'Jaji' Mbarouk Salim Mbarouk awekewe pingamizi na Godbless Lema.

Khakha

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
2,982
1,009
wakuu JF,

Kufuatana na taarifa zilizoko bungeni kuwa Mbarouk S Mbarouk hana sifa za ujaji, nimeonelea ni muda muafaka kwa kamanda Lema kumwekea kipingamizi kwenye shauri lake la rufaa mjini Arusha tarehe 20 sept.

Sababu ni kwamba hajakidhi vigezo vya kuwa jaji hata wa mahakama kuu as per constitution. Au km anajiona guilty ajitoe tu akamalizie llb yake kwa prof. Mbwete.

nawasilisha
 
Ni mara chache sana mtu anayempinga hakimu au jaji mwisho wa siku akashinda kesi. Hapa Lema nahisi anatukosesha ushindi hapa. Akumbuke alipomkataa Jaji Arusha na pia Kafumu alipomkataa jaji tabora matokeo yake ilikuwa nini. Ni mtazamo wangu tu
 
mwana mpotevu hiyo ni haki ya kila mtu na usipokuwa na imani na jaji kwa nn huishi kwa mashska hyo ni haki ya kila mtu kikatiba na kama kweli jaji hana vigezo ya nini kuendelea kusikiliza kesi?
hapo ni haki yake kukataa rufaa hata akishindwa arusha ss hatuna tatizo na hilo mbona hata jiwe litapita kaka?

Lema hana sababu ya kumkataa huyo jaji kilaza kwani katika jopo lao wako watatu na hao wengine wawili ni majaji mahili; hakuna sababu ya kumkataa muacheni kwani mpaka sasa nadhani amekwisha fedheheka!!
 
Kwa waliosoma sheria, huyu Jaji Mbarouk ndio mnamsikia leo? Huyu mzee ni Jaji tangu utawala wa Mwinyi i guess, na he holds an advanced deploma in law (an equivalent to LL.B) by that time of course, ndio sifa iliyofanya apewe ujaji tangu miaka hiyo ya 80. Ametoa hukumu nyingi sana! Na ni jaji aliyemakini.

My take, hapa siasa imeingilia profession. Tuache ushabiki usio na tija.

Kwenye ukweli tukubali kuwa ni kweli, na tusipotoshe.
 
Ulichoandika chote kimeharibiwa na maneno 'I guess'. Inawezekana vyoote vingine ume-guess pia. Maswali ni je, kweli anasoma LL.B ya OUT? Kama ni kweli, kwa nini? Kuwa judge isitoshe ku-justify kuwa aliisoma sheria...pengine ni mwendo wa kupeana. Tupe uhakika mkuu.
 
Back
Top Bottom