Jaji wa Marekani Aliyewalawiti Wafungwa Kufungwa Maisha

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082


3287242.jpg

Jaji Herman Thomas Thursday, October 08, 2009 12:24 AM
Jaji 'Basha' wa nchini Marekani ambaye alikuwa akiwamendea wafungwa wanaume na kuwalawiti baadhi yao ili awapunguzie adhabu zao huenda akahukumiwa kifungo cha maisha baada ya kupandishwa kizimbani. Jaji Herman Thomas, jaji ambaye alikuwa akiheshimika sana kiasi cha kwamba alikuwa akitabiriwa kuwa jaji mkuu wa kwanza mweusi wa Alabama Kusini, huenda akahukumiwa kwenda jela maisha baada ya kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuwalawiti wafungwa wanaume ili awapunguzie adhabu zao.

Jaji Thomas anakabiliwa na tuhuma za makosa 78 ya kukiuka misingi ya kutoa haki, kulawiti wafungwa, kuwateka wafungwa na kuwashambulia waliokataa kulawitiwa.

Jaji huyo mwenye umri wa miaka 48, alijitetea kwamba hakufanya kitendo hicho na kwamba alikuwa akikutana na wafungwa ili kuwapa miongozo bora.

Wakili wa jaji huyo alidai kwamba mteja wake amebabimbikiwa kesi hiyo na wafungwa ili kumchafulia jina lake kwa kazi nzuri ya ujaji aliyoifanya kwa miaka 20.

Jaji Thomas na wakili wake walidai kwamba kesi aliyofunguliwa ni njama za wanasiasa ambao hawapendi mafanikio yake.

Lakini mahakama iliambiwa kwamba Jaji Thomas alianza kufuatiliwa mienendo yake baada ya kuibadilisha hukumu ya binamu yake mwaka 2006 ingawa hukumu ya kesi hiyo ilikuwa imetolewa na jaji mwingine.

Mahakama iliambiwa pia kwamba jaji Thomas alizichukua kesi walizopewa majaji wengine bila ya kufuata taratibu husika.

Baadhi ya wafungwa wanaume walielezea jinsi walivyotolewa jela na kupelekwa kukutana na Thomas kwenye gari lake au ofisini kwake.

Awali kulikuwa na taarifa za wafungwa kuvuliwa nguo zao za ndani na kisha kuchapwa bakora halafu ndipo zilipojitokeza taarifa za kulawitiwa kwa wafungwa na wafungwa wengine kulazimishwa wajipigishe punyeto mbele yake.

Wafungwa wote waliolawitiwa na jaji huyo walikuwa ni wafungwa weusi hakukuwa na mfungwa mzungu kati yao.

Alama za bakora kwenye ****** ya baadhi ya wafungwa na pia alama ya majimaji ya mbegu za kiume za mfungwa aliyelazimishwa apige punyeto kwenye zulia la ofisi ya jaji huyo ni miongoni mwa vielelezo vya ushahidi dhidi ya jaji huyo.

Wafungwa waliotoa ushahidi waliweza kuelezea vizuri kabisa jinsi ilivyo ofisi ya jaji huyo ambayo haina madirisha.

Thomas alijiuzulu nafasi yake mwaka 2007 baada ya tuhuma za wafungwa kuchapwa bakora kwenye makalio yao kusambaa.

Waendesha mashtaka walisema kwamba kuna wafungwa 15 wapya na wa zamani ambao wako tayari kutoa ushahidi wa kulawitiwa na jaji huyo.

Ushahidi huo utachukua wiki kadhaa na jaji Thomas huenda akahukumiwa kifungo cha maisha iwapo atapatikana na hatia.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3287242&&Cat=2
 
Back
Top Bottom