Jaji Mkuu Kushiriki Hukumu ya Lema

Historia inaonyesha kwamba kwenye shauri ambalo jaji mkuu ni mwanajopo hukumu itafurahisha upande wa serikali

Kama ilivyokuwa kwenye shauri la mgombea binafsi lililofunguliwa na Mtikila
 
tunaomba haki itendeke ili huyu jaji aonekane anafanya kazi akifanya ujinga itakula kwake atajipaka matope mbele ya wananchi
 
mingoi kwa lugha yetu ni mwanamke mwenye waume wengi sanaaaaaa

Viva kamanda lema

V
SENGEREMA

Lugha gongana!kwetu ni mwamaume rijali mpenda masaburi.Mi ninajivunia tasfiri ya kwetu we tupia na la kwenu tena utapenda mwanangu mwenyewe.
 
Majaji wakuu hawajawahi mwangusha Rais aliyewateua kwa hiyo tusitegemee Chande kufanya miujiza zaidi ya kuikazia hukumu. Ninachoona hapa ni kuwa Lema hatashinda hii kesi kwani JK ameamua kuisimamia mwenye we haswa ukizingatia Othman ni Mwinyi na Lema ni dini tofauti
 
Wale waliokuwa na KIkwete kikazi,kifamilia,Jeshini wametuthibitishia kuwa ni mtu mwenye visasi na mwenye roho ya ukatili tumeona sasa wote wanaompinga anawaua kama Daudi Mwangosi,Dr Ulimboka,Mwakyembe,Prof Mwaikusa,Prof Mwandosya
Jaji Chande ni ndungu na zoka wa damu moja yaani wamezaliwa tumbo moja na zoka hana sudi nzuri na chadema
ukweli Lema aendelee na M4C kwa sababu chande asingechukua kesi ndogo kama hii anaenda kukaza hukumu tuu bila aibu akitekeleza mapenzi ya aliyekwenda kumsakanyua huko East timo alikuja hapa na utapiamlo unamuonaje sasa anameremeta
 
Wakuu wala msitegemee tofauti zaidi ya maudhi,si ajabu ukasikia shauri hili lipelekwe bungeni likajadiliwe zaidi.Mm naona turudie tuwapige 9 kwa 0,Arusha3,Sumbawanga3,Igunga3 ili wakalale
 

na Grace Macha, Arusha

JAJI Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, ataungana na majaji wa Mahakama ya Rufaa, Natalia Kimaro na Salum Massati, kusikiliza rufaa ya kupinga kuvuliwa ubunge ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), akichukua nafasi ya Jaji Mbarouk Salim Mbarouk.


Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya mahakama hiyo iliyosainiwa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Malewo, ambayo imebandikwa kwenye ubao wa matangazo inaonyesha kuwa mabadiliko hayo yataanza Septemba 20, mpaka mwisho wa vikao hivyo Oktoba mosi mwaka huu.

Kwa upande wake, wakili wa Lema, Method Kimomogoro, alisema atashirikiana na wakili mwenzake Tundu Lissu katika shauri hilo litakalosikilizwa kwa siku moja na kupangiwa tarehe ya kusomwa hukumu, aliongeza kuwa tayari alishaitaarifu mahakama juu ya suala hilo tokea Agosti 28, mwaka huu.


Uamuzi huo wa Lissu kumwakilisha Lema kwenye shauri hilo utamkutanisha mahakamani hapo na kaka yake, Wakili, Alute Mughwai anayewawakilisha wanachama watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel, na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililopelekea kutenguliwa kwa ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni mbunge huyo alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian, kwa kutumia lugha ya matusi.


Awali Lema kupitia wakili wake, Kimomogoro, aliwasilisha kwenye mahakama hiyo hoja 18 za madai akipinga kutenguliwa kwa ubunge wake na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu.


Kwenye baadhi ya madai hayo, Lema aliiomba Mahakama ya Rufaa kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu, uliotengua ubunge wake, huku akiitaka imtangaze kuwa mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini.


Aidha, aliitaka mahakama hiyo ya juu, iwaamuru walalamikiwa katika shauri hilo walipe gharama za rufaa hiyo pamoja na zile za kesi iliyomalizika kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.


Katika madai mengine, Lema anamlalamikia, Jaji Gabriel Rwakibarila, aliyesikiliza kesi hiyo kuwa alitoa uamuzi wake kwa kuzingatia maneno ya uvumi, huku akipuuza ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.


Lema anadai kuwa jaji alikosea wakati alipoamua kuwa mpiga kura yeyote anaruhusiwa kupinga matokeo ya uchaguzi hata kama haki zake za msingi hazijaguswa.

 
oh ooooooh JAJI Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman aingia... yeye ni CCM

Yeye ni Mzanzibari hivi atapewa kitambulisho cha WAGENI? na Sio cha WATANGANYIKA??? Kama Z'Bar wanawafanyia waBara?
 
Tundu Lissu VS Alute Simon Lissu Mughwai (kaka yake mkubwa),,kama Movie vile, kazz kwel kwel,,
 
kamanda lisu ni nomaaaaaaaaaaaaaaaa.jamani hakuna kitu kizur sana kama kusoma hasa sheria cheki lisu mambo anayofanya very profeshino ,BRAVO,BRAVO LISU,BRAVO CDM
 







jaji%20chande.jpg

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, atakuwa miongoni mwa jopo la majaji wa Mahakama ya Rufani watakaosikiliza rufani ya aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema.

Jaji Chande atashirikiana na majaji wengine wa mahakama hiyo, Natalia Kimaro na Salum Massati kusikiliza rufani hiyo namba 47/2012 ya mwaka 2012.

Orodha ya awali ilionyesha kuwa rufani hiyo ya Lema kupinga kutenguliwa kwa matokeo ya uchaguzi wa ubunge katika uchaguzi wa mwaka 2010, ingesikilizwa na Jaji Mbarouk Salim Mbarouk, Jaji Kimaro na Jaji Salum Massati.

Hata hivyo, ratiba mpya inaonyesha kuwa Jaji Mkuu Chande, amechukua nafasi ya Jaji Mbarouk.

NIPASHE imeshuhudia ratiba ya vikao vya mahakama hiyo iliyosainiwa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Maxmillian Malewo, ambayo imebandikwa kwenye ubao wa matangazo.

Hata hivyo, haikufahamika ni sababu zipi zimesababishwa kuondolewa kwa Jaji Mbarouk katika orodha ya majaji wa kusikiliza rufani hiyo. Hakuna ofisa yeyote katika ofisi ya Msajili aliyekuwa tayari kuzungumzia suala hilo.

Rufani hiyo inatarajiwa kusikilizwa Septemba 20, mwaka huu na baadaye kupangiwa siku ya kusomwa kwa hukumu.

Wakili wa Lema, Method Kimomogoro, alisema kuwa atashirikiana na Mkurugenzi wa Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa Chadema, Tundu Lissu katika shauri hilo.

Kimomogolo alisema badiliko hilo la kuongezeka Tundu Lissu, tayari ameshaitaarifu Mahakama tangu Agosti 28, mwaka huu.

Lema, aliandika madai 18 na kuyawasilisha Mahakama ya Rufaa baada ya kutenguliwa ubunge wake Aprili 5, mwaka huu.

Lema katika hoja zake, anaiomba Mahakama ya Rufaa kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu uliomtengua ubunge wake.

Pia anaiomba Mahakama ya Rufaa kumtangaza kuwa mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini pamoja na kuamuru walalamikiwa katika kesi hiyo walipe gharama za rufaa hiyo na kesi ya Mahakama Kuu.

Kadhalika, Lema anamlalamikia Jaji Gabriel Rwakibarila, wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, aliyesikiliza kesi hiyo kwamba hakutoa hukumu kwa kuzingatia ushahidi halisi uliotolewa mahakamani, bali alifanyia kazi uvumi.

Hoja nyingine ya Lema ni kwamba Jaji Rwakibarila alikosea kuamuru mpiga kura yeyote kuruhusiwa kupinga matokeo ya uchaguzi hata kama haki zake za msingi hazijaguswa.

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilitengua ubunge wa Lema katika kesi ya kupinga matokeo yake iliyofunguliwa mahakamani hapo na walalamikaji hao ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Shauri lililopewa namba 13/2010, lilifunguliwa na walalamikaji hao wakipinga matokeo hayo na kudai kuwa Lema alikiuka kanuni, maadili, taratibu na sheria za uchaguzi na kesi hiyo kusikilizwa na Jaji Rwakibarila ambaye ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga.

Jaji Rwakibarila aliteuliwa kusikiliza kesi hiyo iliyovuta watu wengi kufuatia Jaji Aloyce Mujulizi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kujitoa, baada ya upande wa walalamikaji kumkataa kwa maelezo kuwa haukuwa na imani naye.

Katika shauri hilo, walalamikaji walidai kuwa Lema wakati wa kampeni zake alitoa lugha za matusi, kashfa na udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya aliyekuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo kupitia CCM, Dk. Batilda Burian katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Katika hukumu yake, Jaji Rwakibarila alisema amebaini kuwa katika mikutano 60 ya kampeni za uchaguzi huo, mikutano minane iligundulika kuwa Lema alikiuka maadili ya kampeni za uchaguzi.

Jaji Rwakibarila alisema Mahakama imebatilisha matokeo ya ubunge wa Lema kutokana na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo.

Alisema madai hayo pamoja na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, Mahakama imeridhika kwa kuwa Lema alikiuka sheria na vifungu vyake vinavyokataza kufanya kampeni kwa misingi ya ubaguzi wa kidini, ujinsia na kikabila, hivyo kwa misingi hiyo Mahakama inatengua matokeo ya uchaguzi wa ubunge wake kama walivyokuwa wameomba walalamikaji.

Jaji huyo pia alimwamuru Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, George Hurbert, kupeleka nakala ya hukumu ya kesi hiyo katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa hatua inayofuata.

Lema alikuwa akitetewa na Method Kimomogoro wakati wadai wakiwakilishwa na mawakili wawili, Alute Mungwai na Modest Akida, huku upande wa serikali ukitetewa na Timon Vitalis na Juma Masanja.




CHANZO: NIPASHE


 
Haya sasa tunasubiri tuone namna mahakama inavyoweza kuwatendea haki wote. Mimi si mwana sheria ila navutiwa sana na hii rufani niweze kona mwisho wake na jinsi haki inavyotolewa kwa wote (lema na mdai wake) kwa kusheza na sheria.
 
Mbona sijaelewa hapo kwamba itasikilizwa tarehe 20 sept. na kisha kupangiwa siku ya hukumu! Ina maana inasikilizwa siku moja tu basi?

Hiyo Bench naiona iko makini sijui Lissu ana maoni gani katika hao majaji manake makala yake ileee ya kujitetea bungeni ikiwachana baadhi ya majaji.
 
hapo inabidi sheria + busara vyote vitumike katika kutoa uamuzi........mambo ya siasa yana taabu sana yakiingia kwenye sheria
 
Chadema watashind kesi kama haki ikitendeka kwani yule voda vasta aliyehukumu kesi ya arusha anajua madudu aliyofanyafa.....kwamimi binafsi hukumu tayari ninayo,nasubiri tu uthibitisho kuona lema anarudishiwa ubunge wake na kama alitukana basi adhibiwe kwa style nyingine lakini sio kupora uwakilishi wa wana wa nchi.....aliyestahili kupolwa ni dalali kafumu na makongoro mahanga
 
Back
Top Bottom