Jaji Kiongozi aibipu Serikali.. tena.!

Tunampongeza Jaji lakini tutampongeza sana hayo aliyoyasema yakianza kutekelezwa tukiwaona wanaosota magerezani kwa miaka mingi wanaachiwa huru.

Huu ni mwaka wa uchaguzi, haiyumkiniki watakaoachiwa huru kwa uamuzi huo wataishukuru Serikali ya CCM ...!


Mkuu Boramaisha,

Tabia yetu ya kufanya kila jambo ni Siasa inatupa shida sana...lakini wenye matatizo ni sisi wenyewe kama ambavyo hapo juu umeonyesha dhahiri. Sasa ili tukunufaishe wewe na wengine wenye mawzo kama yako; tusiwaachie hao wenzetu huru mwaka huu kwa sababu wataisifi CCM..!!!!
 
Tatizo la utendaji ndani ya nchi yetu ni mfumo. Mfano mfumo wetu wa kimahakama una kasoro kubwa katika uendeshaji kesi. Police ndie mtuhumu, mkamataji, mwendesha mashtaka na hata kesi nyingine wanafanya ruling. Mfumo huu umempa police mamlaka kubwa iliyopelekea urasimu mwingi. Majaji ukiwafuatilia kwa makini utagundua kuwa wanaifuata sana haki ila tatizo ni kwa mahakimu na mapolisi. Binafsi napendekeza kama watu wamekaa remand mda mrefu kwa kisingizio cha ushahidi kutokukamilika basi kama ikithibitika kutenda kosa, kifungo atakachofungwa kijumuishe mda aliokaa ndani tangu siku ya kukamatwa kwake. Na kama ikithibitika hana kosa serikali inapaswa kumlipa fidia ya mda wake wote alioshikiliwa.
 
Nimetembelea ndani ya magereza nimegundua watu wengi wanaendelea kukaa magerezani kutokana na upelelezi wa kesi zao kutokamilika, huu sio utaratibu wa kutenda haki,huyu mtu atakaa gerezani kwa miaka mingapi ili upelelezi ukamilike?"alihoji Jaji Jundu.[FONT=ArialMT, sans-serif].[/FONT]

I hate this statement kwamba mpaka mtu atembelee ndio anajua... yaani kwenye mfumo wetu wa utawala huwezi kuwa na hizo information kwenye desk lako mpaka kila mtu atembelee sasa kwani siuta-staafu kabla kuwatemblea magereza yote... kwa hiyo hayo magereza mengine je... please do not take us like kids.
 
Hili liinchi bwana, wakati wa kesi ya Dito walianza kugoma na wakafikia kwenye hali nzuri kidogo lakini inavyoonekana wamerudi kule kule walikoanzia.

MM Mwanakijiji unasema uchunguzi uchukue mwaka mzima huoni kwamba kama mtu hana hatia kukaa rumande kutampotezea zaidi ya miaka 10 ya maisha yake? Uchunguzi usizidi mwezi moja ukichunguza kesi nyingi zinaairishwa kutokana na sababu ambazo hazina msingi wowote ni upuuzi tu.. Fweza zipo zinaliwa na mafisadi kuna sababu za kutosha kuajiri wafanyakazi zaidi kwenye hii secta ili kuliondoa hili tatizo.
 
I hate this statement kwamba mpaka mtu atembelee ndio anajua... yaani kwenye mfumo wetu wa utawala huwezi kuwa na hizo information kwenye desk lako mpaka kila mtu atembelee sasa kwani siuta-staafu kabla kuwatemblea magereza yote... kwa hiyo hayo magereza mengine je... please do not take us like kids.


Si kweli kwamba mtu akisema ametembelea magereza inamaanisha hajapata tarifa mezani. Kwangu mimi, nikisikia mtu kama huyu ametembelea magereza naweza kufikiri kwamba amepata taarifa mezani, lakini kwa sababu ni mtu mwenye kutaka kufanya due diligence, kuhakikisha, asiyependa umangimeza wa kutoa orders ofisini wakati haelewi kinachoendelea in the field.

Kwa msingi huu, mimi naona jambo la Jaji Mkuu kutembelea magereza ili kuhakikisha na kupata live examples ni swala la kupongezwa na kupigiwa mfano, na wala si la kushutumiwa.

Nisingependa Jaji Mkuu atoe maamuzi ya kimangimeza bila kufanya uchunguzi, tena nimefurahi kuona Jaji Mkuu anafanya ziara yeye mwenyewe bila kutegemea taarifa za wasaidizi ambazo mara nyingine hujaa habari zisizo sahihi.
 
nadhani mahakama ianze kutumia hiyo sheria na kuwafungulia watu.. ili serikakli iamke.. na kuachana na hizi dana dana.. si unaona hata walijaribu kutumia kwenye kesi ya mgombea binafsi?
Tatizo la section 225 ( discharge na siyo acquital) mshtakiwa akiachiwa anaweza kukamatwa tena hapo hapo ( nje ya mahakama) na mchezo ukaanza tena upyaaa!
 
I posted this information for archiving in 2008. Originally I posted it to one government website that was purpoted to be collecting people's opinions.

I repost it here again:
Tuesday, January 15, 2008

Ikumbukwe tu ilishasemwa…

[FONT=verdana,geneva]Wizara [inayohusika na sheria na katiba] itoe Waraka wa Serikali wa Kuongeza kanuni zifuatazo kwenye uendeshaji wa Kesi za Jinai na za Madai:[/FONT]​
[FONT=verdana,geneva]1. Kabla ya Kumtia Hatiani Mshtakiwa Yoyote, akabidhiwe nakala ya Mwenendo wa Kesi. Kabla ya Kutolewa Hukumu yoyote, Mshtakiwa apewe nakala ya Mwenendo wa Kesi.[/FONT]​
[FONT=verdana,geneva]2. Hukumu inapotolewa kwa Kesi yoyote, Mshtakiwa apewe PAPO HAPO nakala ya Hukumu. Kwa mshitakiwa asiyeona, mwenendo wa Kesi, pamoja na Hukumu viwe kwa maandishi maalum ya wasioona.[/FONT]​
[FONT=verdana,geneva]3. Kama Mshitakiwa atatiwa hatiani pasipo kupewa nakala ya mwenendo wa Kesi KABLA ya kutiwa hatiani, hatia hiyo isitambuliwe kisheria.[/FONT]​
[FONT=verdana,geneva]4. Kama mshtakiwa yoyote atahukumiwa pasipo kukabidhiwa nakala ya Hukumu PAPO HAPO, basi Hukumu hiyo ihesabiwe kuwa ni batili, isipokuwa pale mtu anaposhitakiwa pasipo kuwepo Mahakamani, ambapo itamlazimu Mtoa Hukumu kuiweka Nakala ya Hukumu hiyo tayari.[/FONT]​
[FONT=verdana,geneva]5. Muda wa Mahabusu uhesabiwe kwenye kifungo [Mahabusi zina hali mbaya zaidi kuliko hata magereza!, au, Mahabusu wana hali mbaya zaidi kuliko Wafungwa!] Mtu anayekaa Mahabusu kwa Muda unaofikia Kiwango cha Chini cha Adhabu, Aachiliwe Huru, na kesi yake ifutwe. Mtu anayekaa mahabusu Miaka Kadhaa, Halafu akahukumiwa kwenda Jela Miaka Kadhaa+Miaka Kadha wa Kadha, basi atakaa jela Miaka Kadha wa Kadha tu, kwa vile ashakaa Mahabusu miaka kadhaa.[/FONT]​
[FONT=verdana,geneva]6. Kwa kosa lolote lenye adhabu ya Kifungo cha zaidi ya Miaka Mitano (5), Rufaa iwe ni \'automatic\' - Mshitakiwa hahitaji kufanya lolote ili kesi yake iangaliwe na Mahakama ya Juu zaidi… Labda kama Mshitakiwa mwenyewe atasema bayana hataki Rufaa. [Ufaransa ni moja ya nchi zifanyazo hivyo][/FONT]​
[FONT=verdana,geneva]7. Kanuni ya Adhabu itamke kwamba "Kifungo cha Maisha" maana yake ni "Miaka 15 Jela". Adhabu zote zinazozidi Miaka 15 zipunguzwe na kuwa kuwa "Kifungo cha Maisha" au, vizuri zaidi, cha chini ya hapo. [Sweden hufanya hivi pia][/FONT]​
[FONT=verdana,geneva]8. Pawepo na "Automatic Parole" kwa vifungo. Labda tuseme 60% ya kifungo itakuwa gerezani, na 40% itakuwa ya "parole", labda isipokuwa mfungwa atakuwa anatumikia pia adhabu nyingine muda huo wa 'parole'.[/FONT]​
[FONT=verdana,geneva]"Ukitaka kujua watu ni binadamu kiasi gani, tembelea magereza yao!" - Nukuu[/FONT]
 
Katiba ya Marekani iko against kitu wanaita "Double Jeopardy".

Yaani hairuhusiwi kumshtaki mtu mara mbili kwa shitaka lilelile.

Kwa hiyo ndio maana utakuta polisi / waendesha mashitaka wa huku wanatumia akili nyingi na maarifa tele kupeleleza na kuandaa mashitaka.

Kwa mfano, mtu ukikutwa na mali ya wizi, lakini yule aliyeibiwa aliuawa; watakushitaki kwa kosa linalohusiana na mali ya wizi, mpaka wapate ushahidi wa kuwa ulihusika pia na mauaji. Kwa vile wakikupeleka mahakamani kwa mauaji bila ushahidi, kesi ikatupwa, hawawezi kukushitaki mara nyingine, maana hiyo itakuwa "double jeopardy".

Kwetu kama ndio ulikuwa mtu wa mwisho kuonekana na marehemu, basi ujue ndio maisha yako "yataozea" jela. Ukikutwa unatembea mitaani usiku wa manane, washtakiwa kwa mashtaka ya wizi, au 'uzembe na uzururaji'.

Kwa ufupi bado tunaigiza mfumo wa sheria na haki. We are not serious.

Mlenge
 
tatizo kila mtu anajua kuongea linapokuja swala la utekelezaji ndo inakuwa kazi!
 
Binafsi sina ufahamu mkubwa wa mambo ya sheria na mahakama,lakini kwa mujibu wa habari hii je tatizo ni SERIKALI au MAHAKAMA?Maana kama suala lingekuwa ni kuhusu serikali basi Jaji Kiongozi asingewashauri mahakimu "kutumia busara" bali angeishauri serikali.Hivi huyu mheshimiwa Jaji Kiongozi angekuwa anatafsiri kauli zake kwa vitendo,hao mahakimu wanaofinya haki za watuhumiwa si wangashapata mwamko wa namna flani?

Na japo anachozungumza kina maana kubwa,napatwa na wasiwasi katika mifano hai aliyotoa hususan huo wa mwanamke aliyefungwa kwa kosa la deni.Mbona hatuelezwi hatma ya hakimu aliyetenda miscarriage hiyo ya justice?

Kaulizi nzuri pasipo matendo thabiti haziwezi kubadili mwenendo mbaya wa mambo katika jamii yetu.
 
Mkuu Boramaisha,

Tabia yetu ya kufanya kila jambo ni Siasa inatupa shida sana...lakini wenye matatizo ni sisi wenyewe kama ambavyo hapo juu umeonyesha dhahiri. Sasa ili tukunufaishe wewe na wengine wenye mawzo kama yako; tusiwaachie hao wenzetu huru mwaka huu kwa sababu wataisifi CCM..!!!!

Ninakupata vyema kwa nguvu ya mia. You got me all wrong buddy. I did not say watu wasiachiwe huru. Nimempongeza Jaji kwa mawazo yake mazuri. Nilichofanya ni kutoa angalizo kwamba wapo watakaoitumia hii habari njema ya kazi nzuri ya Jaji Kiongozi kwa manufaa yao kisiasa . Sintoshangaa wakati wa kampeni akatokea kiongozi wa CCM na kusema alichokifanya Jaji ni kutimiza ahadi za Chama Tawala kwa wananchi. And mind you, hili ni "Jukwaa la Siasa".
 
Back
Top Bottom