Jakaya ajiandaa kuchukua point tena

Taifa_Kwanza

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
443
86
Mswada wa Sheria ya kupitia/kutengeneza katiba mpya nchini utakaowasilishwa bungeni umeridhiwa
na Rais Kikwete uende jinsi ulivyo sababu anajua utapingwa kila kona, vijijini, mashuleni na vyuoni,
vijiweni, sebureni na vyumbani, bungeni, maofisini, kwenye vyombo vya usafiri, Mahotelini
na kwenye vilinge vya pombe,kwenye TV, Magazetini, hapa hapa Jamii forums etc.

Huku akiwa anajua kwamba utapingwa vilivyo ndani na nje ya nchi, pia anajua kwamba mswada
huo utapitishwa (labda ukiwa umefanyiwa marekebisho madogo madogo ya lugha) kwa kishindo
kwa sababu ya wingi wa Wabunge wa CCM.

Yeye Mwenyewe, Jakaya, bingwa wa usanii nadhani kuliko marais wote waliopo sasa duniani, hatasign mswada huo ili uwe sheria aslani, na safari hii amejiandaa kulishangaa hata bunge kwa
kupitisha mswada ambao unapingwa na jamii nzima, atasema na yeye hakubaliani nao.

Yes Kama alivyopinga kulipwa kwa Dowans huku akiwa ndio hasa aliyetoa maelekezo ya kuanza
mchakato wa Malipo atarudia ile ile.subirini muone.
 
Mhmm!Kumbuka kuwa kuna nguvu ya umma ipo nyuma yake inampumulia hivyo usidhani mambo ni rahisi rahisi kama uonavyo,kuna watanzania makini wenye uchungu na nchi yao na wanajua haki zao kw sasa.
 
Asaini au asisaini, Katiba iwe mbovu au isiwe mbovu, but katiba mpya ndiyo itakayoitoa ccm madarakani. Kivipi; Katiba mpya ikiwa nzuri, itaweka vipengele vitakavyoondoa chance ya uchakachuaji, so kuwa rahisi kwa wapinzani kushinda. Ikiwa mbaya au asipokuwepo, itawapa wapinzani mtaji wa kuishitaki serikali kwa wananchi, nao wataichukia zaidi, na hata kama serikali ikichakachua 2015, wananchi wataiondoa kwa nguvu ya umma kwa sababu watakuwa na hasira za kukosa katiba mpya...
 
ngoja tuone itakuaje...!! Nina imani kalata hii ya katiba ikichezwa vizuri itakuwa mtaji nzuri kwa wapinzani kuigeuza CCM jiwe la chumvi lenye rangi ya mkaa.
 
Mswada wa Sheria ya kupitia/kutengeneza katiba mpya nchini utakaowasilishwa bungeni umeridhiwa
na Rais Kikwete uende jinsi ulivyo sababu anajua utapingwa kila kona, vijijini, mashuleni na vyuoni,
vijiweni, sebureni na vyumbani, bungeni, maofisini, kwenye vyombo vya usafiri, Mahotelini
na kwenye vilinge vya pombe,kwenye TV, Magazetini, hapa hapa Jamii forums etc.

Huku akiwa anajua kwamba utapingwa vilivyo ndani na nje ya nchi, pia anajua kwamba mswada
huo utapitishwa (labda ukiwa umefanyiwa marekebisho madogo madogo ya lugha) kwa kishindo
kwa sababu ya wingi wa Wabunge wa CCM.

Yeye Mwenyewe, Jakaya, bingwa wa usanii nadhani kuliko marais wote waliopo sasa duniani, hatasign mswada huo ili uwe sheria aslani, na safari hii amejiandaa kulishangaa hata bunge kwa
kupitisha mswada ambao unapingwa na jamii nzima, atasema na yeye hakubaliani nao.

Yes Kama alivyopinga kulipwa kwa Dowans huku akiwa ndio hasa aliyetoa maelekezo ya kuanza
mchakato wa Malipo atarudia ile ile.subirini muone.

Wow!
...................................................
 
Back
Top Bottom