Jaji warioba: Tumejipanga kuwa na katiba mpya 2014

armanisankara

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
283
49
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Warioba (kushoto) akiongea na Mawaziri wa Katiba na Sheria kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Mathias Chikawe (kulia) na Abubakar Khamis Bakari (kulia kwa Jaji Warioba) nje ya ofisi za Tume mara baada ya Mawaziri kutembelea ofisi za Tume leo (Jumatatu, Sept. 3, 2012). Katikati ni Naibu wa Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki na wengine ni watendaji kutoka Tume na Wizara za Katiba na Sheria (Picha na Tume ya Katiba).Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imesema imejipanga kukamilisha majukumu ndani ya muda uliowekwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 na hivyo nchi kuwa na Katiba Mpya ifikapo mwezi Aprili, 2014.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Joseph Warioba amewaeleza Mawaziri wa Katiba na Sheria kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa pamoja na changamoto zilizopo, dhamira hiyo ya Tume ipo palepale.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom