Jakaya Kikwete kuwa mwangalifu na marafiki zako

natofautiana na ww kdg unapomshauri atawale..., ungesema aongoze nchi, there is a big difference between a ruler and a leader

Nadhani alimaanisha kwamba kama ni kuongoza ndicho anachofanya sasa. Kutawala ni kuwaonyesha hawa wanaomdhoofisha kwamba dola ipo na awatie adabu.
 
Napata shaka pia kama uliyoyasema hayafahamu. Huyu haambiliki watu wamesema sana anaenda jukwani kuwaombea kura na kuwasifia atachukua hatua gani unadhani? Pili mwenzake alikuwa anaongea na waandishi wa habari kakatisha maongezi hayo nakudaiwa kaitwa ikulu, unavyodhani kaitwa na nani huko kama sio rais wako unaempamba yuko karibu na familia ya baba wa taifa?

Rafiki yako hawezi kufanya kitu bila kumshauri japo yapo machache anaweza fanya bila kuomba ushauri kwanza, lakini vyovyote iwavyo yuko pamoja nao ungeshauri tumwombe kwa nguvu atupishe nchi hii si yake na marafiki zake na ikulu si mahala pakunywea chai na rafiki zake ambao wewe umesema wanatuhujumu

Wakati mwingine huyo jamaa wa Monduli ni kutaka sifa tu. Rais hawezi kupanga mpango wa mauaji dhidi ya mtu, kwa lipi hasa? Yeye anakaribia kung'atuka na hakuna yeyote ambaye ni tishio kwake. Kwa nini afanye hivyo? Huko ndo kumharibia tunakolalamikia.
 
Angalia usijempiga ngumi mtu hapo karibu yako. Kwakuwa ndio Rais wetu tusikate tamaa, tuendelee kumshauri achukue hatua madhubuti dhidi ya marafiki zake wanaoshutumiwa kwa UFISADI.

Kamwe hawawezi. Muovu siku zote hushindwa na hawa jamaa wana siku zao zinahesabika.
 
We mwita kweli shmo la choo kila kimba linapokea!hv unazani 2naposema kilam2 anahtaji rafik unazani ni rafk gan?n rafk mwenye kukupeleka kuzuri sio moton,go 2 hell mwita25
 
Nafikiri huo ushauri hata kijana mwenzangu Riz1 uwa anampa sana baba yake na wanafamilia wengine, sema huyu JK ni muoga sana na wote hawa wamejua udhaifu wake ndiyo maana utasikia wanasema wamemjua toka sabini na ngapi sijui au themanini na ngapi

Politics is neither rational nor emotional, huyu jamaa angekuja kwangu nimpe nadharia nzuri za siasa
 
Uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 ulitoa matokeo yaliyokupa weweushindi wa kimbunga wa asilimia 80 na ushee. Waliokupigia kura zilizokuwezesha kuingiaIkulu ni watanzania waliokuamini na kukupa dhamana uwaongoze. Hapa sitakikukubaliana na "marafiki zako" wanaodai kuwa wao ndio waliokuingiza Ikulu. Miminamini kuwa umeingia hapo kwa maamuzi yako wewe binafsi, watanzania, na, barakaza Mwenyezi Mungu. "Marafiki zako" hao wameanza kujisema hadharanikuwa wao ni WAUAJI (rejea thread ya Membe kuwa Muangalifu: Adui yako humjui), na kama hilo halitoshi, wanakuhusisha wewe ktk DHAMBI hiikubwa kuliko dhambi nyingine yeyote. Wanafanya hivi kwa sababu weweunawakaribisha "mahali patakatifu" kunywa nao chai na kuwasikiliza wanayokuambia.Kuna baadhi yao wamesikika wakisema kuwa wao wanatoka ktk kabila yenye damu yakuua. (Kabila hilo halipo katika bara la Afrika lililojaa ustaarabu na heshima kwa maisha ya binadamu wengine), hivyo wao kutoa roho ya mtu sioissue kabisa."Marafiki" hawa wakija kwako wanakuwa watiifu nawanyenyekevu kama masista pale Vatican, lakini wakitoka tu hapo Ikulu, wanarudiktk damu yao ya asili. "Marafiki" hawa wameisha gundua kuwa huna msaada kwaokwani wanazongwa na matatizo lukuki toka kwa wenye nchi, lakini hawapati msaadawako. Wewe unalijua hilo kwani unashindwa kuwasaidia kwa kuhofia reactions yawaliokudhaminisha Ikulu.Kitendo cha wewe kuwasaidia kitakutenganisha nandugu zako wa kweli (hawa ni marafiki zako waadilifu). Ukiwapoteza tu nduguzako hawa, basi ujue kuwa "marafiki zako" wanafiki ndio watakaokuwa wa kwanzakukutenda kwani hutakuwa na pa kwenda. Nimesoma sana vitabu vyote vya dini zetu Tukufu,bado sijaona sehemu inayokuagiza wewe kama Kiongozi wa juu kabisa ktk nchiKUWATETEA watu wachache wanaolihujumu Taifa ambalo wananchi wake wamekuamini nakukupa dhamana ya KUWALINDA. Rudi tena ktk dini yako na ujiulize, je, upo Ikulukwa akili ya kuwatetea marafiki zako wanaohujumu mali za wananchi ambao nimasikini? Jibu utakalolipata LIFANYIE kazi bila kuchelewa. Imani ya watanzaniakwako inapungua kila kukicha, hii ni kwa sababu wanaona mambo yanakwendakinyume na walivyokutegemea. Wananchi hawakutegemea kama ungeendelea kukaakimya huku ukiona wazi kuwa Chama chako kinahujumiwa, familia yako inahujumiwa,marafiki (ndg zako) wanahujumiwa, na nchi unayoiongoza inahujumiwa. Kibayazaidi ni kuwa, wanaofanya hujuma hizo ni marafiki zako ambao badounawakaribisha Ikulu. TAFAKARI, CHUKUA MAAMUZI. Taifa zima lipo nawe, unaogopanini? Hivi unadhani ukimaliza muda wako wa kutawala bila kuwachukulia hatuazinazostahili hawa marafiki zako utaishi kwa amani? Usidanganyike hata chembe,utasakamwa mpaka na majirani zako, utakuwa mpweke, utabaki peke yako. Ulipokuwa unagombea mwaka 2005 wananchi walikufananishana Hayati Julius Kambarage Nyerere, wakajenga imani kubwa kwako kutokana namisimamo yako, umakini wako, na ukaribu wa familia yako na ya Mwl. Nyerere.Wakajua kuwa umebeba siri ya uongozi toka kwa marehemu Mzee Mrisho, na Hayatibaba wa Taifa, Mwl. J. K. Nyerere. Sifa ya wazee hawa sote tunaijua, lakini siohivyo unavyofanya. Unawaumiza watetezi wako wa kweli. Wewe ni MTAWALA,TAFADHALI TAWALA NCHI HII. Waliokupa dhamana hawana pa kwenda kwa sasa,usiwaache jangwani, Mungu atakuuliza, umewaacha wapi na vipi waja wangu?

Tiote
Ujumbe wako umefika na natumaini Mhusika ameupata au hata watu wa karibu yake watamfikishia, ila Sikio la Kufa halisikii Dawa.
Nchi, Taasisi, hata Ukoo haviongozwi na Utashi wa mtu, rafiki, vinaongozwa na Katiba, Sheria, Mwongozo, Maadili ambayo Nchi wamejiwekea kupitia wawakilishi wao either wabunge etc.
Sasa Nchi ikiongozwa na kikundi cha watu wenye malengo ya ubinafsi na ufisadi haya ndio matokeo yake,

Maoni: Bado hajachelewa anaweza kurekebisha kasoro iwapo anavyozidi kuwa kimya ndio matatizo na Imani ya Wananchi inavyopungua, anatakiwa awe na hii kauli " I dont Believe Nothing What I hear and I Believe Half what I see", hawaletee maendeleo na kuondoa kero zote Wananchi kwa Kasi Mpya, Ari Mpya na Nguvu Zaidi

Napenda Kuwakilisha
 
Tiote
Ujumbe wako umefika na natumaini Mhusika ameupata au hata watu wa karibu yake watamfikishia, ila Sikio la Kufa halisikii Dawa.
Nchi, Taasisi, hata Ukoo haviongozwi na Utashi wa mtu, rafiki, vinaongozwa na Katiba, Sheria, Mwongozo, Maadili ambayo Nchi wamejiwekea kupitia wawakilishi wao either wabunge etc.
Sasa Nchi ikiongozwa na kikundi cha watu wenye malengo ya ubinafsi na ufisadi haya ndio matokeo yake,

Maoni: Bado hajachelewa anaweza kurekebisha kasoro iwapo anavyozidi kuwa kimya ndio matatizo na Imani ya Wananchi inavyopungua, anatakiwa awe na hii kauli " I dont Believe Nothing What I hear and I Believe Half what I see", hawaletee maendeleo na kuondoa kero zote Wananchi kwa Kasi Mpya, Ari Mpya na Nguvu Zaidi

Napenda Kuwakilisha

Well said lakini mimi nimejawa na matumaini kwamba this President is nobody's hostage. Kuna wakati watu hawa watajuta kumfahamu, hata kama wanasema hawakukutana barabarani.
 
Uhai wa Ua liloota ndani ya chupa unategemea ni uwepo wa chupa.mpk kufika 2015 tutasikia na kuona mengi.
 
Back
Top Bottom