Jakaya Kikwete - Baba wa Katiba Mpya

Kama ninavyokumbuka, wakatiwa kampeni za uchaguzi wa uraisi wa mwaka 2010, ni Dr, Slaa ambaye alitoa ahadi kuwa kama akichaguliwa kuwa raisi, ataanza mchakato wa kuandika katiba mpya ndani ya siku 100. Jambo hili lilipingwa sana na viongozi wa serkali ya ccm. Nilimwona kwa macho yangu, waziri wa sheria wa wakati huo, celina Kombani akipinga jambo hilo. mwingine aliyekuwa anapinga uandikwaji wa katiba mpya alikuwa ni mwanasheria mkuu Werema, kama sikosei. Ni baada tu ya kuona kwamba wananchi, CDM na vyombo vingine vya jamii vimepania kuwepo kwa katiba mpya, ndipo rais Kikwete, akatangaza kuwa pawepo na katiba mpya.

Mimi nashangaa kwa nini watu wengine wanachukulia wananchi kuwa ni mazezeta ambao hawana kumbukumbu wala hawajui ni kitu gani kinachoendelea? Ama ni mbinu ya kupindisha uongo ili uonekane kuwa ni ukweli? Hata hivyo, kwa hali ya kawaida, ukweli unajitokeza siku zote. Ni Dr. Slaa pamoja na CDM ndio waliotoa wazo la katiba mpya na ccm walikuwa wanalipinga.

Kusahau Ruksa. Tukumbushane! 1. CHADEMA yaandaa mkakati mzito kudai Katiba mpya
2. Chadema kuanza mchakato wa Katiba Mpya ndani ya siku 90

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa kitawasha moto wa madai ya kutaka Katiba mpya itakayokidhi matakwa ya wote.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano katika mahojiano maalum, Dk. Slaa alisema mabadiliko ya Katiba wakati huu ni ya lazima na kwamba chama chake kimejipanga kuuelimisha umma kudai mabadiliko hayo.

Dk. Slaa ambaye alikuwa mgombea urais wa CHADEMA na kutoa upinzani mkali kwa mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, na kuambulia ushindi mwembamba, alisema hivi sasa chama chake kinaweka mikakati ya harakati hizo kwa kuwashirikisha wataalam wake wa ndani na nje ya chama.

"CHADEMA ni chama makini, si chama kinachofanya mambo kwa kukurupuka. Tunaandaa mkakati wa mwaka 2011-2015. Ifikapo Januari mwakani, tutapeleka mkakati huo kwenye vikao vya bodi, Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Baraza Kuu baada ya hapo tutaenda kwa wananchi na kuwasha moto nchi nzima kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kudai Katiba mpya," alisema Dk. Slaa.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, CHADEMA inatambua kuwa suala la mabadiliko ya Katiba ni kilio cha Watanzania wengi, hivyo iko tayari kushirikiana na vyama, taasisi na watu binafsi ili kuhakikisha Tanzania inapata Katiba mpya.

Wakati wa mikutano yake ya kampeni, Dk. Slaa katika mambo 15 ya vipaumbele vyake, aliahidi kufanya mabadiliko makubwa ya Katiba ndani ya siku 100 za kwanza endapo chama chake kingeingia madarakani.

Alikuwa akitoa ahadi hiyo kila mahali alipofika kuomba kura za kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Kasi ya CHADEMA kutaka mabadiliko ya Katiba, imechagizwa zaidi na matokeo ya uchaguzi mkuu ambapo mgombea wake, Dk. Slaa anaamini kushindwa kwake kumetokana na mfumo mbovu wa vyombo vinavyosimamia uchaguzi yaani Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), inayodaiwa kukibeba chama tawala.

Kuhusu kumtabua au kutomtambua Rais Kikwete, Dk. Slaa alisema Kamati Kuu ilipokea taarifa ya matokea ya urais; akayajadili na kukubaliana kuwa matokeo yaliyompa ushindi Rais Kikwete yalichakachuliwa kutokana na mfumo mbovu wa Katiba.

Alisema kutokana na sababu hizo, CHADEMA imependekeza kuundwa kwa kamati huru itakayochunguza matokeo hayo na kutoa taarifa itakayolenga kuweka wazi juu ya kila kitu kilichojiri kwa manufaa ya taifa.

"Ushahidi wa matokeo kutoka katika vituo kutofautiana na yale ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi; karatasi za matokea kufutwa ni vielelezo tosha kuwa matokea hayo yalichezewa,"alisema Dk. Slaa.

"Kisheria Tanzania ina Rais na sisi CHADEMA tunasema nchi hii ina Rais, lakini njia iliyotumika kumpata Rais huyo si halali na hilo ndilo lililosababisha wabunge wa CHADEMA kutoka nje siku ya ufunguzi wa Mkutano wa Bunge," alisema Dk. Slaa.

Wakati kasi ya kutaka mabadiliko ya Katiba ikiwa juu, Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani, alitoa kauli iliyoibua mjadala kuwa serikali haiwezi kufanya mabadiliko hayo kwa madai kuwa haina fedha.

Hata hivyo kauli hiyo ilipingwa na wengi wakiwemo baadhi ya majaji na viongozi waandamizi wastaafu. Moja wa majaji hao ni Amir Manento na Jaji Mkuu Augustine Ramadhan; lakini pia Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Waziri Mkuu wake, Frederic Sumaye, viongozi wa dini, wasomi na wanazuoni mbalimbali, wanaharakati, na wengineo wengi wanaunga mkono hoja ya kuandikwa Katiba mpya.
 
Dr Slaa ndie baba wa katiba mpya jk anatimiza ilani ya cdm pia amempoza Dr Slaa baada ya kumuibia kura 2010
 
ni aibu kubwa kwa mtu mzima kuwa muongo slaa alitoa ahadi moja tu kuwa atahakikisha nchi haitawaliki wala hausiki na katiba mpya yeye anachochea vurugu tu keshaisha ndo basi tena.
Mkuu umesahau zile machinga complex 5 tulizoahidiwa na Kikwete hata kiwanja hakipo?
 
Torabora wamekuachia?

Sikuwa Torabora. Nlikuwa kwa Obama. Nlimpelekea rasimu ya katiba. Kaniahidi atakuja Julai kuwabwenga makwenzi wote wanaoleta uchakubimbi kwenye katiba mpya.

Kwa msaada wa watu wa Marekani na vitongoji vyake.
 
Atakumbukwa kwa kufanya urais kuonekana 'cheap'.

Atakumbukwa kwa kutekeleza ilani ya CHADEMA na kupuuza ahadi zake 100 na ushee.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Nashangaa hakuna anaye mzungumzia Mchungaji Mtikila!! Jaribu kufatilia historia yake tangu kuhanzishwa harakati zake - jamaa huyu ni jasiri SANA - tuwe wakweli, mambo mengi aliyo kuwa anapendekeza yameingizwa katika mapendekezo ya katiba mpya.

JK anapaswa kupongezwa kwa kuona mbali na kuamua kuhunda tume yenye Wazalendo wa kweli na wadilifu, kusema kweli ameonyesha ujasiri mkubwa kwa kuwatehua raia ambao walikuwa wanahikosoa Serikali yake bila woga i.e alijua wazi kwamba jamaa hao si wanafiki au watu wanao jipendekeza kwake - kwa akili za kawaida tu mtu mweledi kama yeye alijua wazi kwamba wakiwekwa kwenye tume watachangia kwa kiwango kikubwa bila ya kujali itikadi za vyama vyao au kutaka kuwalinda watu waovu, Bravo JK.
 
Kwa nini uliniacha?

Sikuwa Torabora. Nlikuwa kwa Obama. Nlimpelekea rasimu ya katiba. Kaniahidi atakuja Julai kuwabwenga makwenzi wote wanaoleta uchakubimbi kwenye katiba mpya.

Kwa msaada wa watu wa Marekani na vitongoji vyake.
 
Katika mchakato wa kuandika katba mpya RAIS JAKAYA KIKWETE ameandika historia mpya. kikwete ana sitahili kupongezwa na atakumbukwa daima.

JK Kikwete ni BABA WA TAIFA WA KWELI!
Ni baba wa katiba mpya ya wanchi.
Ni baba wa ujenzi wa mabarabara.
Ni baba wa kuruhusu uhuru hali wa habari.
Ni baba wa ukuzaji mkubwa wa Demokrasia nchini.
Ni baba wa uanzishaji vyuo vikuu vingi nchini.Nk

Note: JK Nyerere ndiye aliyetengeneza katiba ya kidikteta mwaka 1962(The republican constitution), ambayo ilimpa madaraka yote Raisi(yeye). Je kwa uovu huo nyerere anastahili kuitwa baba wa taifa? Jibu: Hastahili hata kidogo, alikuwa dikteta.
 
Why are some Africans looking for a strongman instead of strong institutions?

Is it that they are still looking for their autocratic chiefs subconsciously?

The entire process was collaborative, why exalt one person? In this age?
 
Fuatilieni historia ya Mchungaji Mtikila, miaka ya 1990s alipokuwa akiukosoa uongozi wa Marehemu Julius Nyerere. Huyu ndiye aliyekuwa miongoni mwa Watanzania wasioogopa kusema wazi kuwa utawala wake ulikuwa Autocratic! Na ndiye aliyetoa rai kwa nguvu ya kutaka Katiba Mpya.
 
Back
Top Bottom