Jaji mkuu chande; mahakama itatumia simu na internet kuendesha kesi zake

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
MWENENDO WA KESI KUENDESHWA KWA NJIA YA SIMU NA INTERENETI.
Wakuu,
Kuna taarifa ktk gazeti la Mwanahalisi kuwa Mahakama itaanza kutumia simu na mtandao wa interneti kuwasiliana na wateja wao ( washtaki na washtakiwa)
Hayo yalisemwa na Jaji mkuu wa Tanzania Othman Chande wakati wa hafla ya kuapishwa kwam majaji 10 walioteuliwa na Rais JK.
Namnukuu, serikali imejipanga kuboresha mfumo wa mahakama hasa ktk usikilizwaji wa mashauri kwa kuboresha mfumo wa kurekodi mwenendo wa mashauri hayo. Ktk uboreshaji huo pia mahakama inatrajia kutambulisha huduma mpya ya taarifa kwa njia ya simu, ambapo wananchi wenye kesi mahakamani watapafa fursa ya kutambua/kufahamu mienedo ya kesi zao kupitia simu za mikononi, alsema Jaji Othman.
Mfumo huo pia utanenda sambamba na mfumo wa internet ambapo nakala za mashauri yaliyotolewa mahakamani yatawekwa humo mtandaoni.
My take,
Mimi naona kama ni hatua nzuri ya kupunguza mrundikano wa watu mahakamani.
 
ni hatua nzuri na ilishaanza kitambo ktk mahakama ya biashara na pia wana website yao
lakini je mahakama yenyewe imebadilika ktk kutumia mfumo wa sheria za zamani ambazo zinachangia kwa
kiasi kikubwa uchelewashaji wa kesi? kama sivo hata wakitumia internet wkt sheria ni zile zile haitasaidia
kesi kuwahishwa kusikilizwa mapema
pili wamewasomesha watumishi wangapi ICT kama mahakimu na majaji ili kukabiliana
na matumizi ya teknolojia ya kisasa?
mahakama zina computer ngapi huko mikoani na vijijini?
nyingi bado zinatumia typewritter
ni wazi nyingi hazina computer
wala mitandao ya internet na fungu linalotengwa kwa ajili ya mahakama ni dogo
sana. nina mashaka na utekelezwaji wa hili azimio la jaji mkuu
kwa wakati huu.
 
Back
Top Bottom