Jairo asimamishwa kazi

Status
Not open for further replies.
Huu niuonezi wa wazi! Sikubaliani kabisa na uamuzi wa serikali....hivi Jairo alichokuwa anafanya sikilikuwa na baraka za waziri na naibu waziri wake? Iweje rungu limwangukie yeye? I hate Tanzania.

Mkuu unachosema ndio mawazo yangu na mimi pia, haiwezekani Katibu Mkuu ahonge wabunge bila Mawaziri wake kuwa na taarifa na kuridhia mpango huo!! inasikitisha sana mtu anaumbuliwa kwa jambo alilotumwa na watu wengine!! Niwazi kabisa kwamba Waziri na Naibu wake ndio wahusika wakuu kwenye sakata hili, nao pia washurutishwe kuachia ngazi- na hata kama wangekuwa hawajui, lakini si kuna suala la uwajibikaji? Jambo kubwa kama hili litokee chini ya himaya yake wala usitingishike! Sasa hii wizara ya utawala bora ya nini kama haiwezi kumshauri raisi kwenye mambo yaliyo wazi namna hii?
 
Ni usanii mtupu ndugu yangu unaofanywa na hii Serikali iliyojaa Mataahira katika kulinda maslahi yao binafsi badala ya Watanzania ambao tumewapa dhamana kubwa ya kutuongoza. Kila siku iendayo kwa Mungu madudu na uozo kibao!!!! :( :( :(

Usanii ulianzia pale MKP aliposema hana mamlaka naye. Sote tunajua kuwa huyu ni mteule wa rais lakini utendaji wa serikali uko mikononi mwa waziri mkuu na hasa ukizingatia kuwa ilikuwa ni shughuli za bunge ambazo yeye ndiye kiongozi wa shughuli za serikali bungeni. Alichopaswa ni kumsimamisha kazi kwanza ili kusubiri uamuzi /hatua zaidi kutoka kwa aliyemteua. Ila suala likageuzwa geuzwa kwa siku kibao eti leo ndo tunaambiwa kasimamishwa. Hapo tumeimbishwa.
 
Kasimamishwa kazi halafu badae atarudishwa kazini au inakuaje! Kosa si lipo wazi hii ya kusimamishwa kazi imetoka wapi tena, Pinda nae kumbe ulikuwa mkwala siku ile bungeni
 
Wanaongezea ile bilioni kwani tume nayo inataka mgawo wake, kuna nini cha kuchunguza hapo sasa. Hii nchi ni bora tuongozwe na wazungu sasa, pengine watakuwa hata na uchungu kidogo.
 
Mkuu ushahidi wa kitu gani, au kwenye ile barua kulikuwa na kitu gani cha ajabu ili kitumike kama ushahidi, ni mbunge gani aliyepewa rushwa...kama kuna mbunge aliyepewa rushwa ajitokeze.

chloroform in action
 
Wachunguze 'upitishaji' wa budget kwa wizara zote sio hii ya Nishati na Jairo peke yake.
Barua yake Jairo ya mchango imetumia maneno "kama ilivyo kawaida" what kawaida?

Wakifanya hivyo timbwili lake si kidogo. Nahisi ajira mpya za ma PS zitatengenezwa. "Kama ilivyo kawaida" hahahaha hakuna aliye salama hapo
 
Breaking news,hivi punde Katibu wa wizara ya nishati na madini Bwana,David Jairo amesimamishwa kazi,taarifa hiyo imetolewa na katibu mkuu kiongozi philemon Luhanjo ,amesimamishwa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma anazokabiriwa nazo.source ITV breaking news.
Mwisho wa uchunguzi tutaambiwa hana hatia, kazi mwendo mdundo, na mpaka hapo itaonesha kuwa Wabunge walioibua sakata lile ndo wanaleta maneno mingi ya uongo!! Sasa sijui kanuni na mwongozo vitatumika? Na hizo hela zitarudishwa kwenye idara au ndo zilisharudishwa?
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo amesimaishwa kazi! Akiongea na waandishi wa habari mjini Dodoma mapema leo, Katibu Mkuu Kiongozi, Philomon Luhanjo, alisema kuwa Jairo amesimamishwa kazi kuanzia kesho ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili zilizotolewa bungeni…mapema wiki hii. Jairo anatuhumiwa kuandika barua ya kuchangisha fedha milioni 50 kwa idara 20 ili zitumike kushawishi wabunge wapitishe bajeti ya wizara yake. Haijaelezwa amesimamishwa kwa muda gani.

MY TAKE:
NGELEJA..MALIMA ...??????????????????

 
Hiviee..kapewa likizo ya malipo!

Na hii tuiingize humu JF yani upewe BAN with benefits...
Unaweza kucomment on other forums except ile uliyotukana/vunja sheria.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom