Jaji Warioba ambana Jussa kuhusu Muungano wa mkataba

Mkuu
Ungeweka makala yote, ambayo itamwacha mtu kujitafsiria vile apendavyo.

Makala hii link Home

Baada ya kuisoma makala hii. Jussa anasema ukifika wakati mwafaka serikali zitakaa na kuamua vipi zigawane madaraka. Inaonekana una msimamo wako kuhusu Jussa na umepata nafasi ya kumpiga madongo.

Alichosema Jussa ni kuwa "kesi iko mahakamani, hapaswi kuizungmzia" lol.
Mkuu Nonda, huyu Jussa is strongly anti Watanganyika kwa sentiments anazozifahamu mwenyewe.
Amekuwa akipiga domo daima dumu na kutukana waTanganyika walioko Visiwani na hata walioko Tanganyika.

Kwa upande wangu sina sababu yoyote ya kutompiga madongo kwa msimamo wake huo.
Suala la kuumbuliwa na Jaji Warioba nafikiri si kwa bahati mbaya, kwa kufanya hivyo amuonyesha ulimwengu alivyo debe tupu lisilo acha kutika.

Mshaurini huyo Jussa ,a sijifiche nyuma ya pazia la "kesi iko mahakamani", wakati wa mbichi na mbovu ni sehemu kama lipoitiwa, Tume ya mabadiliko ya katiba.

Suala aliloulizwa lilikuwa simple, aeleze au atoe mifano ya mikataba ya muungano anayoitetea, akashindwa kufanya hivyo.

Ni dhahiri kuwa licha ya maneno mengi , uelewa wa sheria ni kiduchu, na hata research hajafanya kwa kitu anachokitaka kisheria.

Kwenye sehemu za wasomi huyu jamaa mshaurini asikimbilie kiti cha mbele, asije umbuka bure kama hivi sasa.
 
Mkuu Nonda, huyu Jussa is strongly anti Watanganyika kwa sentiments anazozifahamu mwenyewe.

Mshaurini huyo Jussa ,asijifiche nyuma ya pazia la "kesi iko mahakamani", wakati wa mbichi na mbovu ni sehemu kama lipoitiwa, Tume ya mabadiliko ya katiba.

Kwenye sehemu za wasomi huyu jamaa mshaurini asikimbilie kiti cha mbele, asije umbuka bure kama hivi sasa.

Mkuu
Ushauri uliotoa hapa, natumai wadau wake watamfikishia.

Pia kama umeangalia picha, link ipo post # 46 Jussa amekaa nyuma.

Mimi katika ile makala kuna vitu mbili imenivutia.

Moja hii: Akifafanua, Jaji Warioba alisema kimsingi kudai Zanzibar iwe na mamlaka kamili, huku Tanganyika nayo ikiwa na mamlaka yake ni sawa na kuvunja muungano.

Si kawaida kwa Jaji Warioba kutumia neno Tanganyika. Jee Mzee Warioba ameanza kuhisi sasa kiini macho na madudu ya muungano yameanza kufahamika kwa wadanganyika wengi?(aka wananchi tunaoburuzwa na CCM)

La pili hili :
Akishauri Nahodha alisema hata hivyo ni vyema ikafika mahali kukawa na mabunge mawili , moja dogo litakaloshughulikia mambo ya Muungano na jingine lishughulikie mambo ya Tanganyika.

Link ya makala http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=46930

Katika haya mawili una maoni gani?

Unafikiri Tz bara (ukiini macho), irudishe jina lake la asili, Tanganyika(uhalisia)? na pia iwe na bunge lake kwa mambo ya Tanganyika?
 
Mkuu Nonda, huyu Jussa is strongly anti Watanganyika kwa sentiments anazozifahamu mwenyewe.
Amekuwa akipiga domo daima dumu na kutukana waTanganyika walioko Visiwani na hata walioko Tanganyika.

Kwa upande wangu sina sababu yoyote ya kutompiga madongo kwa msimamo wake huo.
Suala la kuumbuliwa na Jaji Warioba nafikiri si kwa bahati mbaya, kwa kufanya hivyo amuonyesha ulimwengu alivyo debe tupu lisilo acha kutika.

Mshaurini huyo Jussa ,a sijifiche nyuma ya pazia la "kesi iko mahakamani", wakati wa mbichi na mbovu ni sehemu kama lipoitiwa, Tume ya mabadiliko ya katiba.

Suala aliloulizwa lilikuwa simple, aeleze au atoe mifano ya mikataba ya muungano anayoitetea, akashindwa kufanya hivyo.

Ni dhahiri kuwa licha ya maneno mengi , uelewa wa sheria ni kiduchu, na hata research hajafanya kwa kitu anachokitaka kisheria.

Kwenye sehemu za wasomi huyu jamaa mshaurini asikimbilie kiti cha mbele, asije umbuka bure kama hivi sasa.

hata warioba debe tupu yupo kwa maslahi ya tanganyika msaidie na wewe kutupa mfano mmoja tu katika dunia hii badala t'nia ni nchi gani yenye aina ya muungano kama huu wa upande mmoja tatizo mna chuki nae jusa kwa ukweli anaowaeleza
 
Granted.

Lakini hata hiyo CCM sponsored process, once ukishakubali kushiriki, umeshai legitimize.

Na hapa tunaona muwakilishi wa upinzani -CUF- anajiumauma, anasema anataka muungano wa mkataba, anaulizwa mkataba wa aina gani, ooh nina mifano 100, haya tupe mfano mmoja basi tuusome tujue unamaanisha nini.

Anajiuma.

Watu wanaulizwa wanataka katiba ibadilishwe vipi, wanasema mambo ya ajabu huko, mara nchi iwe na muhimili wa dini kama nyongeza ya executive, legislature and judiciary. Watu wanataka katiba iruhusu kuoa wake mitala wakati haki za kikatiba kufanya hivyo zipo tayari.

Huwezi kuwa na a meaningful constitutional review process kama watu wako hawajui hata kusoma na kuandika kwa viwango vinavyotakiwa.

Na hapo ndipo CCM inapopata ushindi, mpeleke Warioba aende kusikiliza Waswahili wanaobishana mambo legal kwa unazi.

Matokeo yake mtu anasema ana mifano 100, anaambiwa taja mmoja, ananywea.

Ny father is stronger than your father style!

MKUU unategemea mtu aliyesoma Elimu dunia awe na akili kweli?.
 
mm nilifatilia yale mazungumzo, kwa kweli nimesikitishwa na mengi sana.

niweke wazi mm ni muumini nnaeamini kua zanzibar tunataka mamlaka kamili, na nilizani kua mkataba ndio njia njema ya kutufikisha tupatakapo.

baada ya kusikiliza nimegundua wenye kutaka tuelekee kwenye mkataba hawajajipanga, akiwemo alhabiby Jussa. maana mheshimiwa katuuliza kama mkataba si upo wa Afrika mashariki, kwa hio ww unazungumzia kuvunja muungano na tukutane huko. au unasemaje. akasema swahib wangu kwa kujiuma uma kua yy hataki kuvunjika kwa muungano bali uwe wa mkataba, sasa tueleze mgawanyo wake na uendeshaje wake utakuwa vp ? rafiki yangu kaanza kutuangusha ss wafuasi wake. kwa kweli kwa elimu yangu hii ya darasa la saba nimeanza kun'gamua kua nimepandia gari bila kuangalia linaelekea wapi. sasa nimkamate konda anishushe kabla sijapotea na nikashindwa kujua vya kurudi.

MSIMAMO ULIO SAWA NNAONA NI KUA KILA NCHI IWE HURU NA PASIWEPO MUUNGANO WOWOTE, TUKUTANE EAC, AU, SADC AU COMESA AU UN. HAKUNA SULUHISHO JENGINE.
 
Hivi bara hivi visiwa vina manufaa gani kwetu? Mi naona tuachane navyo kwanza wanapandikiza chuki tu.
 
Tatizo hapa mnakuwa mnashindanisha vichwa viwili tofauti. Cha awali ni kile chenye kusema ukweli na kusimamia haki na kile chenye unafiki na uroho wa madaraka na kupenda ukubwa.

Binafsi namfahamu sana Joseph Warioba tokea akiwa wizara ya sharia na naujua uwezo wake vilivyo sana. Naweza kusema ni mganga njaa tu kama angekuwa mtu makini asingeweza kukubali TUME hii kwani alishawahi kuongoza Tume ya Rushwa lakin mpaka leo ipo kwenye kabati na hata hii kama angekuwa mtu makini asingekubali kwani alikatazwa kuujadili muungano.

Kwa hayo tu unajuwa fika huyu ni mganga njaa na mpenda madaraka japo hana uwezo nayo. Je mnajuwa kuwa aliwahi kughushi kura huko kwao BUnda na ubunge wake ukateuliwa.

Naamini wazi Warioba huyu hana uwezo kabisa wa kushindana na kijana kama JUSSA. Namshangaa baba zima kama hili linatolewa kamasi na mapovu na mwanasharia wa juzi juzi tu.

Ushauri wangu kwa Warioba: kama umekosa asubuhi huwezi pata jioni. Hishma ni bora kuliko vyeo.

Hapo kwenye RED kunaeleza kinachokusuma kuandika haya!

Mkuu ingekuwa vyema tungeona clip ya maojihano ili tuwe kwenye nafasi nzuri kujadili bila kusukumwa na personalities za watu (Jussa na Warioba).

Lakini nilikuwa nshasikia watu wakilalamika kuwa, tume ya katiba inawafanya watu kama vile wapo mahakamani (Kwa kuwabana na maswali) badala ya kuchukua maoni yao. Japo naamini maswali ni muhimu kama mtu akiwahajaeleweka ili tume isiwe na tafsiri tofauti na ile iliyolengwa na mtoa maoni.

Kwa ili la Jussa kaambiwa wewe unataka kuvunja Muungano sijui limekaaje tena!
 
Hakika JUSSA anawakosesha usingizi waTanganyika na hata kumuona ni mwiba mkuu.

Hongera sana Jussa hakika wewe ni kichwa.

Huyo kichwa mwenye mifano zaidi ya 100 ameshindwa kutoa hata mmoja ndio unamsifia! Si yeye, Duni Haji, Seif wala Pro Lipumba anaweza kutoa mifano hata miwili ya Muungano wa Mikataba, ni kujaza ujinga tu akili za watu.

Jiondoeni tu ktk Muungano, mjiunge na ndugu zenu wa Visiwa vya Comoro muendelee kuzalisha wakimbizi na kupata haki ya kuzamia Ulaya.
 
Mkuu
Ushauri uliotoa hapa, natumai wadau wake watamfikishia.

Pia kama umeangalia picha, link ipo post # 46 Jussa amekaa nyuma.

Mimi katika ile makala kuna vitu mbili imenivutia.

Moja hii: Akifafanua, Jaji Warioba alisema kimsingi kudai Zanzibar iwe na mamlaka kamili, huku Tanganyika nayo ikiwa na mamlaka yake ni sawa na kuvunja muungano.

Si kawaida kwa Jaji Warioba kutumia neno Tanganyika. Jee Mzee Warioba ameanza kuhisi sasa kiini macho na madudu ya muungano yameanza kufahamika kwa wadanganyika wengi?(aka wananchi tunaoburuzwa na CCM)

La pili hili :
Akishauri Nahodha alisema hata hivyo ni vyema ikafika mahali kukawa na mabunge mawili , moja dogo litakaloshughulikia mambo ya Muungano na jingine lishughulikie mambo ya Tanganyika.

Link ya makala Home

Katika haya mawili una maoni gani?

Unafikiri Tz bara (ukiini macho), irudishe jina lake la asili, Tanganyika(uhalisia)? na pia iwe na bunge lake kwa mambo ya Tanganyika?
Mkuu Nonda, muungano inbidi uwe kwa ridhaa za pande zote mbili, yaani Zanzibar na Tanganyika, kama zilivyokuwa kabla ya mwaka 1964.
Si kweli kwamba Warioba amelitumia Jina la Tanganyika kwa kutambua kuwa muungano ndo kwaheri.
Tanganika itabaki kuwa Tanganyika na hata Mwalimu alilitumia sana kueleza mikanganyiko ya muungano.

Ni dhana potofu kufikiri kwamba Tanganyika tunautaka sana muungano,zaidi ya kubeba matatizo ya kiuchumi ya Zanzibar , Tanganyika inachofaidika na huo muungano ni kidogo sana.

It takes two to tango,kama Zanzibar hawautaki muungano suala simple ni kuligomea bunge la muungano na kurudi Zanzibar ili taratibu za kugawana mali na madeni zianze.

Siafiki mawazo ya Mhe. Nahodha, suala ni kama muungano unavunjika kila taifa libebe mzigo wake wenyewe.
 
Barubaru,

Bado sijaona mtu mwenye mifano 100 na kushindwa kutaja hata mmoja anakosesha watu usingizi kivipi.
Halafu hapo tunaambiwa tunakoseshwa usingizi. Talk about a fool applauding another fool!
 
Mkuu ingekuwa vyema tungeona clip ya maojihano ili tuwe kwenye nafasi nzuri kujadili bila kusukumwa na personalities za watu (Jussa na Warioba).

Lakini nilikuwa nshasikia watu wakilalamika kuwa, tume ya katiba inawafanya watu kama vile wapo mahakamani (Kwa kuwabana na maswali) badala ya kuchukua maoni yao. Japo naamini maswali ni muhimu kama mtu akiwahajaeleweka ili tume isiwe na tafsiri tofauti na ile iliyolengwa na mtoa maoni.

Kwa ili la Jussa kaambiwa wewe unataka kuvunja Muungano sijui limekaaje tena!

Mambo ya katiba yanataka specificity.

Mtu anakwambia anataka muungano wa mkataba, of course utataka kumuuliza mkataba wa kivipi.

Tatizo watu wanachuklulia process ya mabadiliko ya katiba kama majadiliano ya kawaida ya siasa ya kawaida. This is a rare opportunity and should be treated so.
 
Ninaanza kuwa na wasiwasi kuhusu uhuru wa kutoa maoni. Tume ipo pale kuratibu mawazo huru kutoka kwa wananchi wote (wasomi na wasio wasomi). Sasa haya ya kumshambulia Jusa yanatoka wapi. Tusilazimishane kuukubali muundo wa sasa wa Muungano. Moja anasema serikali moja, mwingine serikali mbili, mwingine muungano wa serikali tatu, Jusa nae kasema Muungano wa Mkataba (MoU) na mwingine muungano uvunjike na usiwepo kabisa. Hii ndio demokrasia. Mwisho wa siku tutajua ni wangapi wanapenda muungano wa aina gani kutokana na maoni yaliyotolewa. Tume ikianza kujionyesha kuwa wao ni wasomi zaidi kuliko wengine tutapoteza dira na malengo ya mchakato huu.
Yaani katika maoni yote nilosoma basi yako ni best kabisa nakugongea five bila ya wasi mkuu
 
Mahojiano ya warioba na Jussa..

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amembana Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Mkongwe (Cuf), Ismail Jussa aeleze kuhusu mfumo wa uendeshaji wa Muungano wa mkataba unavyopaswa kuwa na mgawanyo wake wa madaraka.
Jaji Warioba alichukua hatua hiyo baada ya Jussa kusimama na kutoa maoni ya kutaka mfumo wa Muungano wa mkataba, wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipokuwa ikichukua maoni ya Wawakilishi mjini Zanzibar jana.Alimtaka Jussa atoe mfano angalau mmoja au miwili ya uendeshaji wa serikali ya mkataba ili Tume yake ipate ufahamu katika mapendekezo yake.

Jussa alisema anayo mifano zaidi ya 100 lakini akadai wakati ukifika serikali zinazohusika zitakaa na kuja na fomula ya mgawanyo huo pamoja na uendeshaji wake kimadaraka.

Hata hivyo, Jaji Warioba kwa upande wake akionekana kutoridhika na maelezo hayo ya Jussa alimtaka kuiambia Tume alivyojiandaa na Muungano wa mkataba kinyume na mfumo dola uliopo.

“Bwana Mwakilishi hebu tupe lau mfano mmoja au muundo wa uendeshaji wa Muungano wa serikali ya mkataba ili uweze kukidhi haja yako na kutuonyesha njia” alisema Jaji Warioba.

“Hebu tuweke wazi juu ya utashi wa mpango unaofikirika wa kuwa wa serikali ya mkataba, nafikiri unachokusudia ni kutaka kuvunja Muungano uliopo” alisema Warioba.
Hata hivyo, Jussa alibaki katika msimamo wake huku akisisitiza kuhusu kukaa kwa serikali mbili na kutoa mfumo wa uendeshaji wa serikali ya mktaba.

Akifafanua, Jaji Warioba alisema kimsingi kudai Zanzibar iwe na mamlaka kamili, huku Tanganyika nayo ikiwa na mamlaka yake ni sawa na kuvunja muungano kwa kuwa kila upande utalazimika kuwa na kiti Umoja wa Mataifa (UN).

“Tanganyika na Zanzibar zikiwa kila moja ina mamlaka yake hakutakuwa na neno Muungano, ndiyo maana nasema nisaidiwe juu ya kupata mfumo wa kuendesha Muungano unaotakiwa chini ya mkataba” alisema Jaji Warioba.

Akiwekea mkazo katika hoja iliyotolewa na Jaji Warioba, mmoja wa Makamishna wa Tume hiyo, Paramagamba Kabudi, alisema inasikitisha kuona hadi sasa wanaotaka Muungano wa mkataba wanashindwa kutoa rasimu ya mfano wa serikali ya mkataba ili kuisaidia Tume juu ya kile wanachokitetea.

Wakitoa maoni yao mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM na CUF waligawanyika pande mbili huku wale wa CCM wakitetea mfumo wa serikali mbili na wa CUF wakitaka Muungano wa mkataba.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Shamsi Vuai Nahodha alisema muundo wa Muungano wa serikali mbili ndiyo muafaka kwa kuwa umeonyesha faida katika masuala ya ulinzi na usalama lakini pia ukijenga umoja wa kitaifa.

Akishauri Nahodha alisema hata hivyo ni vyema ikafika mahali kukawa na mabunge mawili , moja dogo litakaloshughulikia mambo ya Muungano na jingine lishughulikie mambo ya Tanganyika.

Aidha alitaka nafasi ya Rais wa Muungano itolewe kwa zamu kila upande uwe na kipindi cha miaka kumi.

“Mgawanyo wa mapato usiangalie idadi ya watu kwa vile hata kama Serikali moja ikiwa na watu wawili bado ina jukumu la kuwapatia maisha bora na huduma wananchi wake” alisema.

Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Zanzibar Said Ali Mbarouk alisema mfumo wa sasa wa Muungano una matatizo kwakuwa kuna mambo ambayo si ya Muungano lakini yanasimamiwa na Muungano kinyume na makubaliano ya mwaka 1964.

Aliyataja baadhi ya mambo aliyodai yanayoleta mkanganyiko kuwa ni utalii, maliasili, habari na michezo ambayo alisema yanahitaji kuwekewa utaratibu na kuzungumziwa kwake katika medani za kimatifa.

Waziri asie na Wizara Maalum Machano Othman Said alitaka mfumo wa Muungano wa sasa uendelee na kutaka Rais wa Zanzibar kubaki kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohamed Raza alitaka Rais wa Zanzibar awe na mamlaka sawa na Rais wa Muungano pamoja na Zanzibar kupata nafasi ya kujiunga na jumuiya ya OIC na nyingine za kiuchumi duniani.

Tume ya mchakato wa ukusanyaji wa maoni inayoongozwa na Jaji Warioba ipo visiwani Zanzibar na tayari imekutana na wananchi katika mikoa ya Kaskazini Unguja na Pemba.
 
Nchi ya wajinga na magaidi. Unajaribu vuta attention ila kiukweli lazima achemshe kwa vile hajaelimika huyo Jussa.Zaidi ya kufanya fujo hawezi fanya jipya.
 
mm nilifatilia yale mazungumzo, kwa kweli nimesikitishwa na mengi sana.

niweke wazi mm ni muumini nnaeamini kua zanzibar tunataka mamlaka kamili, na nilizani kua mkataba ndio njia njema ya kutufikisha tupatakapo.

baada ya kusikiliza nimegundua wenye kutaka tuelekee kwenye mkataba hawajajipanga, akiwemo alhabiby Jussa. maana mheshimiwa katuuliza kama mkataba si upo wa Afrika mashariki, kwa hio ww unazungumzia kuvunja muungano na tukutane huko. au unasemaje. akasema swahib wangu kwa kujiuma uma kua yy hataki kuvunjika kwa muungano bali uwe wa mkataba, sasa tueleze mgawanyo wake na uendeshaje wake utakuwa vp ? rafiki yangu kaanza kutuangusha ss wafuasi wake. kwa kweli kwa elimu yangu hii ya darasa la saba nimeanza kun'gamua kua nimepandia gari bila kuangalia linaelekea wapi. sasa nimkamate konda anishushe kabla sijapotea na nikashindwa kujua vya kurudi.

MSIMAMO ULIO SAWA NNAONA NI KUA KILA NCHI IWE HURU NA PASIWEPO MUUNGANO WOWOTE, TUKUTANE EAC, AU, SADC AU COMESA AU UN. HAKUNA SULUHISHO JENGINE.
Mtu wa Pwani,

..usije ukasema we did not tell u about this.

..sisi wengine kwa muda mrefu sana tumekuwa tukisema hapa JF kwamba muungano hauwafai wa-ZNZ.

..kwamba mnachohitaji wa-ZNZ ni uhuru kamili na kama ni mashirikiano na Tanganyika basi iwe kupitia EAC,SADC, etc.

..Mh.Jussa awe mkweli tu kusema kwamba wanachotaka wao ni mkataba na Tanganyika. mkataba huo unaweza kuwa ktk masuala ya ulinzi na usalama, au uhamiaji etc.

..hili suala la kusema eti "muungano wa mkataba" ni ujanja-ujanja tu wa kuficha nia ya kuvunja muungano.

..sielewi kwanini Jussa anasita kutamka kwamba muungano uvunjwe, badala yake anajificha nyuma ya kauli mbiu ya "muungano wa mkataba."
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nonda, muungano inbidi uwe kwa ridhaa za pande zote mbili, yaani Zanzibar na Tanganyika, kama zilivyokuwa kabla ya mwaka 1964.

It takes two to tango,kama Zanzibar hawautaki muungano suala simple ni kuligomea bunge la muungano na kurudi Zanzibar ili taratibu za kugawana mali na madeni zianze.

Siafiki mawazo ya Mhe. Nahodha, suala ni kama muungano unavunjika kila taifa libebe mzigo wake wenyewe.
Baada ya miaka 300, Wascottish yamewatosha. Cameroon amekubali yaishe. Bofya link
kilataifakubebamzigowakeaaha
 
Back
Top Bottom