Jairo kwenye Jarida la the Forbes

Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
7,237
9,871
we acha tupunguze hasira za akina jairo kujilipa allowance za kufa mtu, tugeukie kwenye orodha ya matajiri vinara 40 kutoka Afrika waliotajwa na jarida la Forbes siku nne zilizopita. Jamaa kutoka Nigeria Bw. Aliko Dangote anaongoza, pia katika orodha hiyo yupo mKenya na mZimbabwe...hapo Zimbabwe mnajifunza nini Watanganyika wenzangu? Hakuna Mtanzania hata mmoja hata!....Wakati Jairo anaiba wewe chapa kazi tu,amini utaingia kwenye the Forbes
 
Mh! Watanzania utajiri wao hauwekwi wazi, kwani vyanzo vyake havijulikani. Mara nyingi unakuta ni utajiri wa deals
 
hata kama sio wa deals,watanzania huwa tuna phobia ya kuitwa tajiri...labda kumbukumbu za Nyerere kuwaita matajiri(hata wale waliojituma na kufanikiwa )majina mabaya kv wanyonyaji, pia Mzee Sokoine na sera yake ya Wahujumu uchumi (wazee wawili kijijini kwetu walitelekeza gari mpya Isuzu roli tani 7 kisa walikosa kuandika mchanganuo wa jinsi walivyopata gari lile!)
 
Bora umeliona hilo. Nimeshangaa watu wanavyochangia wakati Heading na content haziendani!!
Sorry kwani unatakiwa uchangie title au content!? I think kaiweka title hivyo ili avutie watu waifungue thread yake
 
Rudi shule ukajifunzi uandishi. Jinsi ya kuoanisha heading na content ya habari yako. Sio unakurupuka kama mtoto wa shule ya msingi.
 
Rudi shule ukajifunzi uandishi. Jinsi ya kuoanisha heading na content ya habari yako. Sio unakurupuka kama mtoto wa shule ya msingi.

nafanya utafiti juu ya tabia ya watu kushobokea headings...mbona watanzania wengi tunapenda kusoma udaku?
 
Unafaa kufanya kazi kwenye magazeti ya udaku kwenye section ya headlines making
Maana heading na ulichoandika no correlation.
Jipange ulete maada ingine
 
we acha tupunguze hasira za akina jairo kujilipa allowance za kufa mtu, tugeukie kwenye orodha ya matajiri vinara 40 kutoka Afrika waliotajwa na jarida la Forbes siku nne zilizopita. Jamaa kutoka Nigeria Bw. Aliko Dangote anaongoza, pia katika orodha hiyo yupo mKenya na mZimbabwe...hapo Zimbabwe mnajifunza nini Watanganyika wenzangu? Hakuna Mtanzania hata mmoja hata!....Wakati Jairo anaiba wewe chapa kazi tu,amini utaingia kwenye the Forbes

Miaka 10 ijayo mimi nitakuwemo, i promise
 
Unashangaa Mzimbabwe kuwemo katika orodha ya watu 40 matajiri barani Afrika?!

binafsi nachukia hii tabia ya visingizio kama hivi:...thamani ya shilingi yazidi kushuka,ukosefu wa ajira n.k. Nimei-point zimbabwe kwa mkabala huo,hebu angalia thamani ya pesa zao, bado watu wanachapa kazi. Utaniuliza kupatikana mtu mmoja tajiri ndio kigezo?hapana sio kigezo ila ni ishara kwamba usivunjike moyo kwa sababu ya thamani ya hela,
 
Back
Top Bottom