J. Samwel Malecela ni mgonjwa

Dunia ya sasa ni vigumu sana kumchagulia mtu sehemu anayohitaji kupata huduma. Huu ni ulimwengu wa kibepari, mteja anafuata panapomfaa. Pamoja na hayo Mh. Malecela ni mmoja wa mawaziri wakuu wastaafu, nadhani ana stahili anazopokea ambazo zinamwezesha kutibiwa nje

Sina shaka gharama ya matibabu imebebwa na serikali kwa asilimia 100 kwa kuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu, hivyo hoja ya kutibiwa Muhimbili iko pale pale. Kama serikali imedhamiria kupunguza matumizi makubwa yasiyo ya lazima ni muhimu kuepuka gharama kama hizi. Kama wapo Watanzania wamefanyiwa operation Muhimbili na matokeo ni mazuri kwa nini Malecela naye asifanyiwe hapo? Izingatiwe kwamba capacity building ya kuwezesha Muhimbili ilitumia fedha nyingi sana za walipa kodi lengo likiwa ni kuepusha gharama za kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi. Hapa ndipo unaweza kuona tofauti kati ya mlala hoi na asiye mlalahoi, tukumbuke kwamba maisha ni muhimu kwa kila mtu, je serikali inatoa fundisho gani kwa Watanzania? Kwamba kumbe pale Muhimbili ni kwa ajili ya akina fulani tu na viongozi wao waendelee kutibiwa nje ya nchi? Ule usemi kwamba binadamu wote ni sawa sasa umefia wapi? Je Muhimbili walishindwa kumfanyia opereation na kutoa rufaa kwenda nje au hata hapo Muhimbili hakukanyaga?
 
Samahani kama nitakuwa nimewaudhi, kwa nini hawa wanasiasa wetu hawatibiwi Muhimbili au Mwanayamala kama sisi wengine?

kwa nini watoto wa viongozi wa umma hawasomi shule za primary aka kayumba na zile za kata aka ngumbaro walizoziasisi wenyewe? kaa chini tafakari then chukua hatua.
 
Samahani kama nitakuwa nimewaudhi, kwa nini hawa wanasiasa wetu hawatibiwi Muhimbili au Mwanayamala kama sisi wengine?
Uko sawa Mkuu
Haa Mku uko sawa tu!
Lakini inaelekea hujawa circumcised, mimi daktari niliyesajiliwa njoo huku madongo kuinama nitakupatia huduma nzuri tu.
 
Back
Top Bottom