Jaji kesi ya Lema Arusha kashikishwa kitu na mafisadi?

Nimesema mahali pengine watu mnawapa credit sana ccm kiasi kwamba hata kutishia hawajaribu tena wanahitaji kurusha majina mawili matatu na watu wanakuwa wanyonge ghafla. Lema anaendelea kuwa mbunge kesho hakuna cha Lowassa wala shemeji yake Lowassa. Anayetaka kusherehekea aanze tu sasa.

Acheni kuwapa ujiko hivyo!

Nakukubali sana MMKJ.. Ni kweli watu wanaweweseka sana wakisikia CCM na hii inatokana na kuwa CCM wamekuwa na hila muda wote na imetokea kuwa wamekuwa wanafanikiwa mara nyingi kwa kutumia hizo hila na mbinu zao mbali mbali kiasi cha kuwaaminisha wengi kuwa jamaa wakitaka kitu wanaweza na wanapata ukizingatia kuwa wana dola.

Lakini watu wanatakiwa watambue kuwa wakiamua hayo yasitokee inawezekana kwani ni juzi tuu tumeona sauti ya umma ikiamua basi CCM haina uwezo wa kubadilisha matokeo. Au mnafikiri hawa jamaa hawana akili ya kuona hali ilivyo ? Mnafikiri hawakujaribu kutumia mbinu zao na hila zao chafu na mbaya za kila siku huko Arumeru Mashariki? Je waliweza?

Basi kuanzia leo tunatakiwa tujiaminishe kuwa tukiamua hakuna linaloshindikana. I mean UMMA wa Watanzania ukiamua basi CCM imekwenda na maji kwa kasi ya ajabu.

YES we CAN...
 
Jamani jambo kama hili likitokea nebulous tulibebe kitaifa! Tufanye maandamano ya Taiga Mzima tusiwaachie Arusha or singida pekeyao gani wakifanya hivyo tu wawe wamechokoza mzinga wa nyuki uchaguzi wote tz urudiwe na jk stoke tumexhoka huu upuuzi!
 
Hizo ni propaganda.CCM wanaweweseka sana tu.Kwa kupima tu je nguvu ya umma ipo Arumeru au kwa Lema.Yani kwa ujumla hapo kulikuwa hamna kesi ya kujibu ni propaganda tu.Kama ulifwatilia hii kesi kulikuwa hamna cha maana zaidi ya Propaganda.Kwa ujumla katika kesi zote, aliyekalia kuti kavu ni Makongoro Mahanga.Yaani huyu fisadi wa Kura kesi ishamlalia halafu unaweza kuhonga vile vile ukaliwa kichwa ingawa umetoa hela zako.Kiistoria vitu vya underground havina mashiko.Tunajua kuwa kwa vyovyote vile Arusha mjini ni ya CDM.Hata kama mafisadi walishatoa hongo ila kwa nguvu walioionyesha Arumeru na kushindwa ni dhahiri kwa Lema hawana lao.
 
Kumeibuka tetesi kwamba, hukumu ya kesi ya Mh.Godbless Lema, inaweza kutenguliwa kwakuwa hakimu wa Hiyo kesi amepewa Mshiko mzito na kundi la Mafisadi, ili kana kwamba kurudiwa kwa uchaguzi mdogo na kurirejesha jimbo la Arusha mjini kwa CCM..!

Napenda nijiulize kwanini EL na kundi lake hawajifunzi, kwani arumeru walijidanya wakitumia Washili watachukua jimbo kirahisi (wazee wa kimeru), na vile vile kwakuwa Sumari ni Ukoo mkubwa

Na sasa Arusha Mjini, wamategemea nini kama vijijini tu arumeru kuliwashinda,,kwasababu kwa kifupi tu. CCM hawakubaliki sehemu za Mijini..,na vile vile kutenguliwa kwa ubunge arusha mjini kutaongeza chuki dhidi ya CCM, watu watachagua tu CHADEMA kwa hasira kutokana na mazingira ya kesi yenyewe! na CCM itaendelea kuangamia kisiasa..!

Hata kama wakitumia hoja, eti CHADEMA wameharibu uchumi wa Arusha na kuufanya mji wa vurugu, tukicheki kwa makini, ni nani anayeamuru Polisi kupiga mabomu wananchi kama sio serikali ya CCM kwasababu wajibu wa polisi ni kulinda raia bali sio kupiga na kuwanyanyasa wananchi, na nani ambaye anayesababisha Uchumi wa Arusha kuwa mgumu kama sio Serikali ya CCM..! kwasababu Serikali ya CCM ndio ina dhamana ya kusimamia Uchumi kwa ujumla nchini ina mamlaka dhidi ya BOT,Wizara ya Fedha..,na mbunge tu hawezi kubadilisha huo mfumo.,

Kama ukitaka kuamini CCM hawana akili, wanaona madaraka ni matamu zaidi kuliko Maslahi ya nchi, wako tayari kupiga mabomu wananchi Arusha mjini, ili kumkomoa Lema na CHADEMA, huku wakisahau Arusha ndio kitovu cha UTALII nchini..,baadaye wasije kujiuliza kwanini Idadi ya watalii imepungua nchini...najua watailaumu CHADEMA,..lakini wajue CHADEMA ndio sauti ya wengi..kwahyo itakuwa ni sawa na kuwalaumu wananchi kiujumla ambao wameichoka serikali ya CCM na kuichagua CHADEMA kwa maendeleo na demokrasia ya Kweli..!

Napenda niseme, ndg.Nape Mnauye..katibu CCM-Uenezi, naamini katika CCM wengi ww ndio unaakili, upo critical na unique, kishauri chama chako kiachane na suala la Arusha...,mjipange tu paka 2015..,ni sawa sawa na kumlazimisha msichana umuoe wakati ana mimba ya mwanaume mwingine na kashachumbiwa na huyo mwanaume!

Sasa hivi kazi yenu ni moja tu..,kukisafisha chama na kuwafunga wale paka wawili kengele (mafisadi wawili waliobakia baada ya yule mmoja kujivua gamba) nadhani unawajua
 
Ccm nikama kichwa cha mwenda wazimu wanauona ukweli lakini hawataki kuukubali ukweli.
kwanza wasijaribu kabisa kumuingilia mbunge wetu kwani naamini hapo Arusha itatokea vita ambayo haijawahi tokea katika historia ya nchi hii.
chonde chonde enyi ccm msijaribu wala kufikiria hii kitu mtajajuta kumbukeni Arusha si yenu tena.
 
ccm wanasumbuka nisawa na mtu anaye zama kwenye maji hudiriki kushika maji ili ajiokoe kumbe maji hashikiki anazama chdema ni maji hashikiki ,ni moto wa mbugani
 
Baada ya matokeo ya Arumeru Mashariki sidhani kama kuna Mwana CCM yeyote ana hamu tena by election, tena kwa JIMBO HOT kama la Arusha MJINI labda kama ingekuwa huko BUBUBU.

I believe Jaji atatenda HAKI hakuna haja ya ku-panick, hata kama CCM walikuwa wame plan DIRTY tricks baada ya matokeo ya Arumeru watakuwa wamepiga ABOUT TURN, si Dr. Baltirida Burian atapenda tena kupanda jukwaani Arusha.
 
weita mwongezee bia mleta habari.mpe na supu ya kongoro na ndizi mbili. Bili kwangu.
 
unajua hawa magamba wanazani wao wanajua siasa sana,kinachofanyika hapa nikutaka kupenyeza hizi habari masikioni mwa watu ili zizoeleke ,kusudi wakichakachua hukumu umma usishtuke,hakuna chochote,harafu kwann utuletee habari za baa?hizo niza f.book
 
inaonekana aibu waloipata huko Arumeru haikuwatosha , basi sasa wasubiri aibu nyingine kubwa huko arusha mjini, chadema hata ikimsimamisha mtoto ashindane na magamba, pale arusha, bado mtoto atapita tu!!!!
 
Wanauona ukweli lakini hawataki kuukubali ukweli

Ccm nikama kichwa cha mwenda wazimu wanauona ukweli lakini hawataki kuuona ukweli.
kwanza wasijaribu kabisa kumuingilia mbunge wetu kwani naamini hapo Arusha itatokea vita ambayo haijawahi tokea katika historia ya nchi hii.
chonde chonde enyi ccm msijaribu wala kufikiria hii kitu mtajajuta kumbukeni Arusha si yenu tena.
 
Aisee nahisi ntakuja Arusha na SNIPER yangu km ni kweli CCM na EL wamehonga basi na wao wataondoka kimtindo huo. JINO KWA JINO PAMBAF!!! hakuna mwenye hati miliki na hii nchi
 
Inavyoonekana hakuna hata mmoja wenu aliekoment anyejua uhuru wa mahakama nini, mahakama haihukumu kishabiki, wala usitegemee unachokiwaza pekee kitendeke ndio uone kuwa haki imetendeka. Mimi binafsi nilikuwa nahudhuria mikutano ya uchaguzi ya Lema, hakuna kampeni za kipuuzi na kihuni kama zake. This guy hafai kuongoza hata kundi la machizi. Tokea kaingia madarakani what did he do mpaka sasa, kuna kilichoongezeka hapo mjini arusha zaidi ya kupungua kwa watalii kutokana na siasa chafu alizoziendesha yeye, hakuna haja ya kukumbatia watu kama yeye wanaotuletea hasara badala ya faida, uhuni hauna nafasi kwa nchi ya wastaarabu kama hii. Wote tunapenda mabadiliko lakini si katika hali ya kihuni, tufuate utaratibu na kufanya siasa safi sio CDM au CCM au CUF. Tunahitaji sera na si uhuni. Sitashangaa Lema akishinda au akishindwa kwani moja wapo kati ya hayo lazima yatokee na mahakama itakuwa imetenda haki. Kusema kuwa Jaji kapokea rusha this statement is baseless and ungrounded..huwezi niambia jaji kama huyu mwenye uzoefu apokee rushwa kwa kesi kama hiii ambayo jamii nzima wanasubiri matokeo yake, judiciary pia kabla ya kuteua majaji wanaangalia sifa za jaji na uzito wa kesi. Stori za baa hazina nafasi mahali hapa, kaongeeni na walevi wenzenu huko baa.
 
Mkuu,
Hicho ni kizazi kilicholelewa kwa kufundishwa woga! Hawajiamini na wamekuwa kama Mbwa koko. Muda wote mkia ...... Hata m/kiti wa mtaa/kitongoji ni kama Mungu kwao. Wanakuwa moulded kwamba ukitaka maisha yako yaende vizuri lazima uisapoti ccm! Ni vigumu kuwa kuamini jaji anaweza kutenda haki. Wanachojua ni kwamba maisha yanaenda kwa kutelekeza matakwa ya ccm!
Naamini mafuriko ya mageuzi yatawazoa na kuwabadilisha maana ukijaribu kuwaelimisha watabaki wanakushangaa wewe ni wa wapi, na huijui tz!
Mkuu Filipo

Kuna watu huwa hawaamini kuwa wanaweza kuishi bila CCM yaani maisha yao wameyaweka CCM kwa asilimia 100. Nafikiri kuna baadhi hata wana JF huwa hawachambui mada za kuikosoa serikali na CCM kwa kuogopa kujulikana, ni upuuzi na ujinga.

Tumeona kwenye uchaguzi wa AM walikuwa wanasema kwa CCM chochote kinaweza kufanyia wameiaminisha CCM kama Mungu wao kwamba inaweza hata kuwatabiria siku yao ya kufa. Kwenye kesi ya Lema kama mtu ulikuwa unafuatilia vizuri sioni kesi hapo lakini still watu wanajiaminisha CCM wanaweza kupindua au kuinunua mahakama, yes, kuna vitu vya kupindua lakini hawawezi kupindua kila kitu hata kilicho obvious kama kura za Nassari.

Guys, CCM is not everything relax have fun, mbona wengine tunaishi vizuri tu na CCM hiyo hiyo tena ndani kabisa bila wasiwasi na bila pressure?
 
Back
Top Bottom