Jaka Mwambi huyoo kaenda Urusi sasa

1. Lusinde alikuwa balozi China na Kenya, huku akiwa mjumbe wa NEC na alikuwa akihudhuria vikao vyote bila tatizo.

2. Tunao mabalozi wa qualifications, na mabalozi wa zawadi, na wale ambao ni threat kwa waliopo madarakani, kwa kawaida supporting staff ya any ubalozi huwa ni very srong academically, kwamba it does not matter uwezo wa balozi kikazi, ndio maana siwezi kupoteza usingizi wangu na qualifications za mabalozi wetu,

ukweli ni kwamba, it is a none ishu!
 
Mkuu Nziku,

Heshima mbele, ubalozi kwa kawaida ni nafasi maalum kwa ajili ya rais kuwapa waliomsaidia kushinda uchaguzi,

FMES,
Kwenye mengi uliyochangia humu, sijaona lililo la upeo wa chini kama hicho ulichoandika hapo juu. Kwa mantiki yako hiyo, itabidi tuongeze balozi maana bado akina Lowassa n.k. Hebu tufahamishe wapi ilipoandikwa nafasi ya ubalozi kuwa sawa na vipande vya kanga? Wapi inasema kuwa ubalozi ni sehemu ya raisi kufanyia uzembe wake?


the matter of fact sisi bongo ni moja kati ya nchi chache sana duniani ambao angalau tunajali qualifications,

FMES,
Huu uongo unless una proof kuonyesha jinsi tulivyo makini kuliko nchi nyingine..... sijui zipi hizo. Kupigia makofi kila anachofanya JK ndio kunakoiponza TZ hivi sasa. Why dont you just call spade a spade? Tumejaza kuanzia wakuu wa wilaya mpaka mawaziri watu wa kubebwa tu wasiojua kazi, and then tunataka kulaumu umma kwa nini Azimio la Arusha halikufanikiwa.


Kuna nchi kama USA, mwananchi mmoja tajiri alimchangia Bush kwenye kampeni, na kudai anataka ubalozi Italy, mwingine alidai ubalozi wa Kenya, ili atuime muda mwingi kwenda mbugani, na hawa walisema nia zao mbele ya public, na Bush aliposhinda wakawa.

Huu ni uzushi mwingine, (au tuthibitishie). US mabalozi inabidi wapitishwe na seneti, ndio maana wa kwetu wa hivi sasa aliwekewa ngumu na John Kerry hapo awali, sasa hao wa kwako wangepitaje bila kukubalika?.
 
Mimi kwa mtazamo wangu nadhani kuteuliwa kwa Jaka Mwambi ni zawadi ambayo amepewa na kuachwa kwa Chokala ni matokeo ya Kugombea kinyang'anyiro na maswala ya Ukraine pamoja na kwamba kwa kipindi chake alichokaa Moscow pamekuwa nauhusiano mzuri wa Tanzania na Urusi katika nyanja ya elimu.

Patrick chokala amestaafu kwa mujibu wa sheria kwani kafikisha miaka 60 ambayo mabalozi hutakiwa kustaafu. Kwa hiyo si kweli kwamba ameachwa eti kwa sababu ya kugombania urais au matatizo ya Ukrain.
 
1. Lusinde alikuwa balozi China na Kenya, huku akiwa mjumbe wa NEC na alikuwa akihudhuria vikao vyote bila tatizo.

2. Tunao mabalozi wa qualifications, na mabalozi wa zawadi, na wale ambao ni threat kwa waliopo madarakani, kwa kawaida supporting staff ya any ubalozi huwa ni very srong academically, kwamba it does not matter uwezo wa balozi kikazi, ndio maana siwezi kupoteza usingizi wangu na qualifications za mabalozi wetu,

ukweli ni kwamba, it is a none ishu!

Nani ni hao mabalozi wa zawadi? This is a big issue kwa sisi wengine tunaominywa kulipa kodi kwa ajili ya anasa zao huko balozini.
 
uwezo wa balozi ni muhimu hata kama anao maafisa wenye uwezo.
kuna nyakati inabidi balozi ajenge hoja papo kwa hapo sasa
kama balozi ndo zero basi inakuwa shida. dunia ya sasa uwezo
ni muhimu sana si vyema tukijaribu kuukwepa ukweli huo
 
Mkuu Kafara,

Heshima mbele na karibu tena mkuu, angalau wewe una hoja kidogo maana wengine huko juu ni waste of time hata kuwajibu,

1. kabla sijakujibu ipasavyo, kwa uelewa wako naomba ufafanue kazi za kila siku za mabalozi wetu nje zipi? Kwa sababu haya masuala ya ubalozi na mabalozi tulishayasema hapa JF siku nyingi sana na Mkuu wangu Mwawado, kutoka huko akatuweka sawa exactly kuhusu hiii ishu kwamba ni absolutely none-ishu,

2. Wakuu bongo sio majuu, Tanzania hatuna sheria yoyote inayombana rais achague wasaidizi wa aina gani na wenye qualifications za namna gani, wananchi tunamchagua rais na kumuachia aamue nani anamtaka awe msaidizi wake kuanzia mawaziri mpaka mabalozi, tena afadhali siku hizi tunajitahidi kuwa na wenye uwezo, kwenye awamu ya kwanza utlikuwa na viongozi wengi wasioenda shule kabisa kama kina Kisoki.

Mabalozi kuwa au kutokuwa na qualifications ni a none-ishu, kwani Mahalu si ni professor, au?
 
FMES said:
Mabalozi kuwa au kutokuwa na qualifications ni a none-ishu, kwani Mahalu si ni professor, au?


Hawa watu wanaosema kuwa matumizi mabaya ya vyeo na mali ya umma kuwa ni non-ishu, na kutetea kila wakuu bongo wanachofanya hata kama ni utumbo nafikiri ni sehemu ya mafisadi. Mnasemaje waungwana JF?
 
Mkuu hiyo mob justice na umaarufu unaoutafuta hapa kwa kutumia jina langu hutaupata kwamwe, maana members hapa wanajua ninachosimamia, yaani taifa,

Mahalu ni professor, je hakuwa qualified kuwa kuwa balozi? Mkuu labda ulilie kubadilishwa katiba, otherwise rais ataendelea kuwachagua anowataka, regardless ya uwezo wao na wewe utaendelea kujaza post hapa na kunililia,

mkuu ni uamuzi wa rais kumpa mtu anayemtaka madaraka kwa mujibu wa katiba yetu sio katiba yangu FM-ES, get that mkuu!
 
Ubalozi Tanzania una maana tofauti. Kwanza ni kuondoa nuisance, yaani kuwaondoa wanasiasa ambao ni threat kwa watawala nyumbani, au lugha nyingine kuwanyamazisha, nyingine ni kuonesha urafiki kwa wateuliwa kutoka kwa wanaowateua, kwa sisi Tanzania ni symbol of unity kati ya Tanganyika na Zanzibar.
Lakini kimsingi kwa nchi kama Tanzania ubalozi ulikuwa unatakiwa kuplay bigger role kwenye maendeleo ya nchi yetu, na sio kuwa sehemu ya kuwapatia watu zawadi. Jaka Mwambi ni mwanasiasa ambaye alitakiwa kubaki nyumbani, sasa hivi CCM haiko kwenye shape nzuri, wananchama makini na waadilifu kama yeye walitakiwa kubaki nyumbani. Na huko Russia wangemtuma diplomat kutoka forein.
Uteuzi wa Mlawa naona miyeyusho tuu, huyo mzee alitakiwa apumzike. Ukiangalia alikofanya azi kote huwezi kuona kama alikuwa na mafanikio ya kujidai na hata kujisifu!!
 
Mkuu hiyo mob justice na umaarufu unaoutafuta hapa kwa kutumia jina langu hutaupata kwamwe, maana members hapa wanajua ninachosimamia, yaani taifa,

Mahalu ni professor, je hakuwa qualified kuwa kuwa balozi? Mkuu labda ulilie kubadilishwa katiba, otherwise rais ataendelea kuwachagua anowataka, regardless ya uwezo wao na wewe utaendelea kujaza post hapa na kunililia,

mkuu ni uamuzi wa rais kumpa mtu anayemtaka madaraka kwa mujibu wa katiba yetu sio katiba yangu FM-ES, get that mkuu!

FMES,
Sidhani kama unasimamia Taifa maana taifa sio JK na Masha peke yao.
 
kusema kuwa haijalishi kama balozi anazo qualifications or not, ni maneno yaliyokosa shule.
sasa point ni ipi ya kuwa yeye ni balozi? balozi kazi yake moja ni kumuwakilisha rais kwenye nchi ya kigeni. sasa tunataka kuwakilishwa na mtu asiyekuwa na qualifications kwa vle tu wasaidizi wake wana qualifications za kutosha?
huoni kama hii ni kuwakweza wasaidizi wake ambao itabidi wamsaidie mkuu wao wa kazi kwa kila analolitenda?
balozi anatakiwa awe ndo the most qualified person kwenye ubalozi.
 
..anapelekwa Ubalozini Baada Ya Kupibwa Chini Unaibu Katibu Mkuu Wa Chama ..baada Ya Kuhusika Na Kashfa Ya Ufujaji Pesa Makao Makuu ...pesa Za Uchaguzi Mkuu Ccm..na Pia Pesa Za Kununua Wapinzani..ambapo Kina Akwilombe Walikuwa Wakisainishwa Milioni 2..halafu Anaongezea Sifuri Anasema Amewanunua Milioni 20...mchezo Wake Yeye Na Komba.....pamoja Na Kuwa Ni Kosa Lazima Wamkumbuke ...kwa Kuwa Wote Yeye Na Mwenyekiti Wake Na Sekretariati Lengo Lao Lilikuwa Wizi..yeye Kaiba Pesa..na Chama Kinarubuni Wapinzani!!!..ngoma Droo...mpeni Ubalozi...

Sasa Tunasubiri Kazi Jk Aliyomuahidi Aggrey Mwamry....
 
Mkuu ni maneno yako ndio yanyokosa shule kwa kukataa ukweli, tumewahi kuwa na mabalozi wengi ambao ni mzigo, tena kwenye awamu ya kwanza ya Mwalimu, kuna ambao hata kuandika na kusoma, ilikuwa matatizo, tumekuwa na ma-RC wasiokuwa na shule kabisaa, mpaka leo tuna mabalozi walevi tu kazi hakuna, wale wenye overqualificitaions kina Mahalu ndio hawa wametuingiza mkenge,

Jaka Mwambi, hawezi akawa good enough kuwa kiongoiz wa taifa wa CCM lakini eti hawezi kuwa balozi wetu nje, hayo ndio hasa maneno ya kukosa shule, kwa sababu kama uwezo wake ni tatizo, basi tungekuwa na katiba ya kumbana mpaka asiwe kiongozi wa taifa wa CCM, tuwe na sheria moja inayosema qualifications za viongozi wa vyama, na nyingine ya viongozi wetu serikali, wewe huoni kwamba hiyo itakuwa exactly unachosema hapo, yaaani insanity!

Hizi kelele za Mwambi, kutokuwa na qualifications zilitakiwa kuwa raised toka anapewa uongozi wa CCM, I am afriad kuwa saa hizi ni too late, mwacheni akatuwakilishe huko Urusi.
 
FMES,

Wengine siyo wanachama wa CCM and we could care less if CCM elected an illiterate person to be the Secretary General, lakini unpoongelea muwakilishi wa nchi yetu nchi ya watu wengine then it ceases to be a CCM issue, it becomes a Tanzania issue.Thats why we did not raise the issue before and now it becomes an outrage.

Kama mtu hayuko qualified na wengine wapo qualified kwa nini huyu asiye qualified apewe hii kazi? Ubalozi unafanywa kazi ya kisiasa zaidi kuliko kazi ya kidiplomasia, sasa na haya mambo ya diplomasia ya uchumi hawa vingunge wa NEC wataweza kufanya kazi kweli au ndiyo watajisikia entitlement kuwa "hii kazi nimetunukiwa na rais hivyo hamna yeyote atakayeniambia chochote"

1. Lusinde alikuwa balozi China na Kenya, huku akiwa mjumbe wa NEC na alikuwa akihudhuria vikao vyote bila tatizo

This is a very wasteful attitude, kwamba mtu mmoja ndiye awe balozi na mbunge au mjumbe NEC hata kama hiyo itaiingizia nchi hasara ya mamilioni ya pesa ni upuuzi.Kwani hakuna watu wengine wanaoweza kufanya hizi kazi? Au ndiyo mambo ya u demigod na mtu mmoja kuhodhi madaraka lukuki kama vile ni mali yake?
 
Hawa watu wanaosema kuwa matumizi mabaya ya vyeo na mali ya umma kuwa ni non-ishu, na kutetea kila wakuu bongo wanachofanya hata kama ni utumbo nafikiri ni sehemu ya mafisadi. Mnasemaje waungwana JF?

Ufisadi una sura nyingi sana Mkuu kubwajinga, tusije kuwa tunapigia kelele sura moja kila siku huku tuna indulge kwenye sura nyingine.Mimi nilifikiri JF tuna set standards, sasa kama mambo yenyewe tunafikiri hivi napata mashaka sana.
 
Mkuu kwa kawaida huwa ninakuheshimu sana, nashangaa na hii outburst, unasema nini?

1. Ujumbe wa NEC ni kazi ya kumfanya mtu asifanye kazi ya kumpatia kipato? Unasema ujumbe wa NEC ni a full time job? is that what you are saying mkuu? are you serious?

2. Unasema kuwa ubalozi ni another level kuliko unaibu katibu wa CCM taifa, what a nonesense? Mwambi kama hana uwezo kiuongozi alikuwa hatari kwa taifa akiwa naibu-katibu wa CCM au akiwa balozi Urusi?

Unajua kama definition yako ya ufisadi ni pamoja na kusimamia common sense, basi kutojua unachokisema ndio ufisadi hasa, maana hapa unaonyesha kuwa huelewi madhara ya kuwa na kiongozi wa taifa wa chama tawala asiyekuwa na uwezo, kuwa anaweza kuleta madhara makubwa kwa sababu anahusika directly kwenye maamuzi muhimu ya taifa letu kuliko akiwa Urusi, hili nalo linahitaji darasa kuelewa? au mapka uwe fisadi ndio utaelewa?
 
Mkuu FMES, heshima mbele, let's stick to the issues.

1. Ujumbe wa NEC ni kazi ya kumfanya mtu asifanye kazi ya kumpatia kipato? Unasema ujumbe wa NEC ni a full time job? is that what you are saying mkuu? are you serious?

Kama mtu anatafuta kazi ya kipato then uongozi wa kisiasa Tanzania is not the place.Watu wengi wenye profession na qualification za kuwa mabalozi wana uwezo wa kufanya kazi katika mashirika ya kimataifa na kupata hicho "kipato" unachokiongelea.Kama mtu anaingia katika utumishi wa serikali kwa kutafuta "kipato" ndiyo mwanzo wa kuleta ufisadi.

2. Unasema kuwa ubalozi ni another level kuliko unaibu katibu wa CCM taifa, what a nonesense? Mwambi kama hana uwezo kiuongozi alikuwa hatari kwa taifa akiwa naibu-katibu wa CCM au akiwa balozi Urusi?

Correct,

Ukatibu mkuu wa CCM taifa ni kazi ya chama, CCM just happens to be the ruling party lakini kama isingekuwa hivyo huyu mtu anakuwa sawa na wenzake wa CHADEMA na wengine.Kwa hiyo mimi naweza nisiwe concerned na katibu mkuu wa CCM kama hajui kusoma na kuandika so long as hawatuletei madudu yake katika serikali.Na akileta madudu yake katika serikali nitamwambia upuuzi wenu lishaneni huko huko CCM msitake kutuambukiza watu tusio na party affiliation.

Balozi hata kama ni member wa NEC, anafanya kazi katika capacity ya kiserikali.As long as you are Tanzanian serikali ni moja tu na hii ndiyo sababu inanifanya mimi kama mtanzania niwe na outrage kuona hawa ideologues wanachaguliwa kuwa mabalozi wakati kuna watu kibao wanauzoefu na international relations wanaachwa.

Definition yangu ya ufisadi ni pamoja na ubadhirifu, ubadhirifu wa mali ya umma, ubadhirifu wa trust ya umma. ubadhirifu wa madaraka ya umma.Kama rais atabadhiri madaraka aliyopewa kuteua mabalozi kwa kutapanya political favors badala ya kuteua watu wenye qualifications basi rais ni fisadi na wanaomtetea ni mafisadi by proxy, whether wanajua hilo au hawajui.
 
Sasa exactly unachosema ni nini? Tatizo lako hasa lipo wapi mkuu balozi kuwa mjumbe wa NEC au Mwambi kutokuwa na qualifications za kuwa balozi?

Sioni tatizo lolote balozi kuwa mjumbe wa NEC, ambayo hukutana mara chache sana labda mara mbili au tatu kwa mwaka, na serikali haijawahi kumlipia balozi yoyote safari za kuhudhuria vikao vya chama, sasa what the is outburst for?
 
Jaka Mwambi is an ideologue with neither qualifications nor experience in international relations.He is being awarded the ambassadorship as a political favor at the expense of Tanzania's economy and foreign policy.I am against the habit of presidents appointing emissaries based on political favors.There are so many bright diplomats that can do the job much better.This is my outrage.

The NEC issue was icing on the cake that you brought to the discussion by giving the Job Lusinde example.I am against an ambassador having obligation to a home constituency as pointed out in my Pius Ng'wandu example.Perhaps the nature of NEC's meetings may be a little bit tolerable than ubunge, but the principle stays the same.As a matter of fact kumleta mtu "mara mbili au tatu kwa mwaka" kutoka Urusi au Japan kwa taifa masikini kama Tanzania siyo mchezo, not to mention akiwa huku kule ofisi inakosa balozi.Kama kuna watu wanaweza kufanya kazi hizi hapa nyumbani kwa nini tulundikie responsibilities kibao mtu mmoja?

Ningependa kuona ideologues kama kina Jaka Mwambi hawachaguliwi kuwa mabalozi na badala yake career diplomats wanachaguliwa.Career diplomats by definition hawawezi kuwa tangled up in NEC au ubunge kwa hiyo by appointing career diplomats (mijitu iliyokuwa mi first secretaries na attaches kwa miaka kadhaa maubalozini au iliyokaa MOFA na kupikwa vya kutosha katika foreign policy ya TZ) tunaondoa issue nzima ya balozi kuwa mbunge au member wa NEC.
 
Jaka Mwambi is an ideologue with neither qualifications nor experience in international relations.He is being awarded the ambassadorship as a political favor at the expense of Tanzania's economy and foreign policy.I am against the habit of presidents appointing emissaries based on political favors.There are so many bright diplomats that can do the job much better.This is my outrage.

I full disagree with you!!! Mambo ya experience yamepitwa na wakati!!!

Watu wengi wenye experience wanaboa... are you saing ilikuwa poa maheremu Pual Bomani alivyokuwa kwenye kila board ya kampuni hapa nchini, kwa sababu ya experience... na makampuni almost yote yamekufa?
 
Back
Top Bottom