Jamaa amnasa vibao afisa uhamiaji

pamiho

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
271
35
Kaka mmoja mwenye asili ya Somalia, raia wa Kenya anayesoma nchini Malaysia, wiki iliyopita alijikuta akizua zogo kwenye ofisi ya uhamiaji. Tukio hiko lilitokea mida ya asubuhi baada ya kaka huyo ( anajiita Mzee) kumpatia passport mhudumu (dada) naye akaipokea passport kwa kutumia tissue paper

Kaka huyo alishikwa na hasira sana kwa kitendo hicho ndipo akaamua kumchapa vibao dada huyo mwenye asili ya kihindi kwakuwa alionesha dharau kwa mteja huyo (mzee)

Mzee alikamatwa na polisi akawekwa mahabusu siku 3 kisha uongozi wa uhamiaji ukaamua kuitisha kikao ili wamsikilize kijana huyo. Ndipo alipowaeleza kuwa alilazimika kufanya vile kwakuwa nchi yake yenye heshima ilidhalilishwa na huyo dada.

Uongozi ukaamuru kijana huyo(Mzee) aachiliwe huru kwakuwa mhudumu alikosea sana kushika kwa tissue paper passport ya mteja.

Kwa bahati mbaya tuliokuwepo tukisubiri huduma hiyo tulifurahiswa kwa kitendo hicho cha kumnasa vibao hali ilopelekea kutohudumiwa kwa siku ile na kuambiwa twende siku ilofuata.
 
poleni, huajeleza ofisi za uhamiaji za wapi Malaysia au hapa bongo? nampa big up kwa kumfundisha adabu hata kama kakaa mahabusu siku tatu lakini kaitetea nchi yake.
 
poleni, huajeleza ofisi za uhamiaji za wapi Malaysia au hapa bongo? nampa big up kwa kumfundisha adabu hata kama kakaa mahabusu siku tatu lakini kaitetea nchi yake.

Ilitokea Malaysia siyo Tanzania
 
Safi sanaa :first: ila inaonekana hiyo ofisi haina kinga ya wafanyakazi wake mpaka mtu anakunasa kibao duh, mbona nchi nyingine ofisi za uhamiaji kunakuwa na kioo na kijisehemu hata mkono kupita ni shida??
 
Kitendo cha kukataa kuvunjiwa heshima. Hawa watu wakija kwetu Africa tunawatetemekea sana lakini wao they are so racist.
 
Back
Top Bottom