Jamaa atembea Mtupu kwa TZS 30,000

Mkaa Mweupe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
654
183
Ilikuwa ni siku ya Jumamosi, majira ya saa 11 jioni ambapo mitaa ya Mbezi Beach ilikuwa imetulia na watu wakiendelea na starehe zao. Mara ghafla likazuka kundi la watu wakimfuata jamaa aliyekuwa mtupu huku wakipiga kelele.

Mimi nilidhani kuwa huyu jamaa alikuwa amechanganyikiwa. Mawazo ya awali yalikuwa huenda huyu mtu kavuta bhangi na imemzingua, kwa sababu ni mtu anayefahamika sana hapa mtaani.

Alipofika kwenye maeneo ya bar mmoja hapa mtaani, aliingia hapo na kuzua tafrani kwa wateja kwani nao walidhani jamaa amekuwa chizi. Jamaa akakaa na kuagiza bia huku angali mtupu. Akasikika akijigamba,"Alidhani mi nitashindwa na hiyo elfu thelathini nimeshakula? Kwani ni mwanamke gani ambaye hajawahi kuiona au haijui?..." Alisikika akijigamba. Kama mtu ambaye yu na nguo akakaa kwenye kiti mguu mmoja juu bila ya wasi.

Baada ya kama dakika kadhaa, akatokea kijana mwingine aliyemletea nguo zake. Huyu jamaa akachukua nguo na kuelekea msalani ambapo baada ya kuvaa alitoka huku lile kundi likiendelea kumshangilia kwa ushujaa wake.

Maswali ya kujiuliza:
1. Hivi watanzania ndo tumefikia huku?
2. Hii hali ya uchumi imetufanya watu tushindwe kufikiri.
3. Hali hii ni kuwa amejidhalilisha yeye tu au jamii nzima?

Waungwana tusaidiane mawazo.
 
Eeeh hii ni kiboko, kama ni ujasiriamali naona huu una mwelekeo wa kipumbavu zaidi! Maadili yetu naona yanazidi kudidimia kwa kasi kwa sababu ya kusaka noti. Tufanye hima, stori unazoweza kuzisikia mtaani siku hizi nyingi ni za mambo ambayo zamani hayakufikirika kabisa (ushoga, sijui jicho na uchafu mwingine mwingi tu kama huu)
 
Hii imenikumbusha ishu ya kule Galanos secondary 2004,jamaa alitembea uchi kwa kuahidiwa sh.500 mbele ya wasichana na wapita njia.huu ni ugonjwa wa akili kabisa huu
 
Ilikuwa ni siku ya Jumamosi, majira ya saa 11 jioni ambapo mitaa ya Mbezi Beach ilikuwa imetulia na watu wakiendelea na starehe zao. Mara ghafla likazuka kundi la watu wakimfuata jamaa aliyekuwa mtupu huku wakipiga kelele.

Mimi nilidhani kuwa huyu jamaa alikuwa amechanganyikiwa. Mawazo ya awali yalikuwa huenda huyu mtu kavuta bhangi na imemzingua, kwa sababu ni mtu anayefahamika sana hapa mtaani.

Alipofika kwenye maeneo ya bar mmoja hapa mtaani, aliingia hapo na kuzua tafrani kwa wateja kwani nao walidhani jamaa amekuwa chizi. Jamaa akakaa na kuagiza bia huku angali mtupu. Akasikika akijigamba,"Alidhani mi nitashindwa na hiyo elfu thelathini nimeshakula? Kwani ni mwanamke gani ambaye hajawahi kuiona au haijui?..." Alisikika akijigamba. Kama mtu ambaye yu na nguo akakaa kwenye kiti mguu mmoja juu bila ya wasi.

Baada ya kama dakika kadhaa, akatokea kijana mwingine aliyemletea nguo zake. Huyu jamaa akachukua nguo na kuelekea msalani ambapo baada ya kuvaa alitoka huku lile kundi likiendelea kumshangilia kwa ushujaa wake.

Maswali ya kujiuliza:
1. Hivi watanzania ndo tumefikia huku?
2. Hii hali ya uchumi imetufanya watu tushindwe kufikiri.
3. Hali hii ni kuwa amejidhalilisha yeye tu au jamii nzima?

Waungwana tusaidiane mawazo.

Angefunguliwa mashitaka kwani ni kosa la jinai kutembea uchi mitaani kwa mtu mwenye akili timamu
 
Mawazo ya awali yalikuwa huenda huyu mtu kavuta bhangi na imemzingua, kwa sababu ni mtu anayefahamika sana hapa mtaani.

Alipofika kwenye maeneo ya bar mmoja hapa mtaani, aliingia hapo na kuzua tafrani kwa wateja kwani nao walidhani jamaa amekuwa chizi. Jamaa akakaa na kuagiza bia huku angali mtupu. Akasikika akijigamba,"Alidhani mi nitashindwa na hiyo elfu thelathini nimeshakula? Kwani ni mwanamke gani ambaye hajawahi kuiona au haijui?..." Alisikika akijigamba. Kama mtu ambaye yu na nguo akakaa kwenye kiti mguu mmoja juu bila ya wasi.

Mkaa Mweupe, mnaweza kuwa mwamuona huyo jamaa ni mzima, kumbe ana tatizo fulani. Kama mngeweza kumfikisha hospitali na kupimwa ndio tungesema kweli aliamua kupata 30,000 na kujidhalilisha na vilevile kuidhalilisha jamii. Ila ulivyoiandika hii, una fani ya uandishi wa habari!!!.
 
Angefunguliwa mashitaka kwani ni kosa la jinai kutembea uchi mitaani kwa mtu mwenye

UCHI UKOJE JAMANI!!KAMA HIVYO HAO MALAYA WA JOLI WANGEFUNGULIWA KILA SIKU NA HAO WA AFRIKASANA!!!
Mwache atumie haki yake!!!
 
Height of stupidity.Period.
Itz one of the many scenarios that support NN philosophy of "Miafrika....".
 
sidhani kama huyo jammaa ana sound-mind kama wengine walivyosema. ingekuwa ameonyesha hizo nyeti zake kulekule beach kidogo isingetisha sana, lakini kwa yeye kwenda bar mbele ya kadamnasi, inatufanya tusisimke mwili kwa aibu. He must be crazy for sure!
 
Jamani kutokana na muda niliokuwa nao wakati naanzisha hii thread kuwa ni finyu, sikuweza kuwapasha kinaga ubaga jinsi jambo hili lilivyojiri.

Maeneo ninayoyazungumzia ni eneo ambalo ni mbali kabisa na eneo la Beach. Nadhani kama wenzangu ni watembezi kidogo katika jiji letu la Kandoro, eneo hili ni ile njia inayochepuka upande wa kulia kama unatokea mjini kuelekea Tegeta eneo al maarufu kama Makonde.

Huyu jamaa ukishuka tu pale makonde utamkuta na unaweza kupata hii stori kwa undani.

Siku hiyo ya dahani, alikuwa na wenzake eneo hilo la soko jipya ambapo ubishani ulianz. "OOhh hauwezi kutembea mtupu!", jamaa akauliza, "Una kiasi gani nikuonyeshe kuwa naweza?" Jamaa akapanda dau,"hii hapa elfu thelathini, lakini hauichukui mpaka umenikabidhi nguo zako". Kijana wa watu kuona msimbazi tatu wakati kazi yake inampatia sanasana elfu tano kwa siku, akaamua kujitoa kimasomaso.

"Aahh anatishia mbona anaanza kuvua flana, vua na hiyo track...", alisikika kijana mmoja akimpamba. Jamaa akavua track mpaka ile ya ndani. Akaambiwa sasa zoezi linaanzia pale mwanzo wa masoko mpaka kwenye ile bar maarufu pale mtaani.

Jamaa akaenda kupitia nyuma ya magenge na kuibukia mahala husika. "Astakaful lah", akina dada wakaanza kukimbia wakidhani jamaa kawa chizi. Bila ya wasi jamaa akaanza kupanda na mtaa, tena katikati ya barabara huku lile kundi lilomshawishi likimfuata. Ndio ikawa jamaa amefika kwenye hiyo baa.

Baadhi ya vijana walidai ya kuwa walimsihi asifanye hivyo ila kutokana na jazba aliyokuwanayo aliwaona kama wanambania riziki...

Waungwana mupoo...
 
Hii imenikumbusha ishu ya kule Galanos secondary 2004,jamaa alitembea uchi kwa kuahidiwa sh.500 mbele ya wasichana na wapita njia.huu ni ugonjwa wa akili kabisa huu

alikua anatokea amri abeid au???
 
Hii imenikumbusha ishu ya kule Galanos secondary 2004,jamaa alitembea uchi kwa kuahidiwa sh.500 mbele ya wasichana na wapita njia.huu ni ugonjwa wa akili kabisa huu

alikua anatokea amri abeid au???Tehe tehe
 
Baada ya kama dakika kadhaa, akatokea kijana mwingine aliyemletea nguo zake. Huyu jamaa akachukua nguo na kuelekea msalani ambapo baada ya kuvaa

Kwanini sasa alikwenda msalani kuvaa na badala yake angevalia pale pale. Sikuona sababu ya uchizi wake kwenda vaa kwa kujificha msalani ingali alishaweza kujianika kwa wananchi.

he he, Kweli Bongo kuna kazi sanaaa.
 
Last edited:
alofanya hivi hana tofauti na wale wanaouza nchi kwa maslahi yao.....!!!!
 
Naona hali hii mbaya ya uchumi inafanya psychologically watu wawe insane...this guy is insane i think......Yaani kama ana watoto sasa ni anawafundisha nini watoto wake?....kuwa you can do anything walk out naked just for the sake of tz30,000?...anyways yote maisha kila mtu ana mbinu yake ya kuishi i guess!
 
Back
Top Bottom