Jaji Warioba ambana Jussa kuhusu Muungano wa mkataba

nafikiri ingekuwa busara sana kuweka mjadala maalum wa wazi ikiwezekana kwenye TV na Radio kati ya JUSSA na Warioba mtajua uwezo mkubwa wa Jussa dhidi ya Warioba.

Dr.Napingana nawe kwa hilo.hoja ya hapa si kutaka kujua nani mwenye uwezo wa kujieleza mbele ya Tv,hoja ni kuomba Mh.Ismail Jussa atusaidie maelezo ya muungano wa mkataba utafanya vipi kazi.Hii ni fursa pekee ya kutoa maoni,wewe unataka utupeleke kwenye tv kutafuta umaaarufu?Jussa huwezi kumlinganisha na Warioba hata kidogo
 
Ninaanza kuwa na wasiwasi kuhusu uhuru wa kutoa maoni. Tume ipo pale kuratibu mawazo huru kutoka kwa wananchi wote (wasomi na wasio wasomi). Sasa haya ya kumshambulia Jusa yanatoka wapi. Tusilazimishane kuukubali muundo wa sasa wa Muungano. Moja anasema serikali moja, mwingine serikali mbili, mwingine muungano wa serikali tatu, Jusa nae kasema Muungano wa Mkataba (MoU) na mwingine muungano uvunjike na usiwepo kabisa. Hii ndio demokrasia. Mwisho wa siku tutajua ni wangapi wanapenda muungano wa aina gani kutokana na maoni yaliyotolewa. Tume ikianza kujionyesha kuwa wao ni wasomi zaidi kuliko wengine tutapoteza dira na malengo ya mchakato huu.

Jussa kaombwa atoe mfanoo mmoja, kasema ana mifano mia, kashindwa kutoa hata mmoja.

Mtu kajiuma mwenyewe, kashambuliwa na nani? Wahuni wa JF ambao hata mungu hawamrehemu?
 
Jussa ni hatari, ni mtu anayepaswa kukimbiwa kama ukoma! Hoja zake mara nyingi kama sio zote ni kutaka kuvunja Muungano tena kwa maslahi ya kisiasa! Kwake yeye CUF inashindwa uchaguzi wa Znz kutokana na nguvu ya Bara, hivyo anaamini endapo muungano utavunjwa, basi CUF itaongoza Znz! Ni uroho wa madaraka wa Jussa sio vinginevyo!
 
Who is Jussa so far? Jussa angalia waomani wanawadanganyeni. Kwao ni jangwa na wanatafuta mahala pa kupumulia wakati wa summer.
 
Tatizo hapa mnakuwa mnashindanisha vichwa viwili tofauti. Cha awali ni kile chenye kusema ukweli na kusimamia haki na kile chenye unafiki na uroho wa madaraka na kupenda ukubwa.

Binafsi namfahamu sana Joseph Warioba tokea akiwa wizara ya sharia na naujua uwezo wake vilivyo sana. Naweza kusema ni mganga njaa tu kama angekuwa mtu makini asingeweza kukubali TUME hii kwani alishawahi kuongoza Tume ya Rushwa lakin mpaka leo ipo kwenye kabati na hata hii kama angekuwa mtu makini asingekubali kwani alikatazwa kuujadili muungano.

Kwa hayo tu unajuwa fika huyu ni mganga njaa na mpenda madaraka japo hana uwezo nayo. Je mnajuwa kuwa aliwahi kughushi kura huko kwao BUnda na ubunge wake ukateuliwa.

Naamini wazi Warioba huyu hana uwezo kabisa wa kushindana na kijana kama JUSSA. Namshangaa baba zima kama hili linatolewa kamasi na mapovu na mwanasharia wa juzi juzi tu.

Ushauri wangu kwa Warioba: kama umekosa asubuhi huwezi pata jioni. Hishma ni bora kuliko vyeo.
 
Hakuwa na nondo za kuback up utetezi wake naona amezoea kwenye majukwaa ambapo hupigiwa vigelegele na ndelemo bila objection
 
Hakika JUSSA anawakosesha usingizi waTanganyika na hata kumuona ni mwiba mkuu.

Hongera sana Jussa hakika wewe ni kichwa.

Kwa hiyo unachotaka sema watu wanao'kosesha' usingizi watu wa Bara (if at all wanakosesha mtu usingizi...rejea nukuu ya JK: Kelele za mlango....) wanastahili 'hongera', na huko kwenu ndio 'vichwa'! No matter hamuendelei...
 
Hii makala imeandikwa na Mwinyi Saddallah mtu ambaye siku zote anakua anapindisha kalamu yake pale habari inapohusu masilahi ya Zanzibar. Kwa sisi tuliokuwemo ndani ya Baraza na kuwashuhudia Wawakilishi jinsi walivyokua wakitoa michango yao tunawaona NYOTE ambao munachaongia mada hii ni dhaìri kumbe HAMUJUI MUNACHOKIHUBIRIA!
 
Hakika JUSSA anawakosesha usingizi waTanganyika na hata kumuona ni mwiba mkuu.

Hongera sana Jussa hakika wewe ni kichwa.
Mjibie swali aliloulizwa na Jaji Warioba kuhusu muungano uliofanikiwa kwa mikataba duniani!!
 
kwa ulelewa wake jaji anaona jusa hataki muungano...basi ndo hivyo hivyo hatuutaki hata kama hatuna hoja hatuna sababu hatuna mashiko lakini akili ya kumjua mbaya wetu tunayooo. Watanganyika mna roho mbaya kwa znz muungano hatuutakii hamjui kukataliwa ondoeni majeshi yenu tubaki na kinchi chetu.

Jusa hana mifano mm ninayo ya mkataba wa
eac
eu
kama ni udugu mahusiano haya yanatosha km hamtaki bas

yakhe lum, refer thread ya mwanakijiji kuhusu jinsi ya zanzibar inavyoweza kujitoa kwenye huu muungano bila mikwaruzo wala jasho. Waambieni wawakilishi wenu wapige kura ya maoni kukataa muungano barazani na wazenji wote walioko serikalini bara pamoja na wabunge wenu wasije bara, basi. Pia bilali, nahodha na mawaziri wote wazenji waliopo huku bara wafungashe virago warudi zenji. Hapo mtakuwa na nchi yenu iliyojaa asali na maziwa. Yoote haya anayoongea jusa ni kupoteza muda tu.
 
Natanguliza msimamo wangu (Declare interest).

1. SIUTAKI MUUNGANO WA SASA KWA SABABU NI WA WATU WAWILI NYERERE NA KARUME PAMOJA NA SERIKALI ZA SIKU HIYO.

2. KUIUWA TANGANYIKA KIMAGUMASHI NI KOSA NA NI ZIMWI LITAKALOPASUA CHUPA ILIYOLIFUNGIA

Nataka muungano unaokidhi matakwa ya wananchi. Uwe muungano wa dola mbili Tanganyika na Zanzibar siyo Tanzania Bara na Zanzibar kwa sababu hapajakuwepo dola inayoitwa Tanzania bara iliyoungana na Zanzibar

Mh. Warioba anasimamia hoja ya ulazima wa kuwepo muungano bila kujiuliza uhalali na uhalisi wa muungano kwa matakwa na maslahi ya wananchi wa pande mbili.

Jussa anaweza kuwa mbumbumbu kwa mtazamo wa wanaoulazimisha muungano. Hoja yake na hisia zake zinatuwakilisha wengi mimi nikiwa Mtanganyika. Kama mwana sheria jaji Warioba mvivu wa kutafsiri na kudadavua maana ya muungano wa mkataba. Anadai mifano ya miungano ya mkataba dunia mbona hatoi mfano wa muungano wa sasa tulio nao kama upo duniani?

Ni jukumu lake kuchukua maoni ya wananchi, si kutetea status quo.

Nakusahihisha usijumuishe waTanzania wote na hoja za watawala. Mimi najuta kuwa kwenye muungano huu na naumizwa sana na fikra za kipuuzi za watawala na wakala wao kwenye hili suala. Sababu ni moja tu sijaona manufaa yake zaidi ya matatizo, wala sioni tunakoelekea kuna heri.


Hata mwenyewe muungano uliopo siutaki lakini nataka kutofautiana na wewe kwenye red unaposema muungano ni wa watu wawili Nyerere Karume na serikali za wakati ule wanakuwa sio wawili tena.
Na hapo kwenye bluu wewe ulitaka Warioba atoe mifano ipi wakati umeshasema muungano tayari upo hapa Tanzania au Tanzania haipo duniani
 
Tatizo hapa mnakuwa mnashindanisha vichwa viwili tofauti. Cha awali ni kile chenye kusema ukweli na kusimamia haki na kile chenye unafiki na uroho wa madaraka na kupenda ukubwa.

Binafsi namfahamu sana Joseph Warioba tokea akiwa wizara ya sharia na naujua uwezo wake vilivyo sana. Naweza kusema ni mganga njaa tu kama angekuwa mtu makini asingeweza kukubali TUME hii kwani alishawahi kuongoza Tume ya Rushwa lakin mpaka leo ipo kwenye kabati na hata hii kama angekuwa mtu makini asingekubali kwani alikatazwa kuujadili muungano.

Kwa hayo tu unajuwa fika huyu ni mganga njaa na mpenda madaraka japo hana uwezo nayo. Je mnajuwa kuwa aliwahi kughushi kura huko kwao BUnda na ubunge wake ukateuliwa.

Naamini wazi Warioba huyu hana uwezo kabisa wa kushindana na kijana kama JUSSA. Namshangaa baba zima kama hili linatolewa kamasi na mapovu na mwanasharia wa juzi juzi tu.

Ushauri wangu kwa Warioba: kama umekosa asubuhi huwezi pata jioni. Hishma ni bora kuliko vyeo.

Mkuu hapa umenena, hawa wanaochangia wapo zaidi KIUTASHI. Laiti wangelimuona Warioba alivyotolewa makamasi na Jussa wasingépata uthubutu wa kuchangia hii mada!
 
Hata mwenyewe muungano uliopo siutaki lakini nataka kutofautiana na wewe kwenye red unaposema muungano ni wa watu wawili Nyerere Karume na serikali za wakati ule wanakuwa sio wawili tena.

Quantitavely (Kimahesabu) sina uhakika kama kama karume na nyerere wahesabiwa "pamoja na serikali zao". Mfano tu viongozi ni watu na serikali ni taasisi. Viongozi walivuka mipaka walipo amua kutowashirikisha wananchi wao na kushirikisha vyombo vya utawala wao sintokuwa pamoja nao. Hoja ya sasa ni kusahihisha upotoshaji huo. Wananchi washirikishwe siyo wabariki makusudio na matamanio yao kwa mgongo wa wananchi

Na hapo kwenye bluu wewe ulitaka Warioba atoe mifano ipi wakati umeshasema muungano tayari upo hapa Tanzania au Tanzania haipo duniani

Warioba ana mandate ya kusikiliza maoni siyo kutetea hali ya muungano uliyopo. Mbaya zaidi sina uhakika kama hakiuki maagizo ya Rahisi JK aliyetaka muungano usijadiliwe; mara CCM ikatoa maelekezo ya muungano wa serikali mbili. Yote ni kujikanganya na kujaribu kuhalalisha haramu.

Kifupi Tanzania iliyopo duniani ni magumashi, kwa sababu kama "muungano" wa hao marehemu unaitwa ni wa Tanganyika na Zanzibar ndiyo Tanzania. Tanganyika iko wapi hapa duniani kwa sasa? Nilizungumzia Tanzania bara ambayo haipo si Tanzania. Na Tanzania iliyopo inaundwa na Tanganyika na Zanzibar; kwa hiyo Tanzania inayoundwa na Tanzania Bara na Zanzibar ni magumashi haipo.

Nielimishe
 
Hawa jamaa wanajitoa ufahamu, they know that they need the union to survive, wanajua for sure. Kama "Watanganyika" na wabaya sana wanataka mkataba wa nini na watu wabaya? Kwa nini hawataki total separation tujue moja?
 
Mukitaka musitake zanzibar itatoka kwenye midomo ya wahafidhina
 
They have picked most of the ccm cronnies to be in the review process; they have also bribed them with a lot of money which will most likely give us an unacceptable document!!

Jaji Warioba amejibebebesha jukumu ambalo ni zito ambalo halimo katika majukumu alopangiwa.
Utaelewa ukipitia thread hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/294037-wawakilishi-jaji-warioba-katudanganya.html

Jaji Warioba ni mtu alichangia katika kiini macho cha muungano, kufuta neno Tanganyika na kuifanya Tanzania na baadae Tanzania bara. kuelewa hilo pitia hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/334649-tundu-lissu-na-kiini-macho-cha-muungano.html

Inawezekana Jaji Warioba alikubali kuongoza tume hii ya kukusanya maoni juu ya katiba akijua kuwa lengo la chama chake ni kufuta bara na visiwani; Tanzania bara, Tanzania visiwani ili lile lengo la kukamilisha mazingaombwe litimie kupata Tanzania.

Zanzibar wana katiba yao kwa hiyo wao ni wazi kilichowahusu katika kutoa maoni ya Katiba mpya ya JMT ni kuzungumzia Muungano na vile wanataka uwe. Na hilo lilijidhihirisha Tume ya Warioba ilipokumbana na changamoto hiyo huko Zanzibar. Ndipo Jaji Warioba alijipa madaraka ambayo hakupewa-(muungano ulisemwa ni off-limit isipokuwa kwa kuleta serikali moja(kuuimarisha zaidi)) na kuwataka watu watoe maoni juu ya Muungano pia.

Kwa wadanganyika, ukusanyaji huu wa maoni umeshajikita katika utanzania bara(utanganyika) na uzanzibari. Tunasahau kusemea kuhusu tume huru ya uchaguzi na vyombo vya ulinzi na usalama kuacha kuibeba CCM.

Kwa muelekeo huu Katiba mpya haitokuwa tayari ifikapo 2014. Kwa mwenye macho aone mtego wa CCM.
 
Mukitaka musitake zanzibar itatoka kwenye midomo ya wahafidhina

THIS IS NONESENSE MY BRODA....kama hamjui hata mwataka muungano wa aina gani ni bora mkajipanga upya zaidi ya kutoa kauli za dharau kama zako...nani ni muhafidhina kwa maana yako ya sentensi uliyoitoa?..BARA/TANGANYIKA? be smart ur big boi now.
 
Kwanza warioba yupo pale kutetea sera za ccm sio kukushana maoni mana hukasirika anaetoa maoni kinyume na chama chake au nchi yake tanganyika kwa kumuuliza maswali ya kiajabu akubali mwenye maoni tafauti na yeye na kila mmoja ana haki yake
 
Tena hayo hatujui ila ipo siku tutatoka kwenye midomo ya wahafidhina hii ni Nchi yetu ya Zanzibar na itabakia kua nchi yetu na tutaitetea hadi kufa kwetu
 
Back
Top Bottom