Jaka Mwambi huyoo kaenda Urusi sasa

Mkuu Pundit,

Hiyo scandal mbona sijawahi kuisikia? Au kuna siku iliwahi kuwekwa hapa JF? Au kama kuna kumbu kumbu mahali kwa nini msiilete hapa tukaichambua?

Mwambi anawezaje kuwa hana elimu ya diplomasia, wakati amekuwa naibu katibu mkuu wa CCM, nafasi ambayo mara ya mwisho ilikuwa imeshikwa na waziri mdogo wa sasa wa nje? Wakuu kwewnye elimu na uwezo wa Mwambi kuwa balozi mnakosa hoja.
 
Read the thread bro, mbona kila kitu kimewekwa wazi in this very thread?
 
Mkuu wangu Pundit, nafikiri nimesema ya kutosha, kama kawaida yangu huwa ninafika mahali ninawaachia wananchi waamue ukweli, uongo, unafiki, chuki za binafsi, na uzandiki ulipo.

Ahsante Mkuu tukutane tena kweny ishus zingine.
 
..anapelekwa Ubalozini Baada Ya Kupibwa Chini Unaibu Katibu Mkuu Wa Chama ..baada Ya Kuhusika Na Kashfa Ya Ufujaji Pesa Makao Makuu ...pesa Za Uchaguzi Mkuu Ccm..na Pia Pesa Za Kununua Wapinzani..ambapo Kina Akwilombe Walikuwa Wakisainishwa Milioni 2..halafu Anaongezea Sifuri Anasema Amewanunua Milioni 20...mchezo Wake Yeye Na Komba.....pamoja Na Kuwa Ni Kosa Lazima Wamkumbuke ...kwa Kuwa Wote Yeye Na Mwenyekiti Wake Na Sekretariati Lengo Lao Lilikuwa Wizi..yeye Kaiba Pesa..na Chama Kinarubuni Wapinzani!!!..ngoma Droo...mpeni Ubalozi...

Sasa Tunasubiri Kazi Jk Aliyomuahidi Aggrey Mwamry....

Mkuu PM,
Unaipenda nchi yako kweli?

Nadhani jibu ni ndiyo.

Kama unayotaarifa ya uhalifu kama huo ulioutoa kwanini usiupatie Jeshi la Polisi wahusika wakachukuliwa hatua za kisheria?
 
hivi mbowe anazo qualification za kuwa rais wetu?
maana ana diploma tu na hana experience ya uongozi

Mtu wa Pwani,
Nadhani umemaliza malumbano kwa njia ya T.K.O.

Kinachoendelea ni sasa ni hoja za ziada lakini si muhimu tena kuendelea kujadili.

Ahsante kwa kuhitimisha mjadala.
 
Nimekuwa ninafuatilia postings za Kubwajinga katika threads mbili sasa hii na ile ya Wanajeshi wetu kupelekwa Comoro.

Kimsingi inaonesha kuwa Kubwajinga unakuwa ni mzito wa kuelewa (hata pale unapoelewesha) au hufahamu ni situation gani iliyopo sasa hivi inayompa madaraka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuteua wasaidizi wake mbalimbali.

Kwanza kabisa ni vyema ukaelewa kuwa kazi ya uwakilishi kama ya ubalozi inahitaji mtu mwenye uwezo wa kuongoza, si kila mtaalam ni ana uwezo wa kuongoza. Sifa za uongozi Jaka Mwambi anazo.

Pili, Majukumu ya Ofisi za kibalozi huweza kutofautiana toka nchi moja hadi nyingine kutokana na sababu mbalimbali kama za kiuchumi, kisiasa, kihistoria, kiusalama nk. Kwahiyo Rais huweza kuamteua mtu yeyote mwenye uwezo kuongoza / kuiwakilisha Tanzania. Uwezo huo Rais amepewa kikatiba na ni halali.

Tatu, Ofisi za kibalozi huwa na technical staff ambao ndiyo msingi wa kazi za kila siku za ubalozini. Hawa technical staff ndiyo wataalam unaowasema wewe.

Mwisho kabisa, nikisoma postings zako between the lines zinaonesha udhaifu mkubwa sana, kwani unamwongelea JK kama JK, na siyo JK kama Rais. Ninasema hivi kwa sababu huonyeshi ni wapi Rais amekiuka taratibu za ki-madaraka na ki-mamlaka katika kufanya uteuzi wa Jaka Mwambi.
Inawezekana unamchukia JK kwa sababu ambazo unazifahamu wewe mwenyewe kwahiyo unatumia muda na fursa iliyopo hapa JF kuandika na kutoa 'nyongo', any way kama ni therapy kwako basi mwandikie barua then ipeleke Ikulu.
 
Mkuu Punda,
Nashukuru kuwa umevutiwa na postings zangu ingawa unatengeneza makunyansi contents zake. Hii inaonyesha ubora wake hata kwa wliopotoka, otherwise usingetumia muda wako kusoma na hata ku-comment. Shukhran.

Kuelewa kuna aina nyingi. Mbili za kidemokrasia ni 'your way' or 'my way' lakini sio 'the highway'. Yule anayekuwa upande wa majority ndio anayetambulika kuwa mshindi, upande ambao always nimeangukia. Kwa hiyo, conclusion yako ya kusema KJ haeleweshweki, meanining sifuati unachotaka wewe, haina uzito. Let's have constructive discussion sio kukaa bweteka tu na kuwapigia makofi walioko madarakani kwa vile tu labda tunanufaika na huo uzembe wao. Jenga hoja, kama iko sawa hata mimi nitaku-support.

Mkuu, tupatie hizo sifa za Jaka za kumzidi Chokala, maana mara ya mwisho nakumbuka uongozi chamani alionekana hafai.

Hii inakubalika kuwa ofisi za kibalozi zinatofautiana. Ndio maana tunahitaji wasifu wa Jaka wa sasa unaomfanya afae kutuwakilisaha Russia. Tulio nao sisi ni ule wa yeye kushindwa kazi Tanga, Iringa, CCM HQ n.k.

Kama wataalamu wapo yeye anafuata nini kuongeza gharama na carbon footprint?

Unfotunately humu mtandaoni, JK ni JK kama binadamu raisi wa nchi na sio mungu kama kama ilivyo kwako. Hapa tunaongea vile roho inapenda.

Simchukii JK kwani ni dhambi nami ni muumini wa dhati, lakini ninachukia sana sana sanaaaa yale yeye, wanamtandao na wapiga debe wao wanayoitendea nchi yangu. Sijui wewe mwenzetu unayafurahia? Hebu tufahamishe.
 
Kwa kawaida Mwalimu hufundisha na baadae hutoa jaribio kuangalia wanafunzi wameelewa kwa kiasi gani, lakini bado kuna wengine hupata ZERO.

Kwaheri!!!!
 
Sio kila anayejiita daktari ni daktari, wako akina Dr. Remmy Ongala, Dr.Emmanuel Nchimbi nk. wote ni bogus tu, kwa hiyo ukijiita mwalimu, huwi mwalimu mpaka uhitimu na uwe na cha kufundisha. Mpaka hivi sasa sijakiona zaidi kukataa kujibu hoja. Nakumbushia baadhi hapa:

  1. Sifa za Jaka ni zipi zilizofanya Chokala asifae?
  2. Kama kuna wataalamu kuliko Jaka, anafuata nini Moscow?
Kwako mwalimu.
 
1. Chokala, amemaliza muda wake ndio maana Mwambi anaenda kumbadili hivi hili nalo linahitaji debate?

2. Nafasi ya mwisho ya Mwambi, nationally, ilikuwa ni kama ya Mh. Zitto, kule Chadema, yaaani naibu katibu mkuu wa chama tawala, nafasi ambayo mara ya mwisho ilishikwa na waziri mdogo wa nje Ndugu Idd

3. Mkuu labda utuweke sawa, kwa maoni yako bongo kiongozi wa taifa anayefaa kwa standards zako ni yupi?
 
FMES,
1. Sifa za Jaka ni zipi zilizompeleka maana yeye sio dipolomat?
2. Kama kuna wataalamu kuliko Jaka huko Moscow, yeye anafuata nini?
 
1. Mkuu sasa unashusha hadhi yako na haya maswali, unasema Mabalozi wote tuliowahi kuwa nao toka tupate uhuru walikuwa na sifa za u-diplomat? Mayunga na Liundi walikuwa na hizo sifa?

2. Sasa Tanzania hatuna wataalamu wa siasa kuliko rais wetu, sasa tunahitaji rais wa nini, si tunge ondoa rais, wataalamu watuongoze, duh! Vipi mkuu kuna mtu kaiba code yako nini?
 
FMES naomba ujibu swali nililouliza,

1. Sifa za Jaka ni zipi zilizompeleka maana yeye sio mwanadipolomasia?
2. Kama kuna wataalamu kuliko Jaka Mwambi huko Moscow, yeye anafuata nini?
 
1. Mwambi anaenda kuwa balozi kwa kuteuliwa na rais.

2. Wataalamu huko wanahitaji kiongozi, Bush sio mtaaalamu kuliko wa-Amerika wote, wataalamu wanahitaji kiongozi.

Mwambi anazo sifa zote za kuwa balozi, baada ya kuongoza ngazi mbali mbali za taifa, mpaka ya mwisho ya muhimu sana ya unaibu-katibu wa CCM taifa.
 
Mkuu FMES,
KJ nadhani hana hoja, sababu zote za uteuzi wa Mwambi zipo wazi na sababu za kurudi Balozi Chokala pia ziko wazi, kwahiyo kama nilivyoandika hapo nyuma, ukisoma kwa makini sana postings zake bila hata ya kutaka kumjua kwa sura KJ, unapata ufahamu wa fikra zake nazo ni chuki binafsi dhidi ya JK kama JK tu. Sihitaji PHD kufahamu fikra za KJ maelezo yake pekee yanatosha kwani yanajieleza vizuri.

Lakini jambo la pili, KJ hajui kwamba kila Wizara, idara za serikali, Ofisi za binafsi na hata majumbani mwetu, ni lazima kuwe na watu ambao wana-manage hizo Ofisi. Na ili uweze ku-manage ni lazima uwe na uwezo wa kuratibu (co-ordination) strategies na pia kufanya maamuzi (decision making) kwa kutumia available resources including technical staff. Kuwa na uwezo wa kusimamia utekelezaji wa maamuzi mbalimbali.
Sasa vitu kama hivyo siyo rahisi ukasema vitafanywa na wataalam bila ya kuwa na mipangilio. Mipangilio ambayo ipo inatumika sasa hivi duniani ilikwishatafitiwa na kuonekana kuwa inafanya kazi. Sasa kama KJ anataka kuja na style yake ni bora akatuambia si vibaya.

Hoja ya kwamba wataalam wapo na asipelekwe Mwambi ni hoja dhaifu mno, ni sawasawa na kusema Sir Alex Furguson au Arsene Wenger sio muhimu na hawahitajiki katika timu zao kwani wachezaji wenye vipaji wapo (Ninajaribu kutoa mifano rahisi kabisa ili KJ aelewe)

Hongera kwa kufikisha Mitundiko 4000, si haba!
 
Hoja ya kwamba wataalam wapo na asipelekwe Mwambi ni hoja dhaifu mno, ni sawasawa na kusema Sir Alex Furguson au Arsene Wenger sio muhimu na hawahitajiki katika timu zao kwani wachezaji wenye vipaji wapo (Ninajaribu kutoa mifano rahisi kabisa ili KJ aelewe)

Na hapo akishindwa kuelewa, basi ataelewa 2010
 
FMES,

..Seifu Iddi alikuwa Foreign Service Officer his whole career. Alipanda ngazi mpaka kuwa Balozi wetu China. Baada ya hapo akateuliwa Naibu Katibu Mkuu CCM, na sasa ndiyo amerudi Mambo ya Nje kama Naibu Waziri.

..Najua hayo yote unayafahamu, sasa sijui kwanini unajaribu kumlinganisha Balozi.Seif Iddi na Capt.Jaka Mwambi.

..Raisi ana mamlaka ya kuchagua Mtanzania yeyote yule kuwa Balozi. Sasa hiyo haihalalishi Raisi ateue hata Watanzania wenye MINIMUM QUALIFICATIONS kutumikia ktk nafasi hizo.

..Tanzania ni nchi masikini. Tunapaswa kutumia RASILIMALI zetu, ikiwa ni pamoja na WATAALAMU, kwa umakini mkubwa. Tunapaswa kufanya maamuzi yetu kwa umakini mkubwa kuliko mataifa tajiri na yaliyoendelea.

..Nilitarajia Raisi ambaye ame-serve miaka 10 kama Waziri wa Mambo ya Nje, angeteua Mabalozi from the cream-of-the cream ya Wataalamu wetu wa Diplomasia na Mashirikiano ya Kimataifa. Huu uteuzi wa Capt.Jaka Mwambi unatia mashaka kwa kila anayefuatilia utendaji na ufanisi wa Balozi zetu.

..Wataalamu tunao, kwanini hatuwapi nafasi kutumikia? Kwanini Balozi zetu ziendelee kuwa vichaka vya kuficha vigogo walioshindwa ktk majukumu yao ya awali? Adadi Rajabu alishindwa kama Dir' wa CID, Lt.Gen.Mayunga alituhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za CCM Kilimanjaro, na wengine wengi sina haja ya kuwataja hapa.
 
Maoni na maswali mazito haya lakini kwa kifupi ni kwamba Jaka umekosa hapa nakupeleka kule .Kwamba mshikaji mie ndiye Rais nakatiba inaniruhusu wewe chukua huu ukubwa mengine baadaye .That is my prezidar JK .

Makamba Katibu Mkuu CCM then Mbunge why all that ?
 
Seifu Iddi alikuwa Foreign Service Officer his whole career. Alipanda ngazi mpaka kuwa Balozi wetu China. Baada ya hapo akateuliwa Naibu Katibu Mkuu CCM, na sasa ndiyo amerudi Mambo ya Nje kama Naibu Waziri.

Mkuu Joka,

Balozi Idd, kwanza likuwa balozi Uholanzi kabla ya kwenda u-China, hakuteuliwa isipokuwa alichaguliwa kwenye uchaguzi mkuu wa CCM.

..Najua hayo yote unayafahamu, sasa sijui kwanini unajaribu kumlinganisha Balozi.Seif Iddi na Capt.Jaka Mwambi.[/B
]

Seif Idd, alikuwa balozi, Mwambi alikuwa Capatin wa JWTZ, lakini wote waliishia kuweza kuifanya kazi ya unaibu katibu mkuu wa CCM taifa, kazi ambayo kwangu ni kubwa sana kuliko ubalozi wa Urusi, sasa nashangaa mtu kama wewe kutoelewa hilo mkuu, kwamba akiwa CCm taifa alikuwa ni mmoja wa watengeneza sera zetu za taifa, kwa hiyo kama ni qualifications zingeulizwa huku, lakini sio sasa wakati tayari amesha-function kwenye CCM taifa, kwa kweli ni weak argument, hasa ukielewa kuwa kina Liundi walienda kuwa mabalozi kwa kukimbiza mwenge tu, under Mwalimu.

Mwambi, from Captain wa JWTZ, mpaka kuwa naibu katibu wa CCM taifa, unasema hawezi kuwa balozi wetu Urusi I am lost?

..Raisi ana mamlaka ya kuchagua Mtanzania yeyote yule kuwa Balozi. Sasa hiyo haihalalishi Raisi ateue hata Watanzania wenye MINIMUM QUALIFICATIONS kutumikia ktk nafasi hizo.

Exactly what do you mean? Haya ni mapungufu ya katiba sio ya rais mkuu mbona tunachanganya mambo? Maraisi wetu toka uhuru wamewachagua viongozi wangapi wasiokuwa na uwezo, nani aliwauliza? Kwa sheria ipi? Rais ana mamlaka ya kumchagua anybody you said it sasa tena unamlaumu nini rais ambaye hajavunja sheria?

Wakuu labda kuna something I am missing hapa!
 
Back
Top Bottom