JAJI wa MAHANGA hakuwa na jinsi...

CDM kwenye hili msimlaumu mtu hoja za mpendazoe zilikuwa dhaifu sana na hazina mashiko kama chama chenyewe kilivyo kibabaishaji na hoja za uzandiki

hoja zilikuwa imara sana, sema kitendo cha mihimili kuingiliana kinasababisha mhimili mmoja kuwa ndo kichwa na wengine mikia tu wanalazimika kufuata maamuzi ya mhimili mkuu.

Jaji anateuliwa na rais, hivyo anaweza kufanya lolote ili mradi alinde heshima ya bosi wake. Kwenye katiba ijayo, mihimili hii ienganishwe, na mtu kuwa jaji asiteuliwe, ikiwezekana apigiwe kura ili awajibike kwa wananchi.

au uundwe mfumo maalum wa namna ya kuwapata majaji na sio kuteuliwa na rais, kwani hawawi huru kabisa

Kesi hii tuondoe ushabiki mahanga hakusahili, mnajua kwa nini ameshinda?? Uuuuu..........niiiiii, yaani ni HATARI kuliko ukoma!
 
pia ni muislam kama ilivyo ccm

Mkuu sidhani kama dini ni kitu muhimu sana kwani Mahanga ni Mkristo. Kwamba hukumu ilikuwa na madhaifu twaweza kuthibitisha ila la dini laweza kuwa gumu kuthibitisha. Sidhani kama hili ni suala linalohitaji majibu mepesi kama ya udini mkuu.
 
hauna lolote kuweka ukabila mbele tu

Acha kukuru kakara msichana alichosema mtoa mada kina mantiki na kime play role kubwa sana kwa Mahanga kushinda la sivyo ingekuwa jaji ni neutral tungekuwa tunaongea mengine.
 
Jaji Profesa Ibrahim Hamis Juma alikuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria-Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Aliishia mwaka 2006,akimpisha Prof.Sifuni Ernest Mchome ambaye kwasasa yuko TCU.Jaji Juma ni rafiki wa karibu wa Rais Jakaya Kikwete.Ni Mkurya kama alivyo Mahanga.Jaji Juma alianza kuteuliwa,na Rais, kwenye Kamati ya Uchunguzi wa Mauaji ya Wafanyabiashara watatu,yale ya Zombe,iliyokuwa chini ya Uenyekiti wa Jaji Kipenka Mussa.

Baadaye,mwaka 2008,akateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.Jaji Juma ni mtu wa msimamo.Ni mtu makini.Msimamo wake na umakini wake umemezwa na uhusiano wake wa karibu na Rais na ukabila wake na Mahanga.Hukumu ya leo haikushtua.Ameamua kadiri ya urefu wa kamba yake...

tunaomba muipost hiyo hukumu ili tuweze kuipitia
 
Jaji kuteuliwa na rais haifanyi Jaji asiwe huru, unless huyo jaji ni kichwa maji, hajiamini na hajasoma!

Mbona Utouh anateuliwa na rais na anaibua ma issue kila siku?

Swala sio anateuliwa na nani bali ni mfumo gani mzuri wa kuweka ili wafanye kazi bila woga.
 
itategemeana na jopo na hao wenye nyekundu wakichaguliwa kati yao hilo jopo siyo jema kwa Mpendazoe........

Duh! Sijawahi kuona pumba kama hizi!

Mimi siku zote najua nipo kwenye jukwaa la ma great thinkers! I was so damn wrong!
 
Hahahaaaaa waacheni wafu wawazike wafu wenzao. Kwenye hii kesi CDM haikumpa ushirikiano wakutosha Mpendazoe baada yakuona hoja zao hazina nguvu, wakamuacha peke yake katikati ya bahari ajifie mwenyewe. Na leo ndio kufa kwenyewe kwa Mpendazoe, hoja zake zilikuwa dhaifu sana sana.

wewe hujui unacho kisema,mimi nilikuwepo mwanzo mpaka mwisho yaani leo,Jaji alicho kifanya nikitu tofauti na unachokitetea wewe. Mfano ,jaji wakati anapitia maelezo ya mashahidi ya shahidi Rugema aliyekuwa shahidi wa 5 JAJI "shahidi rugema alisema yeye aliomba polisi wampe mfuko ambao yeye Rugema aliukagua na kukuta mihuri ya tumeya uchaguzi" lakini ukweli shahidi yule wakati anatoa maelazo hakusema hivyo kabisa! yeye alisema kuwa mfuko ule ulidondoka wenyewe bna kupasuka na mihuri kusambaa na ulirudia kusema hivyo mara 6na ukichanganya naile ya kuongozwa na wakili wake mara 2 zinakuwa mara 8, lakini jaji aliye na harufu ya STATE anasema kitu kingine. Huyo jaji sio wakutetea kabisa!!!.
 
Jaji kuteuliwa na rais haifanyi Jaji asiwe huru, unless huyo jaji ni kichwa maji, hajiamini na hajasoma!

Mbona Utouh anateuliwa na rais na anaibua ma issue kila siku?

Swala sio anateuliwa na nani bali ni mfumo gani mzuri wa kuweka ili wafanye kazi bila woga.
ndo maana nchi haiendelei, kama huyu ndiye mtanzania anayeitaji katiba mpya tumekwisha, ikawa asubuh ikawa jioni siku ya pili.
 
Jaji Profesa Ibrahim Hamis Juma alikuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria-Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Aliishia mwaka 2006,akimpisha Prof.Sifuni Ernest Mchome ambaye kwasasa yuko TCU.Jaji Juma ni rafiki wa karibu wa Rais Jakaya Kikwete.Ni Mkurya kama alivyo Mahanga.Jaji Juma alianza kuteuliwa,na Rais, kwenye Kamati ya Uchunguzi wa Mauaji ya Wafanyabiashara watatu,yale ya Zombe,iliyokuwa chini ya Uenyekiti wa Jaji Kipenka Mussa.

Baadaye,mwaka 2008,akateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.Jaji Juma ni mtu wa msimamo.Ni mtu makini.Msimamo wake na umakini wake umemezwa na uhusiano wake wa karibu na Rais na ukabila wake na Mahanga.Hukumu ya leo haikushtua.Ameamua kadiri ya urefu wa kamba yake...

Makongoro si Mkuria. Makongoro ni Mjaluo aliyetokea Kisumu wakahamia Bunda miaka hiyo ya zamani. Jina lake alijaribu kuilatinize ili asijulikane kuwa ni mjaluo. Jina lake la Kijaluo ni Mahanga Ongoro. Kuhusu hukumu nafikiri haki imetendeka na watu humu JF walishaanza kubashiri kuwa atashinda tu.
 
hukumu tayari. Way forward ni walioshindwa kesi kuamua kama wanakata rufaa ambayo iko wazi na ama wanajiandaa miaka mitatu kuweza kujaribu tena.Maisha lazima yaendelee kwa njia yoyote.Kinachosikitisha JF niliyoiheshimu imegeuka eneo la mapambano ya mtu kwa mtu au CCM dhidi ya CDM au Dini A dhidi ya B ambavyo naamini siyo maono ya JF wala siyo ustaarabu.Matusi ya mtu kwa mtu yanawafaa walevi kwa wakati wamelewa tu,kabla hayafai.
Kuna tatizo kubwa sana kwenye Mahakama zetu nchini hata hivyo kwa sababu JAJI anapoteuliwa na RAIS hakuna vetting huru anayofanyiwa tofauti na ilivyo Kenya,kiasi kwamba UHURU wa Mahakama zetu na hususan wa Mahakimu na Majaji wetu UNAHOJIKA.Sasa way forward ni kupigana KATIBA MPYA iweke mamlaka huru za kupembua wateule wa RAIS kama USA na Kenya na kwingineko.
 
Back
Top Bottom