Jakaya Kikwete awasha vita ya rushwa!!!

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,342
6,468
"Safari hii rushwa ilitumika vibaya sana kiasi cha kukitia aibu chama chetu. Namna bora ya kurejesha imani hiyo ni kufuta baadhi ya matokeo ya jumuiya, mikoa na wilaya, vinginevyo tutakuwa na wakati mgumu sana" by JK in TanzaniaDaima 31/10/2012. "Rushwa nje nje wazazi CCM" in Mwananchi 31/10/2012.

Kumbe JK ana mitizamo miwili juu ya rushwa. Kwake yeye kuna rushwa inayotumika vibaya au vibaya sana na vizuri au vizuri sana. Hii ambayo inaendelea kutumika kwenye chaguzi za CCM anasema imetumika vibaya sana au kwa fujo mno mpaka kuoneka kwa wazi na wananchi wote na hata nje ya Tanzania. JK anapenda rushwa inayotumika vizuri sana, sasa naomba atupatie mifano hai ya rushwa iliyotumika vizuri sana au bila kuonekana na kuleta manufaa kwa wanachi walio wengi!
 
Yeye alitoa ngapi kwa wanafamilia wake kuingia NEC???? Kamwe hataweza hili, liko nje ya uwezo wake, anaebisha abishe tu
 
"safari hii rushwa ilitumika vibaya sana kiasi cha kukitia aibu chama chetu. Namna bora ya kurejesha imani hiyo ni kufuta baadhi ya matokeo ya jumuiya, mikoa na wilaya, vinginevyo tutakuwa na wakati mgumu sana" by jk in tanzaniadaima 31/10/2012. "rushwa nje nje wazazi ccm" in mwananchi 31/10/2012.

Kumbe jk ana mitizamo miwili juu ya rushwa. Kwake yeye kuna rushwa inayotumika vibaya au vibaya sana na vizuri au vizuri sana.

Jk anapenda rushwa inayotumika vizuri sana, sasa naomba atupatie mifano hai ya rushwa iliyotumika vizuri sana au bila kuonekana na kuleta manufaa kwa wanachi walio wengi!.....

Hivi wenzetu mnalipwa bei gani na Mbowe + Slaa katika kufanikisha haya muyafanyayo??
Yan kila siku hamkosi na la kusema.
 
Kwa sasa rungu pekee walilobakiwa nalo ili kumdhoofisha EL ni hili la kutengua matokeo_Otherwise
EL ndiye atakayepeperusha bendera ya CCM 2015.
 
Akumbuke kuna aliowapa rushwa wakati anataka kuingia NEC na wao leo ndio wagawa rushwa. Hapo dhadha.
 
Rushwa inayotumika vizuri ni ile ya kuhonga ili umshinde mpinzani kama CHADEMA na rushwa inayotumika vibaya ni ile inayotumika ili kumshinda mgombea mwenza ndani ya chama hicho hicho. Sijui nimeeleweka sawa sawa!
 
Haya tuone ule usemi wa ".....asiye wahi kuiba na aokote jiwe amrushie mwizi".
 
Naomba nikujibu swali lako
Rushwa ikitumika vibaya Jk alimaanisha rushwa inayoharibu mtandao wako uliopo, i mean kama ilitumika kuharibu kambi ya JK.

Rushwa kutumika vizuri JK aliamanisha pale inapotete mtandao wako au mtandao uliopo, au pale unapokitetetea chama katika chaguzi kama hizi za udiwani,ubunge na hata Uraisi
 
Hivi wenzetu mnalipwa bei gani na Mbowe + Slaa katika kufanikisha haya muyafanyayo??
Yan kila siku hamkosi na la kusema.

Kaka akili zako na avatar yako vinaendana kupita maelezo.

Kwani haya yamesemwa na Mbowe? Haya basi tunalipwa kama unavyolipwa wewe na Nape.

Hata Kiswahili hujui utajua siasa! Siku nyingine usiseme BEI gani ikiwa huzungumzii manunuzi. Bei ni kwa manunuzi na sio ujira. Ulitakiwa useme MNALIPWA KIASI GANI sio BEI GANI, sawa mwagito?
 
Uchunguzi uanzie kwa Sumaye, uende Nachingwea, pia UWT hapa nasikia mweshimiwa alitumia takribani mabilioni kadhaa. Halafu vijana, nk. Kama haya yataachwa basi nchi imekwisha
 
Mh. Rais kama tulivyozoea kutoa matamshi ya kienyeji enyeji kama vile maneno "bahati mbaya" kusema kweli neno bahati ni tunu bora kwa yule ajaaliwaye kutunukiwa mwenye kutunuku "bahati" si mwingine bali Mwenyezi Mungu pekee, kwa maana hiyo bahati haiwezi kuwa mbaya kamwe.

RUSHWA NI ADUI WA HAKI, SITATOA WALA KUPOKEA RUSHWA. Kwa msemo huu rushwa haiwezi kupata uhalali wa kutolewa, kupokelewa au kutumika. Hakuwezi kuwa na matumizi MAZURI ya RUSHWA katika lolote lile.

"Kumekuwa na matumizi mabaya ya RUSHWA" Je matumizi mazuri ya RUSHWA ni yepi??? Mh. Rais ukiweza kunipa matumizi mazuri ya RUSHWA basi utakuwa uko sahihi hata kwa matumizi mabaya uliyoyaona katika chaguzi za NEC, UVCCM UWT NA WAZAZI, ambao kwa mantiki walikuwa wawe mfano bora wa maadili.

Tulichokiona ni kuwa ALIANZA MTOTO, AKAFUATA MAMA NA SASA BABA. HATA HIVYO FAMILIA NZIMA TUMETENDA KOSA LINALOFANANA YUPI WA KUMKOSOA MWENZIE. JIBU LA WASLI HILI NI KWAMBA WAKUTUKOSOA NI JIRANI

 
Ukweli ni kua Kikwete anajua kua huwezi kupata uongozi ndani ya CCM bila ya rushwa na ndio yeye amedhihirisha kua rushwa safari hii imetumika vibaya sana.Ingawaje yeye mwenyewe ametokana na rushwa
 
Back
Top Bottom