Jaka Mwambi huyoo kaenda Urusi sasa

Kasheshe,

It is interesting unamleta Paul Bomani.Paul Bomani in this case anaweza kulinganishwa na Jaka Mwambi. Kwa vipi?

Paul Bomani alitunukiwa mikazi kibao, chancellor UDSM, Chairman TBL etc etc, matokeo yake ndiyo hayo unayoyataja. My complain ni kwamba tusimpe mtu mmoja responsibilities kibao, hususan responsibilities ambazo zinakingana.Kama tunataka kumpa ubunge member wa NEC fine, vikao vinaweza kuingiliana, lakini member wa NEC huyo huyo, au mbunge huyo huyo awe balozi? Absurd.

Kusema kwamba experience siyo basis pekee hakumaanishi kuwa experience itupwe.certainly nitakuwa dissapointed kama rais ata appoint career diplomats wenye experience ya miaka mingi lakini hawana results.Tatizo ni kwamba Jaka Mwambi hana experience wala results na zaidi ya hapo ananuka rushwa kama ilivyoelezwa hapo juu.

Ukisoma vizuri utaona sina matatizo hata kama watam fast track mtu aliyesomea "conflict resolution" au "international diplomacy" na anayeweza kutuwakilisha vizuri.Lakini kama kuna watu wenye experience na results it is even better.

Tatizo ni kuwa hakuna mtu anayeweza kubisha kuwa Jaka Mwambi kama alivyoiabisha CCM kwa ufisadi wake hawezi kuzua "Mahalugate" nyingine huko Kremlin.Kwa hiyo this is more than just an issue of experience vs change kama unavyotaka kuliframe wewe.
 
katika mapana yake kazi za ubalozi ni macho, masikio na mdomo wa serikali katika nchi uliopo. hii ni katika nyanja za siasa, uchumi, utamaduni n.k. sasa katika wajibu huu utaona kazi ya balozi ni nini yaani yeye ndo hasa kinara wa majukumu hayo. sasa kama balozi ni zero basi wajibu wake hawezi utenda kwa makini.

katika balozi za nchi kwa nchi (bilateral stations) hutokea balozi kuitwa na serikali husika na kutakiwa kutoa msimamo wa suala la dharura lillilotokea. aidha balozi makini ni yule atakayekuwa na uwezo wa kutafsiri mwelekeo wa siasa, uchumi nk katika mahusiano ya nchi.

katika balozi zinatuwakilisha katika mashirika ya kimataifa (multilateral stations) mara nyingi balozi uhusika katika majadiliano (negotiations) ya masuala yanayoendelea duniani. hapa hata kama balozi anawasaidizi vichwa nadhani ni muhimu na yeye awe kichwa kwani hao wasaidizi watampa brief lakini akikaa kwenye kile kiti na ubao mbele yake umeandikwa tanzania basi balozi ndo mpambanaji na kila atakalozungumza wenzake watasikiliza kwa makini na kusoma between lines. balozi akiwa hovyo nchi itapwaya na hata kwenye vile vikao vya pembeni au vya marafiki wa mwenyekiti haitajumuishwa.

hata hivyo lazima nikiri kwamba pamoja na ukweli kwamba shule ni muhimu katika wadhifa wa ubalozi lakini naamini ubalozi ni zaidi ya shule yaani darasa. umakini, uadilifu na uzalendo ni masuala muhimu.

sasa kama mkuu wetu mpya urusi anafaa au la hilo si la mimi kuamua.

kuhusu mheshimiwa aliyekuwa italia nadhani naye si suala la qualification bali zawadi. yeye alikuwa wizara ya elimu ya juu na aliyekuwa mkuu wa nchi na naamini mchango wake katika timu ya ushindi ndio akaishia na ubalozi mengine ni historia.
 
CCM wamepeleka kada wa Chama chao Russia .Tanzania ina vyama vingi sasa .Je kada huyu anaweza kuwahudumia Watanzania kama watanzania bila kuweka u CCM wake mbele kama boss wake alivyo na tabia hizo ? Maana watu mliyoko nje naami wengi si wana CCM na mnaenda kukutana na Balozi amaanza kuongelea CCM na si Nchi kwa ujumla wake , kikao hicho kitakalika ?
 
hivi mbowe anazo qualification za kuwa rais wetu?
maana ana diploma tu na hana experience ya uongozi
 
Kwa mtazamo wangu nafikiri umefika wakati wa kupiga kelele juu ya marekebisho ya Katiba ambayo kwa sasa Rais ni kama Mungu wa TZ,kwamba anayo mamlaka ya kufanya lolote bila ya kuhusisha idara yoyote.

Kwa uelewa wangu Balozi yoyote angekua bora zaidi kama angekua na taaluma ktk nyanja za kimataifa.Sasa unapotupelekea mtu yoyote from no ...........,hapa rais hajatutendea haki sisi wenye nchi.Na nalisema hilo kwa kuamini kwamba wataalamu wa nyanja za kimataifa hapa TZ ni wengi sana na wangefaa kwa nafasi hiyo JM.
Kama katiba ingekua safi JK alitakiwa kuufahamisha umma vigezo alivyotumia juu ya uteuzi huo wa danganya toto.

JK 2010 usichukue form za Urais kwa sababu hutufai,sisi sio kwamba hatuna macho.Illitrate people may vote for you but ...............
 
Wewe Pundit na Kubwajinga,

Si majuzi tu kule kwenye thread moja mmesema kuwa elimu ya mwenyekiti wa Chadema, sio tatizo kwa uongozi wa taifa, sasa leo mnasema tena elimu ya Mwambi ni tatizo kuwa balozi wetu Urusi, that is wasup?

I mean talking about double standard, can it get lower than this? Mnasema qualification, all Liundi had to do ni kufukuza mwenge na Mwalimu, the greatest ever kumpa ubalozi Paris, Gen. Mayunga, all he had to do ni kupigana vita Uganda kuwa balozi Nigeria, sasa hizo international Relations Skills walizipata saa ngapi? Je kati yenu kuna mwenye rekodi ya perfomance ya hawa ndugu juu?

Anagalau mjumbe anayesema kubadili katiba, heshima mbele mkuu strong point.
 
Mkuu Chingwanji,

Naona umechanganya mambo mkuu, serikali yetu ni ya chama tawala yaaani CCM, sasa balozi aliyechaguliwa na mwenyekiti wa CCM kuiwakilisha serikali ya CCM, sioni inakuwaje awe tatizo kwa wananchi ambao ndio hasa in the first place walioichagua na kuipa madaraka hayo CCM, ambayo iliishia kuiweka serikali yake ili kutekeleza sera za CCM, zilizoahidiwa na kukubaliwa na wananchi hao wakati wa uchaguzi, sasa balozi wa serikali ya CCM atautoa wapi ubavu wa kutomsaidia mwananchi wa Tanzania, aliyeichagua CCM kututawala for the next three more years?
 
Kusema elimu siyo tatizo maana yake siyo kwamba kila tunayemteua asiwe na elimu, na wenye elimu tuwaache.

Kusema elimu si tatizo maana yake elimu isichukuliwe kama ndiyo kigezo cha pekee, kuna vigezo vingine kama track record na performance.Sasa huyu Jaka Mwambi ukimuweka kwenye kila department hayumo, elimu ya diplomasia hana, track record ya performance hana, zaidi ya hapo ananuka rushwa vibaya sana.Sasa unataka kumbeba vipi huyu?

Ukiongelea double standards basi unazo wewe unayemsakama Lowassa lakini uchafu wa Jaka Mwambi katika kuiba hela za rushwa (doubly terrible) huuoni.Nani ana double standards hapo?
 
Mkuu habari za rushwa na Mwambi, ndio kwanza nazisikia hapa JF, siujui ukweli wake na simkatalii alyezisema, isipokuwa zingesemwa mapema kabla hajapewa ubalozi, halafu hizi standard za ufisadi zimeshuhswa mno hapa JF kiasi kwamba sasa sio rahisi kuamini nani ni nani,

Halafu mkuu ufikie mahlai uache ushabiki wa yanga na simba, elimu ni elimu, kama kiongozi either unayo au huna, tulijuwa tu yatakuja kuwashinda ndio maana hata ile topic hatukuigusa kabisaa, sasa unajaribu kusingizia Lowassa, wakati kila m-Tanzania anajua kuwa amepatikana kutokana na ripoti ya kamati ya Mwakyembe, hatujasikia ripoti ya CCM kuwa Mwambi ni fisadi kama Lowassa,

Then again, unajaribu na ku-fail miserably ku-balance kati ya elimu na perfomance, as if sisi wote hapa tumelala, man look here it is about time sasa huko upande wa pili muamue, either tuiongoze nchi yetu tukiwa na elimu, au tuondoe kigezo cha elimu period, lakini msilete hizi nyepesi nyepesi!
 
hivi mbowe anazo qualification za kuwa rais wetu? maana ana diploma tu na hana experience ya uongozi

Huu ni ugonjwa wa kutofikiri, Elimu ya John Major ilikuwa chini sana lakini aliweza kuwa waziri mkuu wa uingereza 1990 hadi 1997, Prof Alberto Ken'ya Fujimori aliweza kuiongoza Peru July 28, 1990 hadi November 17, 2000.kwa shida sana, nafikiri kwa mifano hii 2 tu, utajua huhitaji elimu ya juu sana kuwa kuwa kiongozi wa nchi....Mbowe anastahili kuwa kiongozi wako na watanzania kwa jumla......big up Mbowe
 
Kwa mtazamo wangu nafikiri umefika wakati wa kupiga kelele juu ya marekebisho ya Katiba ambayo kwa sasa Rais ni kama Mungu wa TZ,kwamba anayo mamlaka ya kufanya lolote bila ya kuhusisha idara yoyote.

Kwa uelewa wangu Balozi yoyote angekua bora zaidi kama angekua na taaluma ktk nyanja za kimataifa.Sasa unapotupelekea mtu yoyote from no ...........,hapa rais hajatutendea haki sisi wenye nchi.Na nalisema hilo kwa kuamini kwamba wataalamu wa nyanja za kimataifa hapa TZ ni wengi sana na wangefaa kwa nafasi hiyo JM.
Kama katiba ingekua safi JK alitakiwa kuufahamisha umma vigezo alivyotumia juu ya uteuzi huo wa danganya toto.

JK 2010 usichukue form za Urais kwa sababu hutufai,sisi sio kwamba hatuna macho.Illitrate people may vote for you but ...............

Mkuu,

Nakubaliana na yote uliyosema hasa hiyo sentensi nilioikuza.
 
Sasa hizi ndio tunaita kelele za mlango, kila m-Tanzania ana haki ya kuchukua fomu ya kugombea urais, ni wananchi ndio wataamua, sasa kwa nyinyi mnachotaka ni kumnyima haki yake kikatiba rais wetu wa jamhuri wa sasa kuwa eti asichukue fomu,

Halafu mnatukosea hata adabu na heshima wananchi 80% ya wapiga kura tuliomchagua kuwa rais wetu, kwamba ati sisi ni illitrate, wakuu jaribuni kuwa na heshima na viongozi wetu wakuu wa taifa na wananchi kwa ujumla, mnachoweza kufanya sio kuwatukana wananchi na viongozi wetu, bali tu kukosoa penye mapungufu, na kuwapigia kura wanaofaaa when the time comes, ingwa kwenye hilo bado mnaonekana kuwa nyuma sana, maana tungewasikia majuzi Kiteto.
 
Mkuu Chingwanji,

Naona umechanganya mambo mkuu, serikali yetu ni ya chama tawala yaaani CCM, sasa balozi aliyechaguliwa na mwenyekiti wa CCM kuiwakilisha serikali ya CCM, sioni inakuwaje awe tatizo kwa wananchi ambao ndio hasa in the first place walioichagua na kuipa madaraka hayo CCM, ambayo iliishia kuiweka serikali yake ili kutekeleza sera za CCM, zilizoahidiwa na kukubaliwa na wananchi hao wakati wa uchaguzi, sasa balozi wa serikali ya CCM atautoa wapi ubavu wa kutomsaidia mwananchi wa Tanzania, aliyeichagua CCM kututawala for the next three more years?

Haya ndio yale yale ninayoyaita propaganda za wapiga debe wa wanamtandao. Ndio maana ndani yake hakuna hoja yoyote. Mtu anaposema eti kwa vile tu balozi ni mwana CCM kwa hiyo atamsaidia mwananchi ni ubumbuwazi wa hali ya juu. Kwani mafisadi wote walioorodheshwa hivi sasa si ni wana CCM including aliyekuwa balozi wetu US, Mh. Daraja?
 
Sasa hizi ndio tunaita kelele za mlango, kila m-Tanzania ana haki ya kuchukua fomu ya kugombea urais, ni wananchi ndio wataamua, sasa kwa nyinyi mnachotaka ni kumnyima haki yake kikatiba rais wetu wa jamhuri wa sasa kuwa eti asichukue fomu,

Halafu mnatukosea hata adabu na heshima wananchi 80% ya wapiga kura tuliomchagua kuwa rais wetu, kwamba ati sisi ni illitrate, wakuu jaribuni kuwa na heshima na viongozi wetu wakuu wa taifa na wananchi kwa ujumla, mnachoweza kufanya sio kuwatukana wananchi na viongozi wetu, bali tu kukosoa penye mapungufu, na kuwapigia kura wanaofaaa when the time comes, ingwa kwenye hilo bado mnaonekana kuwa nyuma sana, maana tungewasikia majuzi Kiteto.

FMES,
Hoja yako inaweza kuwafurahisha wanamtandao lakini si kwa wana CCM wngineo walikwishawachoka wanamtandao, including JK. Kwa taarifa yako, 80% ilikuwa ni kwa 2005, hivi sasa kama sijakosea kura za maoni za REDET zinaonyesha 40%.
 
Tayari huna hoja mkuu, sasa kubali yaishe, kama elimu sio tatizo kwa chadema, basi isiwe tatizo kwa ccm hiyo ndiyo hoja ya msingi hapa bro, the rest ya maneno yako ni pure nonesense,

Ubumbuwazi ni kushindwa kuelewa na kukubali ukweli, tena kwa mtu aliyeenda shule kama wewwe, maana mpaka sasa hutaki kukubali kuwa mtandao waligombea na kushinda, na kwmba mpaka sasa ndio wanaotawala hakuna kilichobadilika, balozi wa Tanzania ni muwakilishi wa taifa zima na hatujawahi kusikia akiwasaidia CCM peke yao, zoezi la kubalisha passport limefanyiwa wananchi wote bila kujali vyama vyao vya siasa kwa hiyo msianzishe uzushi hapa,

hizo polls tumezisikia sana hapa toka tukiwa BCS, mpaka leo JF, kuna wakati tukaamini kuwa chadema itashinda urais kutokana na hizo polls za hapa JF, tukaambiwa polls zinaonyesha ushindi wa chadema Kiteto, anyways mkuu you can keep them yaani hizo polls zako against mtandao, zinazokuambia kuwa muungwana alishawachoka mtandao, kalagha baho!
 
Sasa hizi ndio tunaita kelele za mlango, kila m-Tanzania ana haki ya kuchukua fomu ya kugombea urais, ni wananchi ndio wataamua, sasa kwa nyinyi mnachotaka ni kumnyima haki yake kikatiba rais wetu wa jamhuri wa sasa kuwa eti asichukue fomu,

Halafu mnatukosea hata adabu na heshima wananchi 80% ya wapiga kura tuliomchagua kuwa rais wetu, kwamba ati sisi ni illitrate, wakuu jaribuni kuwa na heshima na viongozi wetu wakuu wa taifa na wananchi kwa ujumla, mnachoweza kufanya sio kuwatukana wananchi na viongozi wetu, bali tu kukosoa penye mapungufu, na kuwapigia kura wanaofaaa when the time comes, ingwa kwenye hilo bado mnaonekana kuwa nyuma sana, maana tungewasikia majuzi Kiteto.

Mkuu es swala la 80 % ni bada ya wizi wa kura na mabavu ndiyo leo unalia kila mara na hizo asilimia ambao ndiyo ukweli wa Kiteto na kokote na wewe unajua vyema kwamba CCM huwa hawashindi kwa kura ila mabavu then mnasema wananchi wameamua .Tumezoea haya .
 
This is where I like Watanzania. Every Political appointment has to be justified by amount of expertise and certificates!

It is nonsense period! The state of Tanzania right now it does not matter any more if one has PHD or got a Mpogolo certificate (elimu ya Watu wazima)!

The question becomes again at what interest do these people serve the President and/or Taifa! When we elect a President and surrender as many powers as we have done, we are bind to accept what President's choices are!

We wish that these political and administrational appointments would be based on merits and expertise on specific field, but we fail to realize that this is politics and Rais can appoint anybody on a position that Rais feels he does not have any obligation to appoint an expert to such position!

Hivyo basi, what we need to pray for is that Jaka goes to Russia and do a good job, same way we are wishing Pinda as Prime Minister!

Watanzania due to unsatisfactory perfomance of our government and leaders, we are now equating certificates and subject expert to be the key of our success. Yes we need people who a learned and expert on subject matters, however most important, we need competent and efficient people to execute these responsibilities!

I can see clearly why Jaka is heading to Moscow. To serve the interests of the President! Which includes learning how did Russia government (Communist and KGB) manage to survive the tidalwave to push for transparency, accountability and true democracy. Also how did Putin (Communists and KGB) manage to manhandle all capital reserves of the country and control production while quashing oposition!

Go figure again, why Presidents make appointments!
 
Ukitaka kulinganisha swala la Mbowe na Mwambi kwa utashi wa elimu tu utakosea,rejea hapo juu nime point out kuwa elimu si kigezo pekee, na wala sikuwa namtetea Mbowe.Nilichosema ni kuwa kuna kina Albert Einstein ambao darasani hawakufanya ya maana sana lakini mchango wao kwenye sayansi mpaka leo unajulikana.

Challenge ilikuwa kwa wanaotaka kum discedit Mbowe,ambao hata hivyo hawakutoa vigezo vilivyo unmpeachable, kutuonyesha kimsingi kuwa Mbowe hafai kuwa president.

Hii issue ya Mwambi siyo tu hana uzoefu wala elimu ya diplomasia, cha kutisha zaidi ananuka rushwa.Naweza kuandika kitabu cha 'How to be appointed Tanzanias Ambassador' kwanza climb the party ranks and become influential, create a very embarrassing scandal and next thing you know your buddy the president will get rid of you by apppointing you am assador to some far confines regardless of your abilities.
 
Mkuu Chingwanji,

Heshima mbele mkuu, bungeni si kuna wabunge wa upinzani mkuu sasa waliingiaje huko wakati CCM huwa inaiba kura zote?

Kule Pemba ikawaje CCM ikahsindwa kuiba kura mkuu?
 
Tayari huna hoja mkuu, sasa kubali yaishe, kama elimu sio tatizo kwa chadema, basi isiwe tatizo kwa ccm hiyo ndiyo hoja ya msingi hapa bro, the rest ya maneno yako ni pure nonesense,

Ubumbuwazi ni kushindwa kuelewa na kukubali ukweli, tena kwa mtu aliyeenda shule kama wewwe, maana mpaka sasa hutaki kukubali kuwa mtandao waligombea na kushinda, na kwmba mpaka sasa ndio wanaotawala hakuna kilichobadilika, balozi wa Tanzania ni muwakilishi wa taifa zima na hatujawahi kusikia akiwasaidia CCM peke yao, zoezi la kubalisha passport limefanyiwa wananchi wote bila kujali vyama vyao vya siasa kwa hiyo msianzishe uzushi hapa,

hizo polls tumezisikia sana hapa toka tukiwa BCS, mpaka leo JF, kuna wakati tukaamini kuwa chadema itashinda urais kutokana na hizo polls za hapa JF, tukaambiwa polls zinaonyesha ushindi wa chadema Kiteto, anyways mkuu you can keep them yaani hizo polls zako against mtandao, zinazokuambia kuwa muungwana alishawachoka mtandao, kalagha baho!

Sijui kama elimu sio tatizo kwa CHADEMA, lakini ninachojua hivi sasa ni kuwa kuna tatizo kubwa kwa jinsi wanamtandao (JK et al) wanavyoiburuza nchi yangu. Kibaya zaidi ni pale ninapoona propaganda zao zikiendelea hata kwenye mitandao (internet) badala ya kukazana kutatua matatizo ya nchi.
 
Back
Top Bottom