Jakaya Kikwete kupata tuzo ya Mo Ibrahim?

sina doubt na credibility ya nishani ya Mo, timu inayofanya hiyo kazi ya uteuzi sio ya mchezo ni watu makini, koffi annan, ketumile masire (botswana), salim ahamed salim (tz) na wengine siwafahamu. Vigezo ni pamoja na kuachia madaraka kwa hiari, kuongoza nchi ktk misingi ya kidemokrasia ya kufuata utawala wa sheria. Walio wahi kushinda ni pamoja na mandela, chisano, na mogae
 
JMK anastahiki kupata hiyo tuzo. Ni bahati mbaya hutolewa kwa Marais wastaafu pekee.

JMK anastahiki pia hizo PhD alizotunukiwa, ni mengi aliyoyafanya na anayoyafanya.

Ni kiongozi anaestahili kila sifa ya uongozi, mchapa kazi asiechoka, anakubalika ndani na nje ya nchi.

Mstahamilivu, Mcheshi, Mnyeyekevu, Mjasiri.

Mengi yaliowashinda viongozi wa Tanzania waliopita, kwake kayaweza.

Katatuwa mambo kadha wa kadha kiufanisi mkubwa kabisa.

Leo Tanzania tunaona hata vigogo kama Mramba wakifikishwa mahakamani. Huu ni ujasiri wa hali ya juu. Leo tunaona hata wanaombeza yeye anawafanyia mzaha na kuwaambia "mtarudi". Kudos JMK

Honorary Doctorates are conferred only on those who have achieved the highest national or international prominence in their field. Sasa niambie ni kitu gani ambacho Mh. J.K kafanya kwenye field yake. Uchumi wa nchi unadidimia, mafisadi wanazidi kutafuna nchi, umeme wa mgao kila kuchao n.k.
Ni mazuri yepi ambayo wewe unasema JK kafanya???????? zaidi zaidi ya kuongeza ufisadi na rushwa ndani ya nchi hii.
 
Mbogela unalosema binafsi naona ni ndoto,but inaweza kuwa otherwise only if Shehe Yahya atakutanishwa na Mo Ibrahim mwenyewe mana anaweza mchakachua hadi akajikuta anampa JK iyo tuzo,but otherwise i guess kuna viongozi wengine that deserve the award then JK...

SALAMU ZAKO TOKA ZWOLE..kwi kwi
 
Kuna hadithi inayosema kuwa kulikuwa na mfalme mmoja alishonewa nguo ambazo hazionekani kwa watu ambao dhambi. Wale watu wasiokuwa na dhambi , waliweza kuziona zile nguo. Mfalme aliamini kuwa yeye alikuwa hana dhambi, na hata fundi alipomvalisha zile 'nguo', ili asionekane kuwa hana dhambi, alikiri kweli kuwa zile 'nguo' zilimpendeza, hata kama yeye mwenyewe hakuziona zile nguo, na alijiona yu mtupu.

Mfalme akatoka akakaa katika kiti chake cha enzi akiwa mtupu. Watu pale barazani wakawa wanamsifu kuwa amependeza sana, ingawa kwa kweli alikuwa mtupu. Kila mtu akipita akawa anampongeza mfalme. Alitokea mtoto mdogo ambaye naye alikkuja hapo barazani. Kumuona mfalme, akasema, 'Tazama baba, mfalme yuko uchi'! Baraza zima lilishikwa na aibu na kukawa na kimya. Mzee mmoja akasimama na kusema, 'Kweli mtoto mdogo katuumbua, yeye ndiye tu aliyeweza kuthubutu kuwa mfalme yuko uchi'!
 
Kikwete hakumpeleka Mramba wala wale watuhumiwa wa EPA mahakamani kwa hiari yake. Ukweli ni kuwa baada ya Dr Slaa kuanika ufisadi wa Alex Stewart, EPA, Meremeta, Tangold, n.k.; wahisani waliipa sharti serikali ya Kikwete kuwa wasingetoa hela yao mpaka waone hatua zilizochukuliwa dhidi ya mafisadi. Baada ya hapo Kikwete na serikali yake wakaandaa haraka haraka kesi zisizo na nguvu za kuwatia wahusika hatiani ili waweze kupata fedha.

Hakuna jambo kubwa ambalo Kikwete anaweza kujivunia kufanya zaidi ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, ndiyo maana hata ninyi mnaomwunga mkono mnasema tu, 'mengi amefanya' lakini mnashindwa kuorodhesha hayo aliyoyafanya ili tuyaone kuwa ni mengi na makubwa kiasi gani. Talk quantitavely with data, vinginevyo ni porojo.

Mkubwa hata hicho chuo kikuu cha UDOM hakuna mchango wa maana aliotoa katika ujenzi wake!!!
 
Kuhusu Mramba, kama wananchi wake alipogombania Ubunge wangemkubali hilo sio tatizo la JMK. Jee, aliendelea kuwa waziri baada ya kupelekwa mahakamani?

Katika siasa za Tanzania tumesikia kuna mtu yupo jela na kachaguliwa bila hata ya kuwepo kufanya kampeni. Hilo la Kikwete kumpigia debe Mramba wakati wa kampeni lisikustuwe sana, kwani kama CCM ya huko kwao ilimpitisha kwenye kura za maoni basi ndiye aliekuwa mgombea halali kwa wakati huo.

La tuzo ya Mo, inawezekana ikawa kama ulivyosema, sina ubishi katika hilo.
JK kamwe hawezi pata tuzo ya MO Ibrahim. Sababu za msingi:
1. JK katika serikali yake iliyopita alishindwa kabisa kusimamia utawala bora, kiasi cha nchi kujiendesha bila nahodha. Najua wengi tu wasahaulifu, lakini ni katika utawala wa miaka mitano ya JK tulishuhudia mawaziri wakijifanyia mambo hovyohovyo bila kuwapo wa kukemea (Mfano waziri aliyekuwa anashughulikia maadili ya viongozi kuanza kusutana na wabunge wa chama chake).
2. Katika kipindi cha kwanza cha utawala wake rushwa imekuwa kupita kiasi (imetamalaki) kiasi kwamba watoa rushwa wakubwa wamekuwa wakitoa waziwazi na hakuna wa kuwashika.
3. Katika utawala wake tumeshuhudia demokrasia ikinyongwa kwa kiasi cha kutisha, serikali ilikuwa ndio mwamuzi wa mwisho wa mustakabali wa uongozi wa nchi. Wananchi wamenyang'anywa haki yao mchana kweupe bila woga wala kificho (serikali ya kidikteta).
4. Katika utawala wake umaskini umeongezeka kwa kiasi cha kukatisha tamaa, toka watu 11 milioni hadi 13 milioni.
5. Katika utawala wake elimu kitaifa ilishuka sana toka watu wasiojua kusoma na kuandika 87% mpaka 67%, pia tumeshuhudia ushalishaji wa tabaka la wajinga uliokubuhu, Form IV zero 42%!!!!! Tangu nizaliwe sijawahi kuona takwimu hii.
6. Huduma za afya kuongezeka kwa vifo vya wajawazito na watoto ndio wimbo, huduma nyingine je? Jaza msomaji.
7. Uchumi na fedha: Anguko la uchumi wa nchi toka 2005, mfumuko wa bei kufikia tarakimi mbili, toka 4% aliyoiacha Mkapa, kushuka kwa thamani ya pesa toka Tzs 657 kwa dola mpaka 1600 kwa dola moja ya marekani.
8. Kuvurugika kwa muungano. Wengi hamtanielewa lakini kwa mujibu wa katiba ya JMT na ile ya Zanzibar 2010, muungano haupo!!!!!!
 
Mbogela unalosema binafsi naona ni ndoto,but inaweza kuwa otherwise only if Shehe Yahya atakutanishwa na Mo Ibrahim mwenyewe mana anaweza mchakachua hadi akajikuta anampa JK iyo tuzo,but otherwise i guess kuna viongozi wengine that deserve the award then JK...

SALAMU ZAKO TOKA ZWOLE..kwi kwi

Nyasatu haya mambo hayaendi kwa lobbying, kuna vigezo vya kuzingatia nadhani JK ananafasi kubwa sana akiamua kuinyakua hiyo nishani ni suala la kuifanyia kazi. Nisalimie zwole, doei
 
Hii tuzo imekaa kimtego mno kwa viongozi wa Africa. Nafikiri mo Ibrahim alikuwa mjanja sana kuanzisha tuzo hii akijua fika kuna kipindi cha zaidi ya 10 hatapata mshindi kabisaa
 
Back
Top Bottom