shauri serikali ya chama chako ijitenge na huu ushwauri uchwara, anawaaribia sifa (kama bado sifa zipo).
 
siko kwenye TV lakini kama kasema hayo basi
hayuko TZ. Hajui kinachoendelea. Hajui siasa. Hajui maana ya serikari. Hajui katiba inasemaje.
 
Huyo kijana sisi wengine hatumfahamu, pia hatupo kwenye tv, jaribuni kutoa maelezo kidogo yanayomuhusu ili nasi tumfahamu.
 
Naamuenzi Baba wa Taifa kwa kucheza bao.
Huyu naye alisema angalau yeye anamwenzi baba wa taifa kwa kucheza bao mchezo ambao Mwalimu alitaka uwe wa kimatakifa. hadi mwaka 2015 tutasikia mengi.
 
msimshangae huyu kijana kwani toka enzi akisoma Azania alikuwa akiwachongea wanafunzi kwa walimu, ni tabia yake , na vitamasha vya kuwakilisha vijana ndivyo vinampa vijisenti vya kuweza kudhani amepata kushibisha tumbo,,,

teh teh teh teh, kumbe U knw da guy, kweli ndivyo alivyo, me nilisoma nae" Mbuyuni primary" pale, alikua anatumiwa sana na walimu,. So ni mtu wa kutumiwa always! Nasihi ni gamba jingine linalochipukia..
 
siko kwenye TV lakini kama kasema hayo basi
hayuko TZ. Hajui kinachoendelea. Hajui siasa. Hajui maana ya serikari. Hajui katiba inasemaje.

Yetuwote vipi tena
huyu Jamaa sio kwamba hayupo tanzania. huyu hayupo duniani. hana ufahamu wowote
na maswala ya kiuchumi at the macro level.
 
siko kwenye TV lakini kama kasema hayo basi
hayuko TZ. Hajui kinachoendelea. Hajui siasa. Hajui maana ya serikari. Hajui katiba inasemaje.

HAMPHREY POLEPOLE.
Mkurugenzi mkuu wa TANZANIA YOUTH COALITION.
Ni NGO iko k'nyama dsm inayodai eti kuunganisha vijana wote tz.
Hawa jamaa ni pro-magamba mpaka wanaboa.
Ukitaka kushirikiana nao ni mpaka uwe pro-serikali ya magamba kama wao.
Wanaboa sana. Ni vijana lakini bado hawajafunguka ki-mtazamo.
Sijui ni vijana gani wanaowawakilisha, but it is very sad kwamba hawa ni stambling block against youth development in the country.

They disappoint alot.
 
Kijana ni mtupu ile mbaya .Nimemuona anaongea hadi anaona aibu ana angalia chini muda nilishangaa nikajiuliza naye huyu kasoma ? Asijekuwa yuko hapa JF akajiita a great thinker
 
Back
Top Bottom