Jaji Warioba ambana Jussa kuhusu Muungano wa mkataba

Mtu wa Pwani,

..usije ukasema we did not tell u about this.

..sisi wengine kwa muda mrefu sana tumekuwa tukisema hapa JF kwamba muungano hauwafai wa-ZNZ.

..kwamba mnachohitaji wa-ZNZ ni uhuru kamili na kama ni mashirikiano na Tanganyika basi iwe kupitia EAC,SADC, etc.

..Mh.Jussa awe mkweli tu kusema kwamba wanachotaka wao ni mkataba na Tanganyika. mkataba huo unaweza kuwa ktk masuala ya ulinzi na usalama, au uhamiaji etc.

..hili suala la kusema eti "muungano wa mkataba" ni ujanja-ujanja tu wa kuficha nia ya kuvunja muungano.

..sielewi kwanini Jussa anasita kutamka kwamba muungano uvunjwe, badala yake anajificha nyuma ya kauli mbiu ya "muungano wa mkataba."

Mtu mzima mwenye akili timamu anapodhamiria kufanya nyeti kama la hatma ya nchi basi anakuwa amejipanga vema ana anajua ataangukia wapi kama mambo yatakwenda tofauti. Jussa na wenzake ni wazi hawajajipinga na mbaya zaidi hawajui wanataka nini? Matokeo yake wanajikuta wamejikaanga wenyewe kwa mafuta yao. Utadai vipi muungano wa mkataba wakati uliopo sasa ni wa mkataba? Vunja kwanza huu uliopo ndio uanze ukurasa mwingine, lakini huwezi kula huku na huko ukidhani kila mtu kalala usingizi wa pono!

Matusi na kejeli za wakina Jussa vitaigharimu Zanzibar, Tanganyika watataka sasa wajue (hata kwa muungano wa sasa) Zanzibar wanaweka nini mezani? Hoja ya mgawanyo sawa wa rasilimali kwa madai kuwa tuna nchi mbili ni lazima yaendane na maelezo ya gharama toka kila upande. 50/50 vinginevyo wakae watulie.
 
Baada ya miaka 300, Wascottish yamewatosha. Cameroon amekubali yaishe. Bofya link
kilataifakubebamzigowakeaaha

Kwanini Zanzibar wasifanye kama Scotland kama kweli wanataka 'uhuru? Kwanini Maalim Seif badala ya kuzurura Ulaya asifanye kama anavyofanya Alex Salmond na kuitisha kura za maoni?

Tatizo ninaloona kwa hawa vinara wa kudai uhuru wa Zanzibar ni kurukia mambo. Mara Swiss, mara Senegambia mara mkataba. Na wewe unatuletea Scotland!

Kuna tofauti kubwa sana kati ya Scotland na Zanzibar na kwa hakika kuna tofauti kubwa sana kati ya Alex Salmond (kiongozi wa Scottish National Party) na Maalim Seif. Na moja hizo tofauti ni kwamba Salmond anajua atakata nini and he can articulate his idea/plan. Maalim Seif anataka nini, uhuru kamili, kupumua au mkataba?
 
FJM,

..binafsi naamini Jussa na kundi lake wamejipanga, na wanakwenda vizuri tu ktk malengo yao ya kuuvunja muungano.

..wameweza kupandikiza chuki miongoni mwa wa-Zanzibari dhidi ya wa-Tanganyika. kama huamini tembelea www.mzalendo.net soma maoni yao, na pia angalia video za mikutano ya UAMSHO.

..hata kama Jussa ameshindwa kutetea hoja yake mbele ya Jaji Warioba, muungano huu hauwezi ku-survive kutokana na chuki[pombe,umalaya,ushoga,ukimwi,ujambazi,madawa ya kulevya..vyote vinatokea Tanganyika] na fitina ambazo Jussa na kundi lake wamepandikiza.
 
Last edited by a moderator:

Muungano utavunjika na sababu ni Tanganyika kuchoka kusikiliza matusi huku wanalipa bills.
 
Hakika JUSSA anawakosesha usingizi waTanganyika na hata kumuona ni mwiba mkuu.

Hongera sana Jussa hakika wewe ni kichwa.

Jussa? kwa lipi? Wenye akili Zanzibar wanatumia akili wasio na akili wanatumia mdomo, lakini bahati mbaya wanaongea vapor, hoja zao hazina mashiko.
 
Mtu wa Pwani,

..usije ukasema we did not tell u about this.

..sisi wengine kwa muda mrefu sana tumekuwa tukisema hapa JF kwamba muungano hauwafai wa-ZNZ.

..kwamba mnachohitaji wa-ZNZ ni uhuru kamili na kama ni mashirikiano na Tanganyika basi iwe kupitia EAC,SADC, etc.

..Mh.Jussa awe mkweli tu kusema kwamba wanachotaka wao ni mkataba na Tanganyika. mkataba huo unaweza kuwa ktk masuala ya ulinzi na usalama, au uhamiaji etc.

..hili suala la kusema eti "muungano wa mkataba" ni ujanja-ujanja tu wa kuficha nia ya kuvunja muungano.

..sielewi kwanini Jussa anasita kutamka kwamba muungano uvunjwe, badala yake anajificha nyuma ya kauli mbiu ya "muungano wa mkataba."

nimefatilia maelezo ya Jaji na majibishano ya pamoja na Profesa kabudi. nimetafakari kwa kina kua huu muungano na malalamiko yake hapana suluhishi jengine ila kurudi square zero, nao ni kuuvunja, halafu kama kuna umuhimu wa tanganyika na zanzibar kufunga baadhi ya mikataba ya mashirikiano kwenye sehemu watakazoona zinafaa.

kinachonipa tabu mm, ni kwa nn watetezi wetu, ambao walitushawishi juu ya kutuonyesha kasoro hizi za muungano, na kuja na plan ya mkataba, nikiamini kidhati wakijua kua lengo la mwisho ni kuuvunja wanashindwa kujiamini na badala yake wanauma uma maneno. ningefurahi sana Jussa na wenziwe wangemueleza wazi Jaji warioba na wenziwe kuwa lengo la mkataba kweli ni kuondoa muungano huu tulionao na kuangalia uwezekano wa kuja na mkataba wa mambo tunayokubaliana kwa lugha nyengine si muungano bali ni makubalino ya mambo ya kushirikiana.

nna shaka na mwenendo unavyokwenda na kuchanganyikiwa kwa manahodha, kama safari itafika salama. kwa masikitiko nimesikia pia mh rais Shein amamfuta kazi Mansour mmoja wa manahodha wa Muungano wa mkataba, sijui kwa kiasi gani inaweza kuchangia kuyumba au kupoteza dira safina yetu.

MM SIUMI MANENO MUUNGANO TUUVUNJENI KILA PANDE IPUMUWE, MUUNGNO WA TEMBO NA SISIMIZI NO, TENA NOOOO
 
kutoa maoni ni sawa lakini lazima uwe na uhakika na uthibitisho na kitu unachokisema mkuu, pia uweze kuitetea hoja kwa ushahidi
 
Jusa ni kipofu , jusa Tanganyika ikirudi utakuwa upande wa pemba au unguja? usilete siasa za majitaka kwenye masuala ya muungano
 
Mbona mm nimemuona jaji warioba akijiuma uma wakati anajibiwa na jusa kama yy hajui maana ya muungano wa mkataba y alikua anachukua maoni hayo kwa wananchi hii habari imekaa kiuzushi uzushi nadhani ilikua ya mwandishi wa nipashe anaeitwa mwinyi sadala
 
FJM,

..binafsi naamini Jussa na kundi lake wamejipanga, na wanakwenda vizuri tu ktk malengo yao ya kuuvunja muungano.

..wameweza kupandikiza chuki miongoni mwa wa-Zanzibari dhidi ya wa-Tanganyika. kama huamini tembelea www.mzalendo.net soma maoni yao, na pia angalia video za mikutano ya UAMSHO.

..hata kama Jussa ameshindwa kutetea hoja yake mbele ya Jaji Warioba, muungano huu hauwezi ku-survive kutokana na chuki[pombe,umalaya,ushoga,ukimwi,ujambazi,madawa ya kulevya..vyote vinatokea Tanganyika] na fitina ambazo Jussa na kundi lake wamepandikiza.
Wacha hizo, ati pombe,umalaya, ushoga na ukimwi,ujambzi, madawa ya kulevya vinatokea Tanganyika.

Unajidanganya sana na naona kama unataka kuumbuliwa hapa jamvini.
Kwani unafikiri mabaibui yaliyosheheni wake za watu yanayopita usiku usiku hatuyajui?

Na unataka tumuumbue mama wa kiongozi mkubwa sana ambaye ni fuska wa kutupwa?

Na wizi wa viwanja vya serikali huko Zenj vimefanywa na waTanganyika?

Na je unahabari ya gay sex tourism ya wamarekani wanaoisifia Zanzibar?

Wacha hizo!
 
Ukiangalia video ya kongamano la jumamosi tarehe 6, utasikia wakisema kuwa muungano wa mkataba wamempa nakala Sheni na Maalimu Seif. Kinyume na hayo hawatakubali maoni ya tume.
Hii maana yake ni kuwa tayari wameshaamua wanataka nini na ni lazima Tanganyika ifuate kile wanachokitaka wao.
Wapuuzi hawa wanaamini hivyo!

Kwa upande mwingine Jusa amekiri kuwa ZNZ inaihitaji Tanganyika, kindugu, kiusalama, kiuchumi na kisiasa.
Kiuchumi wanajua kuwa jirani anayeweza kuwaweka sawa ni Tanganyika. Wanajua kuwa nusu ya WZN wanaishi Tanganyika. Chumo la WZN linategemea Tanganyika kama soko la kila kitu kuanzia biashara, ajira n.k

Wanachokitaka hawa akina Jusa ni ZNZ kamili, lakini uwepo mkataba kama wa EU wanavyosema.
Maana yake waweze ku-move kutoka kwao kuja Tanganyika, wapate ajira, wapate huduma za jamii kama elimu na Afya, wapate ardhi, ajira kwa uchache wa kuvitaja.
Wanajua kuwa hawana bajeti ya ulinzi na hilo likiwa nje ya muungano litawaumiza sana.

Wamejipanga sana kuhakikisha kuwa mahusiano na Tanganyika ni kwa faida yao.
Fikiria kuwa katika kongamano hilo wameazimia mambo yafutayo
1. Wawe na kiti UN (Kwa maneno mengine hiyo ni nchi huru kama ilivyo Burundi au Rwanda). Hakuna tatizo
2. Wanataka sarafu yao (Hilo halina tatizo)
3. Wanataka bunge lao (hilo halina tatizo)
4. Mfumo wao wa elimu utakaohusisha mitaala ya Cambridge(Halina tatizo)

Hadi hapo hiyo ni nchi kamili kwasababu walishakuwa na bendera, wimbo wa taifa n.k

Wasichokitaka kiwe chao ni
1. Ulinzi na usalama (Wakijua kuwa hilo ni tatizo kubwa)
2. Uhamiaji (Ili watu wao waendelee kujazana Tanganyika)
3. Utumishi (Ili watu wao wapate ajira)
4. Elimu ya juu (ili watoto wao wasome bure)
5. Ardhi (kwasababu hilo ni tatizo kubwa kwao)

Tanganyika inatakiwa isibabike, waacheni waende zao.
Jiulizeni kama wana nia njema kwanini wanaficha huo mkataba wanaoutaka?

Ahmed Rajab ndiye kiongozi wa mkataba, Jusa na Maalimu ndio waimbishaji, kwa bahati mbaya sana Wazanzibar ni wanakwaya wazuri, weka tungo zenye vina wataimba tu hata kama zinawatusi.
Waliulizwa kuhusu serikali 3 hawakuweza kujibu, Jusa kaulizwa mkataba naye ni mweuupee! yeye anajua mkataba tu halafu tutatafuta formula.

Formula ya mkataba mwisho CHUMBE, Ujinga mwisho chumbe na ujuha mwisho chumbe.
Ukikanyaga Rasi kilomoni, adabu mbele, akili kichwani.
LET ZNZ GO!
 
Kwani Jaji warioba wanaruhusiwa kuhoji mawazo ya mtu au wanapaswa kuyachukua kama yalivyo na wao wakayachambue. Kumbana Jusa na maswali hata kama hoja yake ni ya kishenzi, Jaji warioba amjidhalilisha kwa sababu hiyo sio kazi ya tume kwa hatua hii.
 
Warioba ni roboti?
 
Wahafidhina wasiokubali mabadiliko, usia wa mwalimu, ni serikari mbili, upeo wa fikra ndo umeishia hapo. Hayo ni matokea ya hoja za nguvu na misingi iliyojengewa taifa hili, matokeo yake sasa taifa linamong'onyoka.
 
Nimeshangazwa sana na Huyu Jaj Warioba ,nafikiri sasa hivi yuko katika wakati mgumu sana katika mchako wa kukusanya maoni ya katiba mpya,ninavyoamini anapata misukumo kutoka kwa chama tawal ccm ,lakini sisi wazanzibari tunamwambia kama ataendelea kufanya kile alicho amrishwa na hao vibaraka wake basi anaweza kulitumbukiza taifa letu pabaya sana.

Juzi kulikuwa na ukusanyaji wa maoni ya katiba mpya katika baraza la wakilishi,nimeshangazwa sana na warioba eti anamuuliza jussa kuwa tunataka muungano wa mkataba upi na apewe mifano,inachekesha sana,hata yule mtoto mdogo zanzibar mwenye umri wa miaka 14 atakueleza nini maana muungano ya mkataba. Jengine zaidi alitaka apewe mifano japo mmoja wa muungano wa mkataba huo.

Sasa mimi namuambia Jaji Warioba kama anataka kujua Muungano wa mkataba ni upi ,tayari wananchi washatoa maoni katika tume yake kuwa wataka muungano wa mkataba wa aina gani,na vipi uwe ,au yale maoni walio chukua hakukabiziwa na vijana wake ? Inawezekana maoni yale walio anza kuchukua tayari washatia kapuni watueleze kabisa.

Mimi Nitamdokezea tu kwa maoni ya ya mchakato wa katiba .

Nataka muungano wa shirikisho au kwa jina jengine mkataba,muungano nakupa mfano kama ule wa EU.

Aina ya kwanza ni kama mfano wa European Union ambapo nchi huru hukubaliana kushirikiana katika mambo fulani ambapo mambo hayo hushughulikiwa na commission au tume ambayo inaongozwa na commissioner/KAMISHNA. Commisiion hii huwa ndogo na kazi yake ni kuratibu na kusimamia yale mambo ambayo yamekubaliwa tu. European Union ni mfano mzuri wa ushirikiano huu ambapo ulianza na European Steel and Coal Corperation mwaka 1955, ikabadilika jina ukawa European Economic Community EEC, baadae ikabadilika ikawa European Community EC na mwisho ndio hii inayo endelea hadi sasa European Union EU. Hawa wanashirikiana kwa mambo maalum hasa yanayohusu uchumi, huduma, ajira na nyenginezo.

Aina nyengine ya ushirikiano wa mkataba hujengwa kwa TREATIES Mikataba ambayo nchi husika huamua kushirikiana kwa mambo hayo, katika aina hii ya ushirikiano hakuhitajiki Commission wala serikali ya pamoja badala yake kila nchi ambazo zimo katika ushirikiano huo huunda DESK la ufatiliaji ndani ya nchi kwa yale mambo ambayo wamekubaliana kwenye hizo TREATIES, mfano mzuri ni jumuia ya ushirikiano wa nchi za kusini mwa ASIA kifupi zinaitwa ASEAN au ASSOCIATION OF EAST ASIAN NATIONS. ushirikiano huu umejengwa bila kuwepo na commission na ndio mfumo ambao unatufaa sisi ili kuondoa harama zisizo za lazima na malalamiko, tutakubaliana kushirikiana kwa baadhi ya mambo ambapo kila nchi itakuwa na deski la ufatiliaji ushirikiano huo jinsi unavyotekelezwa, na kila nchi itabakia kuwa na UTAIFA WAKE,hicho ndiccho tunacho kitaka sisi wananchi.

Tanganyika iwepo juu ya meza,zanzibar ipo juu ya meza tufanye shirikisho tu,na hili tunaamini linaweza kuleta matunda makubwa,matunda hayo nchi jirani zinaweza kuungana na sisi kwa aina hio ya shirikisho,lakini sio muungano huu tulio naoo na magube na usanii.

Nashangazwa umekuwa mkali sana,katika hadidu rejea inasema kuwa haturuhusiki kuongea suala la muungano kuvunja ,bali tunaruhusika kuongea jinsi ya kuuboresha muungano zaidi,ndio sisi wazanzibari tumeamua kutoa maoni yetu,tumefanya discusion vya kutosha kabla mchako wa katiba,tumeona kuwa muungano wa shirikisho ndio muungano pekee utakao maliza kero za muungano na manung'uniko kutoka katika pande hizi za muungano.

IKIWA unataka kujua muungano wa mkataba zaidi vipi tutauwendesha,njoo ufungue kongamano zanzibar,njoo na tume yako tutawafahamisha vizuri.
 
Wacha hizo, ati pombe,umalaya, ushoga na ukimwi,ujambzi, madawa ya kulevya vinatokea Tanganyika.

Unajidanganya sana na naona kama unataka kuumbuliwa hapa jamvini.
Kwani unafikiri mabaibui yaliyosheheni wake za watu yanayopita usiku usiku hatuyajui?

Na unataka tumuumbue mama wa kiongozi mkubwa sana ambaye ni fuska wa kutupwa?

Na wizi wa viwanja vya serikali huko Zenj vimefanywa na waTanganyika?

Na je unahabari ya gay sex tourism ya wamarekani wanaoisifia Zanzibar?

Wacha hizo!
masopakyindi,

..what u understood is not what i meant.

..nilichosema ni kwamba wa-ZNZ wamejazwa CHUKI dhidi yetu wa-Tanganyika.

..sasa hivi kila tatizo linalowakabili iwe kijamii,kisiasa,kiutamaduni,na kiuchumi, wanaamini limetokana na muungano, au wa-Tanganyika kutia mguu Zanzibar.

..ukiangalia video za Uamsho utaona chuki hizo na madai yao. kwa mfano, wapo wanaodai kwamba muungano ndiyo umepeleka popobawa Zanzibar.

..natumaini utakuwa umenielewa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom